Hoja ya Edo Kumwembe kuhusu Serikali na upinzani

Kumbe wewe upo kutetea chadema. Hahaha hata Cuf na nccr vikiwahi kuwa vyama vikuu, subiri 2020 chama kikuu kitatangazwa yawezekana ccm au nrd
Wewe unatetea CCM na umetoa mfano wa Marekani na mie lazima niitetee chadema kama wewe ulivyosahau washirika wa CCM vile vyama vya kijinga jinga vya akina Dovutwa, Lipumba na genge lake yaani CUF waasi, Mrema, Cheyo na wenzao wengi.
 
Namkubali sana Edo Kumwembe , sio hapa tu hata Makala zake mwanasport Jicho la mwewe huwa anazipangilia vizuri sana kasema ukweli uliomchungu, huwezi kumuona magonjwa mtambuka, na kundi lao kuja kutia neno hapa, wanasoma tu na kupita.

Wapo lakini wapo Gheto kwa Le mutuz na cyprian Musiba wamelewa chakari hawana ujanja wa kuja jukwaani leo kwa sababu hata boss wao yupo bwiii ni vigumu kuja kuwasumbua watu jukwaani
 
Hili neno la pasaka.
Unawasha televisheni yako, unachukua kikombe cha chai, unasubiri uwekaji jiwe la msingi kwa ajili ya barabara nyingi Kimara. Huyu anatoa hotuba, yule anatoa hotuba, mwingine anatoa hotuba. Mpaka inafika zamu ya namba moja naye anatoa hotuba.
Ndani yake kuna vijembe vingi kwa watu wanaoitwa wapinzani. Kila aliyeongea anaweka dhamira ya kukejeli, kukashifu, kuponda watu wanaoitwa wapinzani. Unaishia kutabasamu. Adui yetu ni umaskini au wapinzani?
Unaposubiri hotuba za mapokezi ya ndege inakuwa hivyo hivyo. Bado unajiuliza swali lile lile, adui yetu ni umaskini au wapinzani? Hata kama wanaongea sana, bado adui yetu ni umaskini. Na siku tukiwa matajiri hakuna atakayeacha kupinga na kukosoa mwenendo wa nchi.
Marekani kuna wapinzani, mitume nao walipingwa. Bahati nzuri kwa watawala wetu ni kwamba wapinzani wetu wanaishia kuongea, hawana dola, hawakusanyi kodi. Wanabakia kuwa mbu wanaozunguka sikio ambao wanakukumbusha tu kwamba milango ipo wazi.
Katika hotuba muhimu, bosi wa mkoa anamkumbusha namba moja kwamba mwaka 2020 atamkabidhi wabunge na madiwani wote kutoka chama chake. Hii itaondoa umaskini? Kwa mfano, hili hata likifanyika nchi nzima, itasaidia kuondoa umaskini?
Kuna mambo ambayo namba moja anayafanya. Muhimu kweli. Huwa nafikiria yanalenga katika kutuondoa hapa tulipo kama Taifa. Ukisikiliza hotuba ya tukio zima unahisi kwamba lengo halikuwa kukabiliana na tatizo fulani bali kuwaonyesha watu kwamba wapinzani hawafai.
Hotuba zetu zinajaa majina ya vyama. Hauwezi kusikiliza hotuba ukakosa kusikia CCM, CHADEMA, CUF, UDP. Hakuna hotuba ambayo tunajadili maendeleo tu. Lazima yataingia majina ya vyama. Dhamira yetu ya kushindana kisiasa ni kubwa kuliko kushindana na umaskini.
Hii inanitia hofu. Tunaweza kusimama na kujadili maendeleo tu bila ya siasa? Kinachonisikitisha ni kwamba tatizo la upinzani ndani na nje ya vyama vyetu haliwezi kumalizika. Wanadamu wameumbwa kupinga au kutokubaliana. Ukitembea na hisia za kukataa hali hii muda wote unajipunguzia siku zako za kuishi.
Tukifanya maendeleo tukumbuke kuna Watanzania milioni 55. Waliopiga kura ni milioni 10, wasiopiga kura ni milioni 45 na wanalipa kodi. Habari ya kuzungumzia siasa katika kila mkutano unaohusu maendeleo inachosha. Tatizo letu kubwa ni umaskini sio upinzani.
Ningekuwa namba moja, mikutano ya uzinduzi wa barabara au mapokezi ya ndege nisingewaita CCM, CHADEMA, TLP, CUF wala chama chochote cha siasa badala yake ningewaita watendaji wa wizara na viongozi wa serikali tu.
 
Hahaha pay respect to Mrema ndiye alithubutu kuingia upinzani

Eddo yupo vizuri sana kwakweli,anajua kujenga hoja, nasikia anataka kugombea ubunge huko kwao kusini, Nadhani anafaa kabisa
 
Hoja ya kisi kabisa.lets do tje work tuache vijembe vya kutwa kusimanga wapinzani.Great writing edo.

Ukumbuke kuwa hakuna siasa wala mikutano mpaka wakati wa uchaguzi, tupate muda wa kufanya kazi.
No bunge live ni gharama.
 
Kwani hao chadema wametufanyia nini cha maana? Nao si genge la watu wachache wanaojinufaisha kwa kula pesa zetu za kodi kwa njia ya ruzuku tu!?

Wakati Nyerere analazimisha kuwatia wakoloni alikuwa amejenga barabara ngapi? Alikuwa amejenga reli yoyote ama kununua ndege yoyote?
 
Hujamjua vzr kabla hajajikita zaidi kwenye uandishi wa Michezo alikuwaga Habari Cooperation alikuwa anaandika Makala kwenye Gazeti la RAI NGUVU ya HOJA ungebahatika kumsoma huko usingeshangaa alichoandika leo
Magazeti ya RAI ya enzi za kina General Ulimwengu na mwenzake mzee Johnson Mwambo nimeyasoma sana. Ila sikumbuki kumwona Eddo akiandika makala za kisiasa.

Nawakumbuka.
1. Joseph Mihangwa
2. Ulimwengu
3. Mwambo
4. Lula wa ndali Mwananzela
5. Prince Bagenda
6. Ahamed Rajab
7. Na yule jamaa wa iringa mwenye kablog kake.
 
Adui wa kwanza ni upinzani.
Adui wa pili ccm wachumia tumbo.
Adui wa tatu umaskini.
Nikipata madaraka naanza kufuta upinzani TZ, then ccm wachumia tumbo, then umaskini.
SIPANGIWI.
Akili yako na john walker hazina tofauti
 
Huenda kaandikiwa na wajanja zaidi kwani mwandishi ni mtu mjanja anayejielewa asiye na Akili za kishamba kama za Cyprian Musiba na Le mutuz
Ampe tu acknowledgement... Ujumbe maridadi sana huu.
 
Wapo lakini wapo Gheto kwa Le mutuz na cyprian Musiba wamelewa chakari hawana ujanja wa kuja jukwaani leo kwa sababu hata boss wao yupo bwiii ni vigumu kuja kuwasumbua watu jukwaani
Wapo wanaringishiana vibamia vyao tu.
 
CCM haipo kuleta maendeleo na wala haimini kwenye maendelo.. CCM ipo kwa ajili ya kutawala na huwezi kuitoa madarakani kwa box la kura wala diplomasia huo ndio ukweli..
 
Hii itakuwa makala ya pili ya Eddo Kumwembe kuisoma. Eddo kaacha uchambuzi wa soka sasa kaingia kwenye siasa?

Ila kasema kweli...
Eddo hajaanza Jana wala Leo kuchambua siasa.. Alikuwa akichambua mpira na siasa pia tangu awamu ya tatu ya mkapa.
 
Sio mbaya, lakini amesahau kuwa anaemzunguzia ni mwanasiasa... Anaishi katika siasa so yale anayoyafanya na kuyaongea ni sehemu ya kazi yake iliyomfanya afike pale, Siasa
Ni kweli mkuu, na hata serikali anayoongoza imetokana na siasa za chama tawala kinachounda serikali.. Lakini pia kwa upande mwingine Eddo yupo sahihi kwa uchambuzi wake.
 
Back
Top Bottom