Hoja ya Edo Kumwembe kuhusu Serikali na upinzani

Hoja ya Edo Kumwembe kuhusu Serikali na upinzani

Adui wa kwanza ni upinzani.
Adui wa pili ccm wachumia tumbo.
Adui wa tatu umaskini.
Nikipata madaraka naanza kufuta upinzani TZ, then ccm wachumia tumbo, then umaskini.
SIPANGIWI.
Ukifuta upinzani Bado kupingwa kupo pale pale Ni kitu Cha asili ya mwanadamu hata mitume waliotumwa na Mungu walipingwa
 
Ukifuta upinzani Bado kupingwa kupo pale pale Ni kitu Cha asili ya mwanadamu hata mitume waliotumwa na Mungu walipingwa
Shetani siyo jina lake la asili,alipompinga Mungu nikapatikana jina la shetani. Kwa mfano huu ujuwe upinzania haukuanza Leo.
 
Unawasha televisheni yako, unachukua kikombe cha chai, unasubiri uwekaji jiwe la msingi kwa ajili ya barabara nyingi Kimara. Huyu anatoa hotuba, yule anatoa hotuba, mwingine anatoa hotuba. Mpaka inafika zamu ya namba moja naye anatoa hotuba.
Ndani yake kuna vijembe vingi kwa watu wanaoitwa wapinzani. Kila aliyeongea anaweka dhamira ya kukejeli, kukashifu, kuponda watu wanaoitwa wapinzani. Unaishia kutabasamu. Adui yetu ni umaskini au wapinzani?
Unaposubiri hotuba za mapokezi ya ndege inakuwa hivyo hivyo. Bado unajiuliza swali lile lile, adui yetu ni umaskini au wapinzani? Hata kama wanaongea sana, bado adui yetu ni umaskini. Na siku tukiwa matajiri hakuna atakayeacha kupinga na kukosoa mwenendo wa nchi.
Marekani kuna wapinzani, mitume nao walipingwa. Bahati nzuri kwa watawala wetu ni kwamba wapinzani wetu wanaishia kuongea, hawana dola, hawakusanyi kodi. Wanabakia kuwa mbu wanaozunguka sikio ambao wanakukumbusha tu kwamba milango ipo wazi.
Katika hotuba muhimu, bosi wa mkoa anamkumbusha namba moja kwamba mwaka 2020 atamkabidhi wabunge na madiwani wote kutoka chama chake. Hii itaondoa umaskini? Kwa mfano, hili hata likifanyika nchi nzima, itasaidia kuondoa umaskini?
Kuna mambo ambayo namba moja anayafanya. Muhimu kweli. Huwa nafikiria yanalenga katika kutuondoa hapa tulipo kama Taifa. Ukisikiliza hotuba ya tukio zima unahisi kwamba lengo halikuwa kukabiliana na tatizo fulani bali kuwaonyesha watu kwamba wapinzani hawafai.
Hotuba zetu zinajaa majina ya vyama. Hauwezi kusikiliza hotuba ukakosa kusikia CCM, CHADEMA, CUF, UDP. Hakuna hotuba ambayo tunajadili maendeleo tu. Lazima yataingia majina ya vyama. Dhamira yetu ya kushindana kisiasa ni kubwa kuliko kushindana na umaskini.
Hii inanitia hofu. Tunaweza kusimama na kujadili maendeleo tu bila ya siasa? Kinachonisikitisha ni kwamba tatizo la upinzani ndani na nje ya vyama vyetu haliwezi kumalizika. Wanadamu wameumbwa kupinga au kutokubaliana. Ukitembea na hisia za kukataa hali hii muda wote unajipunguzia siku zako za kuishi.
Tukifanya maendeleo tukumbuke kuna Watanzania milioni 55. Waliopiga kura ni milioni 10, wasiopiga kura ni milioni 45 na wanalipa kodi. Habari ya kuzungumzia siasa katika kila mkutano unaohusu maendeleo inachosha. Tatizo letu kubwa ni umaskini sio upinzani.
Ningekuwa namba moja, mikutano ya uzinduzi wa barabara au mapokezi ya ndege nisingewaita CCM, CHADEMA, TLP, CUF wala chama chochote cha siasa badala yake ningewaita watendaji wa wizara na viongozi wa serikali tu.[/QUOTE
Edo we ni noma. Kwa wenye akili za kunguni ni ngumu sana kukuelewa.
 
Upinzani huu nadhani ndo umetawala tangu tupate uhuru..ccm wameingia madarakani 2015 tu huko nyuma rais alukuwa mbowe tu hivyo basi ccm adui yao mkubwa ni upinzani ndio maana wanafanya kila hila kuhakikisha upinzani unatokomezwa tanganyika hii..jambo kuu wasilolijua wanaweza kutokomeza upinzani kwa kuua vyama vyote vya upinzani lakini hawatatokomeza fikra za kipinzani katika nchi hii...time will tell
 
Ule msitu wa Mabwepanda(sijui kama nimepatia jina) naona wamefungua mashamba. Wasiojulikana wameokoka,chui anacheza na mwanakondoo. Noeli leo,sikukuu ya amani
 
Back
Top Bottom