Hoja ya Edo Kumwembe kuhusu Serikali na upinzani

Hoja ya Edo Kumwembe kuhusu Serikali na upinzani

Magazeti ya RAI ya enzi za kina General Ulimwengu na mwenzake mzee Johnson Mwambo nimeyasoma sana. Ila sikumbuki kumwona Eddo akiandika makala za kisiasa.

Nawakumbuka.
1. Joseph Mihangwa
2. Ulimwengu
3. Mwambo
4. Lula wa ndali Mwananzela
5. Prince Bagenda
6. Ahamed Rajab
7. Na yule jamaa wa iringa mwenye kablog kake.
Basi mimi nimeanza kumjulia huko hata alipoanza kuandika Makala za michezo nikawa najiuliza atawezaje kuandika michezo maana kwenye Siasa nilikuwa namuelewa vzr
 
.....hao uliowataja nikweli walikuwa waandishi wakubwa wa makala nayule anaependa kujiita mwandishi mjengwa
Magazeti ya RAI ya enzi za kina General Ulimwengu na mwenzake mzee Johnson Mwambo nimeyasoma sana. Ila sikumbuki kumwona Eddo akiandika makala za kisiasa.

Nawakumbuka.
1. Joseph Mihangwa
2. Ulimwengu
3. Mwambo
4. Lula wa ndali Mwananzela
5. Prince Bagenda
6. Ahamed Rajab
7. Na yule jamaa wa iringa mwenye kablog kake.
 
Ndio ukweli kabisa! Umaskini wetu c wapinzani! Wala kuondoa vyama vya upinzani c kumaliza umaskini wetu! Je hayo majimbo yacyo ya upinzani yana tofauti gani ktk maendeleo?
 
Edo namkubali, moja ya watz wenye uwezo mkubwa wa kufikiri
 
Hii itakuwa makala ya pili ya Eddo Kumwembe kuisoma. Eddo kaacha uchambuzi wa soka sasa kaingia kwenye siasa?

Ila kasema kweli...
Yupo kwenye soka ila ana na safu kwenye gazeti la mwananchi kila siku inaitwa "Uchokozi wa Eddo ", ndio hua anaongelea jamii kiujumla
 
Ccm hawajui wajibu wao, wanapaswa kuwaeleza upinzani kwamba ccm wana haki ya kufanya mikutano ili kutoa mrejesho kwa mwajiri. Vyama vingine havina haki ya kufanya mikutano kwani hawana mkataba na wananchi mara baada ya uchaguzi. Shida ya ccm wamekalisha tuuuu hawatoi ufafanuzi. Wao ndiyo wenye ilani. Wanaodai mikutano wanapaswa kufanya mikutano maeneo waliyoshinda kwani ndiyo maeneo waliko na mikataba na wananchi. Shida ccm hawasemi haya.
Hivo ndivo katiba ya nchi inavosema au ni mawazo yko?
 
Kwa kiasi Fulani yuko sahihi kwa maoni yake ila nmkumbushe tu kwenye anga za elimu kuna kitu kinaitwa "reference " kitu hiki huwa kama siraha ya kukulinda pindi ufanyapo jambo la kitaaluma!!

Sasa nashangaa yeye kusema kusiwe na reference ktk uwanja wa siasa????

Yaani source ya Umagufulification asiitaje??? Angewezaje kumagulify bila CHAMA????

Hata hao watendaji wa wizara aliowasema bila CCM,, Chadema,, cuf nk wangetajwa na nani????

Tunakosoa tu kwa sababu tumeumbwa kukosoa!!

Siasa ni maisha... Yaani maji,, umeme,, barabara,, ndege,, elimu,, michezo nk vyote hv ni siasa!!! Development is all about politics!!! You cannot separate the two terms!!! They go together,,, how comes to separate the terms????
 
Unawasha televisheni yako, unachukua kikombe cha chai, unasubiri uwekaji jiwe la msingi kwa ajili ya barabara nyingi Kimara. Huyu anatoa hotuba, yule anatoa hotuba, mwingine anatoa hotuba. Mpaka inafika zamu ya namba moja naye anatoa hotuba.
Ndani yake kuna vijembe vingi kwa watu wanaoitwa wapinzani. Kila aliyeongea anaweka dhamira ya kukejeli, kukashifu, kuponda watu wanaoitwa wapinzani. Unaishia kutabasamu. Adui yetu ni umaskini au wapinzani?
Unaposubiri hotuba za mapokezi ya ndege inakuwa hivyo hivyo. Bado unajiuliza swali lile lile, adui yetu ni umaskini au wapinzani? Hata kama wanaongea sana, bado adui yetu ni umaskini. Na siku tukiwa matajiri hakuna atakayeacha kupinga na kukosoa mwenendo wa nchi.
Marekani kuna wapinzani, mitume nao walipingwa. Bahati nzuri kwa watawala wetu ni kwamba wapinzani wetu wanaishia kuongea, hawana dola, hawakusanyi kodi. Wanabakia kuwa mbu wanaozunguka sikio ambao wanakukumbusha tu kwamba milango ipo wazi.
Katika hotuba muhimu, bosi wa mkoa anamkumbusha namba moja kwamba mwaka 2020 atamkabidhi wabunge na madiwani wote kutoka chama chake. Hii itaondoa umaskini? Kwa mfano, hili hata likifanyika nchi nzima, itasaidia kuondoa umaskini?
Kuna mambo ambayo namba moja anayafanya. Muhimu kweli. Huwa nafikiria yanalenga katika kutuondoa hapa tulipo kama Taifa. Ukisikiliza hotuba ya tukio zima unahisi kwamba lengo halikuwa kukabiliana na tatizo fulani bali kuwaonyesha watu kwamba wapinzani hawafai.
Hotuba zetu zinajaa majina ya vyama. Hauwezi kusikiliza hotuba ukakosa kusikia CCM, CHADEMA, CUF, UDP. Hakuna hotuba ambayo tunajadili maendeleo tu. Lazima yataingia majina ya vyama. Dhamira yetu ya kushindana kisiasa ni kubwa kuliko kushindana na umaskini.
Hii inanitia hofu. Tunaweza kusimama na kujadili maendeleo tu bila ya siasa? Kinachonisikitisha ni kwamba tatizo la upinzani ndani na nje ya vyama vyetu haliwezi kumalizika. Wanadamu wameumbwa kupinga au kutokubaliana. Ukitembea na hisia za kukataa hali hii muda wote unajipunguzia siku zako za kuishi.
Tukifanya maendeleo tukumbuke kuna Watanzania milioni 55. Waliopiga kura ni milioni 10, wasiopiga kura ni milioni 45 na wanalipa kodi. Habari ya kuzungumzia siasa katika kila mkutano unaohusu maendeleo inachosha. Tatizo letu kubwa ni umaskini sio upinzani.
Ningekuwa namba moja, mikutano ya uzinduzi wa barabara au mapokezi ya ndege nisingewaita CCM, CHADEMA, TLP, CUF wala chama chochote cha siasa badala yake ningewaita watendaji wa wizara na viongozi wa serikali tu.
Hata upinzani ikishika madaraka ni lazima nawao viongozi wa chama watakuwepo na watapewa muda wa kutoa neno,embu waacheni na wana ccm muda wao wahutumie vizuri.kinachotakiwa hapo ni kuyaona maendeleo yanayoletwa kupitia wao.
 
tumefika pahala tunaponda kusikia yanayotufurahisha na ili kutimiza azma hii lazime tujitoe ufahamu.kwa sasa wenye mitazamo tofauti na wenye kusema ukweli wote ni maadui wa Tanzania na sio wazalendo.
 
Safi sana Eddo Kumwembe, fungua wenye mtindio wa ubongo waweze kutambua
 
Mwenye taarifa sahihi za uraia wa eddo tunahitaji tafadhali. Kuna kazi maalum
 
Huko nyuma tulifundishwa kuwa maadu watatu ni
1.Ujinga
2.Maradhi.
3.Umaskini
Lakini tulifundishwa pia kuwa ili tuendelee tunahitaji mambo makuu manne.
1.Watu
2.Ardhi
3.Siasa Safi
4.Uongozi Bora
Nikianzia hapo juu kwa maadui wakuu watatu,bado wapo,kwani ukishakuwa mjinga utakaribisha maradhi,na maradhi yakiingia yataleta umaskini.
Kwenye suala la maendeleo watu tunao na ardhi ipo ya kutosha,
Tatizo lipo kwenye Siasa safi na uongozi bora,
Nihitimishe kwa kusema kuwa maadui wetu watatu yaani ujinga,maradhi na umaskin ivinasababishwa na ukosefu wa siasa safi na uongozi bora.
Summarized
 
Kwa kiasi Fulani yuko sahihi kwa maoni yake ila nmkumbushe tu kwenye anga za elimu kuna kitu kinaitwa "reference " kitu hiki huwa kama siraha ya kukulinda pindi ufanyapo jambo la kitaaluma!!

Sasa nashangaa yeye kusema kusiwe na reference ktk uwanja wa siasa????

Yaani source ya Umagufulification asiitaje??? Angewezaje kumagulify bila CHAMA????

Hata hao watendaji wa wizara aliowasema bila CCM,, Chadema,, cuf nk wangetajwa na nani????

Tunakosoa tu kwa sababu tumeumbwa kukosoa!!

Siasa ni maisha... Yaani maji,, umeme,, barabara,, ndege,, elimu,, michezo nk vyote hv ni siasa!!! Development is all about politics!!! You cannot separate the two terms!!! They go together,,, how comes to separate the terms????
Huyo ana Vijihela Vya Kuuza Mashamba Ya Korosho Huko Kwao Kusini
 
Bahati mbaya kuna wanaofikiri tatizo letu ni keki tulio nayo aile nani. Kwa uroho wetu tumepoteza ustarabu na kushenzika. Kwa upande mwingine "Nyerere alitujengea ukondoo"-na kondoo wa nyerere wakawa wengi (miaka 26 wa utawala wake), na shida ni ukondoo huu kurishishwa toka kwa mzazi kwenda kwa watoto. Kuna watu sasa wanadhani wanahaki takatifu ya kutawala wengine, wakajiaminisha hivyo,wakateka vyombo vya dola na kazi yao kubwa ni kuswaga wale kondoo wa nyerere kwa upande mmoja na wako mbioni "kuua" wenye mawazo tofauti. Huu sasa umekuwa ugonjwa wa siasa za Tanzania matokeo yake ndiyo hayo. Kondoo wanaguna chini chini, wakubwa wanawaswaga wakijifanya kuna demokrasia na haki.
Fikiria vyama vitano vya upinzani kwa masaa matano havikujua wapi kwa kurudisha fomu za wagombea wao kule Korogwe na Tume ya Uchaguzi yenye wasomi (Judge na PhD) wana amini hivyo. Na sisi wengine tunaona poa tu au kuguna chini chini. Je tutafika?
Nyerere anahusika vipi na ukondoo wa watanzania waleo? Mwandishi aniceth mihambo anasema huo ni uvivu wa kufikiri ni sawa na wafrika wengine wanao tulaumu sisi wakoloni wakizungu kwa ugumu wa maisha yao wakati tulishawapa uhuru watu kama hawa wala si wa kuhurumiwa.
 
Kwa kiasi Fulani yuko sahihi kwa maoni yake ila nmkumbushe tu kwenye anga za elimu kuna kitu kinaitwa "reference " kitu hiki huwa kama siraha ya kukulinda pindi ufanyapo jambo la kitaaluma!!

Sasa nashangaa yeye kusema kusiwe na reference ktk uwanja wa siasa????

Yaani source ya Umagufulification asiitaje??? Angewezaje kumagulify bila CHAMA????

Hata hao watendaji wa wizara aliowasema bila CCM,, Chadema,, cuf nk wangetajwa na nani????

Tunakosoa tu kwa sababu tumeumbwa kukosoa!!

Siasa ni maisha... Yaani maji,, umeme,, barabara,, ndege,, elimu,, michezo nk vyote hv ni siasa!!! Development is all about politics!!! You cannot separate the two terms!!! They go together,,, how comes to separate the terms????
Silaha
 
Back
Top Bottom