Hoja ya Edo Kumwembe kuhusu Serikali na upinzani

Nyerere anahusika vipi na ukondoo wa watanzania waleo? Mwandishi aniceth mihambo anasema huo ni uvivu wa kufikiri ni sawa na wafrika wengine wanao tulaumu sisi wakoloni wakizungu kwa ugumu wa maisha yao wakati tulishawapa uhuru watu kama hawa wala si wa kuhurumiwa.
Nisome vizuri utaelewa. Na amini hapo juu umeandika kuwa watanzania wa leo wana ukondoo. Pia nimesema "Ukondoo huo" hurisishwa. Hujasikia kwa mfano kuna watu bado wanatimiza ndoto za Nyerere?
 
Hata mawazo yake bahati mbaya yataonekana ya uchochezi
 
ameandika maneno mazuri.
nadhani wapinzani wangekuwa wamewahi kutawala japo awamu Moja, mzigo wote wa watanzania wangebebeshwa.
Wakuu wetu wajikite kwenye maendeleo, wapinzani wawaachie wananchi kwenye box la kura.
Nawew umeandika vyema kabsa ila hapo mwshoni unavyosema wananch waachiwe kwenye sanduku la kura..unakosea sana na unakuwa mnafk sana...maana unajua waz Uchaguzi miaka yote si huru na haki na kikubwa kuna madai ya Tume Huru ya Uchaguz...hembu changia hili la. Tume huru ya uchaguzi,ili mchango wako uwe na uzani sawa
 
mkuu tangu nimeanza kufuatilia siasa za vyama vingi 1995 hadi juzi 2015 sijawahi kuona popote mitandaoni, au kwa wanasiasa wanaolalamika, au kesi mahakamani hasa uchaguzi wa Rais ukionyesha jinsi walivyoibiwa.
Kuhusu Tume kuwa huru naunga mkono, inapaswa kuwa huru zaidi ya hapo kama wadau wa siasa wanavyopendekeza, ila sijawahi kuona ushahidi wa wizi wa kura zaidi ya maneno kuwa kura zimeibiwa. kama uzi umo humu nisogezee mkuu.
 
Kule Israel kulikuwa na yohana mbatizaji hapa tuna yohana muuaji
 
Unawasha televisheni yako, unachukua kikombe cha chai, unasubiri uwekaji jiwe la msingi kwa ajili ya barabara nyingi Kimara. Huyu anatoa hotuba, yule anatoa hotuba, mwingine anatoa hotuba. Mpaka inafika zamu ya namba moja naye anatoa hotuba.
Ndani yake kuna vijembe vingi kwa watu wanaoitwa wapinzani. Kila aliyeongea anaweka dhamira ya kukejeli, kukashifu, kuponda watu wanaoitwa wapinzani. Unaishia kutabasamu. Adui yetu ni umaskini au wapinzani?
Unaposubiri hotuba za mapokezi ya ndege inakuwa hivyo hivyo. Bado unajiuliza swali lile lile, adui yetu ni umaskini au wapinzani? Hata kama wanaongea sana, bado adui yetu ni umaskini. Na siku tukiwa matajiri hakuna atakayeacha kupinga na kukosoa mwenendo wa nchi.
Marekani kuna wapinzani, mitume nao walipingwa. Bahati nzuri kwa watawala wetu ni kwamba wapinzani wetu wanaishia kuongea, hawana dola, hawakusanyi kodi. Wanabakia kuwa mbu wanaozunguka sikio ambao wanakukumbusha tu kwamba milango ipo wazi.
Katika hotuba muhimu, bosi wa mkoa anamkumbusha namba moja kwamba mwaka 2020 atamkabidhi wabunge na madiwani wote kutoka chama chake. Hii itaondoa umaskini? Kwa mfano, hili hata likifanyika nchi nzima, itasaidia kuondoa umaskini?
Kuna mambo ambayo namba moja anayafanya. Muhimu kweli. Huwa nafikiria yanalenga katika kutuondoa hapa tulipo kama Taifa. Ukisikiliza hotuba ya tukio zima unahisi kwamba lengo halikuwa kukabiliana na tatizo fulani bali kuwaonyesha watu kwamba wapinzani hawafai.
Hotuba zetu zinajaa majina ya vyama. Hauwezi kusikiliza hotuba ukakosa kusikia CCM, CHADEMA, CUF, UDP. Hakuna hotuba ambayo tunajadili maendeleo tu. Lazima yataingia majina ya vyama. Dhamira yetu ya kushindana kisiasa ni kubwa kuliko kushindana na umaskini.
Hii inanitia hofu. Tunaweza kusimama na kujadili maendeleo tu bila ya siasa? Kinachonisikitisha ni kwamba tatizo la upinzani ndani na nje ya vyama vyetu haliwezi kumalizika. Wanadamu wameumbwa kupinga au kutokubaliana. Ukitembea na hisia za kukataa hali hii muda wote unajipunguzia siku zako za kuishi.
Tukifanya maendeleo tukumbuke kuna Watanzania milioni 55. Waliopiga kura ni milioni 10, wasiopiga kura ni milioni 45 na wanalipa kodi. Habari ya kuzungumzia siasa katika kila mkutano unaohusu maendeleo inachosha. Tatizo letu kubwa ni umaskini sio upinzani.
Ningekuwa namba moja, mikutano ya uzinduzi wa barabara au mapokezi ya ndege nisingewaita CCM, CHADEMA, TLP, CUF wala chama chochote cha siasa badala yake ningewaita watendaji wa wizara na viongozi wa serikali tu.
Fatilia elimu yamakonda jibu tunalo apuuzwe, baba yake taaluma yake imekula mtu, wakulaumiwa WA awamu yatatu..2020 twende mtaaluma mwenye taaluma isiyo na magumashi membe
 
Very good article

Thanks Edo Lutengano sec school product
Namshanga John wamtwara pekeake waliosoma shule zairinga wako makin Sana, huyu atakua muda mwingi akishinda kiwele kwenye maulazi kule.....
 
Unawasha televisheni yako, unachukua kikombe cha chai, unasubiri uwekaji jiwe la msingi kwa ajili ya barabara nyingi Kimara. Huyu anatoa hotuba, yule anatoa hotuba, mwingine anatoa hotuba. Mpaka inafika zamu ya namba moja naye anatoa hotuba.
Ndani yake kuna vijembe vingi kwa watu wanaoitwa wapinzani. Kila aliyeongea anaweka dhamira ya kukejeli, kukashifu, kuponda watu wanaoitwa wapinzani. Unaishia kutabasamu. Adui yetu ni umaskini au wapinzani?
Unaposubiri hotuba za mapokezi ya ndege inakuwa hivyo hivyo. Bado unajiuliza swali lile lile, adui yetu ni umaskini au wapinzani? Hata kama wanaongea sana, bado adui yetu ni umaskini. Na siku tukiwa matajiri hakuna atakayeacha kupinga na kukosoa mwenendo wa nchi.
Marekani kuna wapinzani, mitume nao walipingwa. Bahati nzuri kwa watawala wetu ni kwamba wapinzani wetu wanaishia kuongea, hawana dola, hawakusanyi kodi. Wanabakia kuwa mbu wanaozunguka sikio ambao wanakukumbusha tu kwamba milango ipo wazi.
Katika hotuba muhimu, bosi wa mkoa anamkumbusha namba moja kwamba mwaka 2020 atamkabidhi wabunge na madiwani wote kutoka chama chake. Hii itaondoa umaskini? Kwa mfano, hili hata likifanyika nchi nzima, itasaidia kuondoa umaskini?
Kuna mambo ambayo namba moja anayafanya. Muhimu kweli. Huwa nafikiria yanalenga katika kutuondoa hapa tulipo kama Taifa. Ukisikiliza hotuba ya tukio zima unahisi kwamba lengo halikuwa kukabiliana na tatizo fulani bali kuwaonyesha watu kwamba wapinzani hawafai.
Hotuba zetu zinajaa majina ya vyama. Hauwezi kusikiliza hotuba ukakosa kusikia CCM, CHADEMA, CUF, UDP. Hakuna hotuba ambayo tunajadili maendeleo tu. Lazima yataingia majina ya vyama. Dhamira yetu ya kushindana kisiasa ni kubwa kuliko kushindana na umaskini.
Hii inanitia hofu. Tunaweza kusimama na kujadili maendeleo tu bila ya siasa? Kinachonisikitisha ni kwamba tatizo la upinzani ndani na nje ya vyama vyetu haliwezi kumalizika. Wanadamu wameumbwa kupinga au kutokubaliana. Ukitembea na hisia za kukataa hali hii muda wote unajipunguzia siku zako za kuishi.
Tukifanya maendeleo tukumbuke kuna Watanzania milioni 55. Waliopiga kura ni milioni 10, wasiopiga kura ni milioni 45 na wanalipa kodi. Habari ya kuzungumzia siasa katika kila mkutano unaohusu maendeleo inachosha. Tatizo letu kubwa ni umaskini sio upinzani.
Ningekuwa namba moja, mikutano ya uzinduzi wa barabara au mapokezi ya ndege nisingewaita CCM, CHADEMA, TLP, CUF wala chama chochote cha siasa badala yake ningewaita watendaji wa wizara na viongozi wa serikali tu.
Exactly!!
 
mkuu tangu nimeanza kufuatilia siasa za vyama vingi 1995 hadi juzi 2015 sijawahi kuona popote mitandaoni, au kwa wanasiasa wanaolalamika, au kesi mahakamani hasa uchaguzi wa Rais ukionyesha jinsi walivyoibiwa.
Kuhusu Tume kuwa huru naunga mkono, inapaswa kuwa huru zaidi ya hapo kama wadau wa siasa wanavyopendekeza, ila sijawahi kuona ushahidi wa wizi wa kura zaidi ya maneno kuwa kura zimeibiwa. kama uzi umo humu nisogezee mkuu.
Mkuu huwez sikia kesi wala mashtaka yoyote maana sheria znasema Tume ndio mtangazaj wa mwsho wa matokeo na HAYATAPINGWA popote pale hata kama n mahakamani..
Hv hili nalo hulijui au ndio unazuga kwa kuwa ww ssm
 
hata kabla ya kutangazwa. sijawahi kuona uthibitisho usio na shaka mkuu.
nilimfuatilia maana huwa wanatuhumu kila chaguzi, ila ushahidi wa tuhuma zile huwa ni hafifu kuliko hata majibu ya tume hiyo isiyo huru.
naomba mfano, au ule wa makontena ya Kura ya Dr Slaa?
 
Back
Top Bottom