Hoja ya Edo Kumwembe kuhusu Serikali na upinzani

Unawasha televisheni yako, unachukua kikombe cha chai, unasubiri uwekaji jiwe la msingi kwa ajili ya barabara nyingi Kimara. Huyu anatoa hotuba, yule anatoa hotuba, mwingine anatoa hotuba. Mpaka inafika zamu ya namba moja naye anatoa hotuba.
Ndani yake kuna vijembe vingi kwa watu wanaoitwa wapinzani. Kila aliyeongea anaweka dhamira ya kukejeli, kukashifu, kuponda watu wanaoitwa wapinzani. Unaishia kutabasamu. Adui yetu ni umaskini au wapinzani?
Unaposubiri hotuba za mapokezi ya ndege inakuwa hivyo hivyo. Bado unajiuliza swali lile lile, adui yetu ni umaskini au wapinzani? Hata kama wanaongea sana, bado adui yetu ni umaskini. Na siku tukiwa matajiri hakuna atakayeacha kupinga na kukosoa mwenendo wa nchi.
Marekani kuna wapinzani, mitume nao walipingwa. Bahati nzuri kwa watawala wetu ni kwamba wapinzani wetu wanaishia kuongea, hawana dola, hawakusanyi kodi. Wanabakia kuwa mbu wanaozunguka sikio ambao wanakukumbusha tu kwamba milango ipo wazi.
Katika hotuba muhimu, bosi wa mkoa anamkumbusha namba moja kwamba mwaka 2020 atamkabidhi wabunge na madiwani wote kutoka chama chake. Hii itaondoa umaskini? Kwa mfano, hili hata likifanyika nchi nzima, itasaidia kuondoa umaskini?
Kuna mambo ambayo namba moja anayafanya. Muhimu kweli. Huwa nafikiria yanalenga katika kutuondoa hapa tulipo kama Taifa. Ukisikiliza hotuba ya tukio zima unahisi kwamba lengo halikuwa kukabiliana na tatizo fulani bali kuwaonyesha watu kwamba wapinzani hawafai.
Hotuba zetu zinajaa majina ya vyama. Hauwezi kusikiliza hotuba ukakosa kusikia CCM, CHADEMA, CUF, UDP. Hakuna hotuba ambayo tunajadili maendeleo tu. Lazima yataingia majina ya vyama. Dhamira yetu ya kushindana kisiasa ni kubwa kuliko kushindana na umaskini.
Hii inanitia hofu. Tunaweza kusimama na kujadili maendeleo tu bila ya siasa? Kinachonisikitisha ni kwamba tatizo la upinzani ndani na nje ya vyama vyetu haliwezi kumalizika. Wanadamu wameumbwa kupinga au kutokubaliana. Ukitembea na hisia za kukataa hali hii muda wote unajipunguzia siku zako za kuishi.
Tukifanya maendeleo tukumbuke kuna Watanzania milioni 55. Waliopiga kura ni milioni 10, wasiopiga kura ni milioni 45 na wanalipa kodi. Habari ya kuzungumzia siasa katika kila mkutano unaohusu maendeleo inachosha. Tatizo letu kubwa ni umaskini sio upinzani.
Ningekuwa namba moja, mikutano ya uzinduzi wa barabara au mapokezi ya ndege nisingewaita CCM, CHADEMA, TLP, CUF wala chama chochote cha siasa badala yake ningewaita watendaji wa wizara na viongozi wa serikali tu.
Hoja makini sana!
 
Sio mbaya, lakini amesahau kuwa anaemzunguzia ni mwanasiasa... Anaishi katika siasa so yale anayoyafanya na kuyaongea ni sehemu ya kazi yake iliyomfanya afike pale, Siasa
 
Kila mtu ana vipa umbele vyake, lakini vya wanasiasa vinatisha. Wanatumia raslimali za umma na muda wetu wananchi kufanikisha mambo yao, wakituhadaa, na kwa ujinga wetu wananchi tukiamini ni kwa manufaa yetu.
 
Tatizo Awamu ya 5 wamejazana wajinga toka utosini hadi unyayo...kichwa kilipokuja kimejaa tope akina bashite nao wakajaa tope!
 
Eddo amewakilisha mawazo yetu tusio wanachama wa vyama vya siasa. Asante sana Eddo.

Vv
 
Haya Edo, bado tunazihitaji makala za Michezo...hii serikali haina huo uvumilivu unaofikiri...ngoja wazuie viza ya kwenda kuchambua mpira SA ndio utajua hii serikali ya aina gani.
Sio kuzuia viza bali kumnyang'anya passport ili kuuchunguza uraia, anaonekana kama mtu wa Msumbiji vile! Nchi hii tumefikia mahali ukitoa hata mawazo mazuri kiasi gani, yakipingana na wanachotaka kusikia wanakutafutia zengwe.

Vv
 
Hujamjua vzr kabla hajajikita zaidi kwenye uandishi wa Michezo alikuwaga Habari Cooperation alikuwa anaandika Makala kwenye Gazeti la RAI NGUVU ya HOJA ungebahatika kumsoma huko usingeshangaa alichoandika leo
Hii itakuwa makala ya pili ya Eddo Kumwembe kuisoma. Eddo kaacha uchambuzi wa soka sasa kaingia kwenye siasa?

Ila kasema kweli...
 
Kaandika vizuri sana lakini wasio na akili hawatamuelewa.!
 
unakimbia bajeti za sheree sijui ya uhuru na n.k una kubali bajeti ya kila uzinduzi kwa hisani ya ccm
Chizcom ndg yangu siyo mbio zote zina lengo la kushinda mashindano zingine ni za kuokoa maisha, aibu, kutoroka nk.
 
Huko nyuma tulifundishwa kuwa maadu watatu ni
1.Ujinga
2.Maradhi.
3.Umaskini
Lakini tulifundishwa pia kuwa ili tuendelee tunahitaji mambo makuu manne.
1.Watu
2.Ardhi
3.Siasa Safi
4.Uongozi Bora
Nikianzia hapo juu kwa maadui wakuu watatu,bado wapo,kwani ukishakuwa mjinga utakaribisha maradhi,na maradhi yakiingia yataleta umaskini.
Kwenye suala la maendeleo watu tunao na ardhi ipo ya kutosha,
Tatizo lipo kwenye Siasa safi na uongozi bora,
Nihitimishe kwa kusema kuwa maadui wetu watatu yaani ujinga,maradhi na umaskin ivinasababishwa na ukosefu wa siasa safi na uongozi bora.
 
Maneno ya Busara sana,

Huu waraka alitakiwa haraka sana

Edo atunukiwe PhD ya heshima Kwenye Sayansi ya Siasa Endelevu.
 
[emoji24] [emoji24] [emoji116]
tapatalk_1544853514742.jpeg
 
Sio mbaya, lakini amesahau kuwa anaemzunguzia ni mwanasiasa... Anaishi katika siasa so yale anayoyafanya na kuyaongea ni sehemu ya kazi yake iliyomfanya afike pale, Siasa
Ila Kazuia mikutano ya Siasa,

Kwamba
"mda wa siasa umekwisha, tufanye kazi"

Cha ajabu Yeye anafanya Siasa.
 
Back
Top Bottom