Hoja: Ufisadi na matumizi ya rasilimali za umma au sarakasi za watuhumiwa?

"The healthy and strong individual is the one who asks for help when he needs it. Whether he's got an abscess on his knee or in his soul."Rona.
A%20S%20103.gif


Kiongozi Nape, kuna watu hapa ambao huwa tu wasomaji zaidi, wachambuzi na wapimaji wa mambo kabla ya kuandika neno.

Mimi nikiwa mwana CCM damu nakupa feedback yangu na natoa ushauri wangu waziwazi bila kumungúnya maneno kama ifuatavyo:

1. Nilishangilia na kupiga moyo konde na kuanza kupangusa vumbi ya kadi yangu ya CCM juu ya Kuchaguliwa kwako katika nafasi ya Ukuu wa Idara Taifani. Ilinitia moyo sana kama kijana mwenye mawazo mapya na pia kama mtu niliyekuchukulia kuwa na msimamo usiopindika katika kutetea maslahi ya umma (rejea skata la jengo la UVCCM n.k).

2. Nilifarijika sana ulipoanza kuongea pasipo kumungúnya maneno juu ya maazimio lya vikao vya juu vya chama likiwemo MAFISADI KUPIMA WENYEWE NA KUJIONDOA VINGINEVYO BAADA YA SIKU 90 CHAMA KITAWAWAJIBISHA!

3. Nilishutushwa na kutetemeka kukusikia mbele ya Luninga ukikana suala la deadline kwa Mafisadi kupewa siku 90. Na ukaanza kudefine dhana ya kuvua gamba in a very philosophical & theoretical manner kama vile: 'tumetawala miaka mingi sasa tumezeeka na hivyo inabidi tutoke ki upya' wakati kila mtu hata mtoto anajua kuwa hiyo dhana ya kujivua gamba ilianza kwa msisitizo wa kuondoa (gamba baya) wale wambao wametuchafulia chama ikiwa ni sehemu ya kujisahihisha na kurejesha heshima na matumani kwa mamilioni ya Watanzania.

4. Hili lisemwalo la wewe kuwa miongoni mwa waanzilishi wa CCJ ni jambo nyeti sana na hivyo linatakiwa kuli handle kwa uangalifu mkubwa.

Sikiliza, kama kweli kutoka moyoni unajua kuwa ulishiriki kwa namna moja au nyingine kutokana na ama kutoridhishwa kwako na mambo yalivyokuwa (kitu ambacho si ajabu ndio maana hata Chama chenyewe kufikia kuona kivue magamba!) au pia kama uliingizwa kimtego bila kujua kibinadamu, ni vyema useme wazi kuwa ni KWELI na kwamba sasa uko CCM na si CCJ kutokana na kile unachokiona kuwa CCM inaelekea kujirekebisha na kurejesha imani kwa Wananchi katika kusimamia masilahi yao kama mwanzo. Na useme waziwazi kuwa, kama kuna mtu anataka kukuadhibu kwa hatua uliyokuwa umeidhamiria basi uko tayari kupokea adhabu hiyo endapo itaamuliwa na vikao husika vilivyowekwa kihalali na CCM.

Mbona kuna wengi walikuwa Upinzani na leo wako CCM (wengine wamepewa uongozi) na hawasemwi? Siri ni kuwa walikuwa wazi! Kujiunga au kuondoka katika chama cha siasa ni kutokana na kile unachoamini na kwamba lazima ukione kinatekelezwa!

5. Kama utaendelea kukana kuwa hukuhusika na CCJ wakati ni kweli ulihusika (nasema kama ndivyo ilivyo, maana Mungu wetu, wewe mwenyewe na mashahidi wa kweli mnajua ukweli) hilo sasa ndilo
KOSA KUBWA KULIKO YOTE na hakuna hatakayekuamini tena. Kumbuka, sema kweli nayo itakuweka huru au sema uongo na uendelee kuwa mtumwa na kukosa heshima na kutokubalika milele!

6. Kama kweli hukuhusika, basi shikilia msimamo wako wa kukataa, lakini suala la kupambana na Mafisadi waziwazi kwa kushirikiana na Katibu MKuu na wengine wote kwa kuwataja majina yao hadharani, kuwapa deadline na kulisimamia lazima lilejewe bila kusuasua. Matendo kama hayo ndiyo yanaweza kufyonza propadanda zote za U-CCJ, Ubaba n.k mara moja. Maana huwezi kuwafanya Watz wajinga kujadili mtu kujiunga na chama cha siasa ambapo ni uhuru wake wa kikatiba akaacha kujadili na kumsifu mtu anayeamua kwa ujasiri kumshughulikia fisadi pasi kumwangalia usoni ambaye anaathiri vibaya mlo, makazi, nishati, biashara, elimu, miundombinu yetu, rasilimali zetu na utu wetu.

Vinginevyo bado mtaonekana mnapwaya sana (hamna afya wala nguvu) katika hizo nafasi na kama ni hivyo nasema, Tanzania ni kubwa sana mtutafute sisi tuwasaidie tupasue majipu na kutumbua usaha ili tupone!

Kamwe sikubaliani na kuendelea kupaka mafuta jibu na kubadilisha mikao na mitembeotukifikiri kuwa siku moja jipu linazama lenyewe!

Ndugu yangu Kibunago,

Kwanza kwa heshima kubwa nikushukuru sana kwa ushauri na mawazo mazuri. Niseme kuwa hakuna shaka kila atakayeamua kuwa mkweli juu ya kauli ya Porokwa anajua kwanini kasema hivyo hasa ikizingatiwa mahusiano yake na monduli na msimamo wangu juu ya Monduli..

Binafsi sioni tabu ya mtu kuanzisha chama kingine cha siasa kwa mujibu wa sheria za nchi yetu sio dhambi wala jinai....Lakini kubwa kwa chama kama CCJ kilichovuma hapa nchini japo kwa muda mfupi nikihusishwa nacho kwa haki sina shida kabisa.... Tatizo hapa labda niamue kuwafurahisha mafisadi wachache MIE NAWAJUA KWA MAJINA NA ROLE ZAO WALIOANZISHA CCJ, NAJUA KWANINI ILIKUFA HAWA WANAODANDIA LEO HAKIKA NI VIBARAKA TU.....

NINGEKUWA NIMEHUSIKA HATA KWA HARUFU SIONI HAYA KUSEMA KISU KIITWE KISU NA UMMA UITWE UMMA.

JUU YA WATUHUMIWA WA UFISADI SIJUI HOJA YA KUWA HATUCHUKUI HATUA INAANZIA WAPI, TULICHOAMUA KWENYE KIKAO NA AMBACHO NIMEKISIMAMIA NA NITAENDELEA KUKISIMAMIA NI KUWA WACHUKUE HATUA WENYEWE BAADA YA HAPO WASIPOCHUKUA HATUA KIKAO KIJACHO CHA NEC TUNAWAFUKUZA. SASA HAPA KATIKATI HATUA GANI ZICHUKULIWE ILI IONEKANE TUNACHUKUA HATUA?

HIKI NI KIPINDI CHA KUSUBIRI NEC IJAYO MUONE KAMA HAWAJATOKA NDIPO NIULIZWE.....MENGINE YALE 24 YANAENDELEA KUCHUKULIWA HATUA NA MOJA NI LA KUVUNJA KITENGO CHA PROPAGANDA NA KUANZISHA KITENGO CHA MAWASILIANO KWA UMMA NA NASHUURU NI WAZO LILOJADILIWA HUMU PIA KWA MUDA MREFU
 
LAT,
Fuatilia historia yangu si mtu wa kupotezea huwa najibu kile ninachokijua na kuamini. Mpaka nikaingia humu kwa jina langu inatosha kukwambia mie mtu wa namna gani.....

Hivi leo inahitaji elimu gani kujua kwanini Porokwa anasema aliyosema? nani tuchukue kauli yake? Aliyeanzisha chama mwenyekiti wa CCJ au Porokwa anayedai alishawishiwa akakataa? Ndo maana nikauliza tuendelee kujadili sarakasi za watuhumiwa wa ufisadi au jinsi rasilimali za nchi zitakavyotumika kuondoa matatizo yetu?

Rasilimali zipi Nape tuongelee?

Hizi zinazoendelea kuvunwa mchana na usiku ama hizi zilizopo mikononi mwa mafisadi kama mashirika ya umma yaliyouzwa kwa bei chee; nyumba za serikali ambazo ziliuzwa bila ridhaa ya umma wa watanzania; viwanja na ofisi za umma ambazo CCM iliipora jamii kubwa ya watanzania nakujipa wao kikundi kidogo bila ridhaa za umma wote watanzania; pesa za EPA ambazo inadaiwa iliigiza CCM madarakani 2005; IPTL; DOWANS; Meremeta na miradi lukuki hewa zilizoratibiwa na serikali ya kifisadi ya CCM? Which exactly amongst these you want us discuss? Please be specific and to the point.

Mimi ni mpinzani mkubwa wa ufisadi na nakuunga mkono katika hili lakini kwangu mimi fisadi ni fisadi hata kama ni baba yangu mzazi ama rafiki yangu. So long as umesema tudiscuss ufisadi ambao hasa ndiyo chanzo cha umaskini wetu basi tusaidie tuanze na lipi kati ya haya machache nayoyafahamu na yamekuwa expose for quite sometimes in various news media.
 
Ndo maana nikauliza tuendelee kujadili sarakasi za watuhumiwa wa ufisadi au jinsi rasilimali za nchi zitakavyotumika kuondoa matatizo yetu?
Heshima yako mkuu, kwanza pole na kazi na nipende kukupongeza kwa uwepo wako hapa kwa sababu kama unataka kusolve tatizo solution yake sio kulikimbia kwa hiyo uwepo wako hapa JF ni kuwa wewe sio muoga wa hoja zetu hapa JF na upo tayari kukabiliana na kila mtu,

back to topic:
Mkuu sasa tusipowajadili na kuwasulubisha hawa wacheza sarakasi hujui kuwa rasilimali zetu zitaendelea kuliwa na hawa jamaa? kwa sababu kizazi chao na system yapo imejikita kila sehemu kwa hiyo tukiwa ignore ni wazi kuwa wataendelea kuwepo na rasilimali zetu hazitaweza kuyaondoa matatizo yetu.na mpaka sasa hivi watu wanakuona wewe kama vuvuzela tu na mbuzi wa kafara, na hivi ni kweli haya unayoyaongea JK kakutuma?na unajua kuwa Lowasa alishasema kuwa hajakunata na JK njiani? Mkuu huna wasiwasi kuwa unaweza kuja kuachwa nyikani?

Mwisho ongea na wakuu wako mtuondolee huu mgao wa umeme

Amani iwe nawe:
 
Aaah baada ya kupata kama simu ya nane toka kwa waandishi wa habari juu ya sarakasi za watuhumiwa wa ufisadi(hasa hoja ya CCJ) nikajiuliza, tuzungumzie ufisadi ambao kimsingi ni namna rasilimali za nchi yetu zinavyotumika katika kushughulikia matatizo ya wananchi au nasi tucheze sarakasi hizi?
nakushauri upitie pitie hii thread itakusaidia huko mbele ya safari

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/138204-mukama-akumbana-na-zomea-zomea-huko-musoma.html
 
Nape,

Mkuu wangu nadhani CCM mnawatania wanananchi ama mnafikiri sisi wazoba kiasi kwamba hata maamuzi ya NEC hayalengi kuliokoa Taifa bali kundi la watu..

Hivi kweli ni akili kwa chama kufikia kukubaliana kuwaacha MAFISADI ndani ya chama na viongozi hadi wao wakubali kujizuru? Yaani kwa muda wa misezi mitatu hawa mafisadi waendelee kufisadi huku mkiomba wajiuzuru kana kwamba chama kina mtakaba nao..Haya baada ya kikao kijacho cha NEC wakiondolewa ndio mtakuwa mmetimiza ahadi kwa kina nani vile maana wananchi wanataka sheria ichukue mkondo wake pale inapotakiwa na sii kumpa mtu muda hali mkijua ni fisadi.

Haya yote yasingetokea mkuu wangu na yawezekana unapigwa vita hivi kwa sababu ya makosa yenu wenyewe kuwapa muda hawa mafisadi wajitanue na pengine hata kujenga ngome zao. Na wala sintashangaa kusikia kwamba wanatumia fedha nyingi sana kujisafisha kwa sababu makosa sii yao bali ya serikali ambayo inaweza kuwapa muda WAHUJUMU UCHUMI wajiengue wenyewe ktk chama ili hali makosa yao sii kuwepo kwao ndani ya chama bali UHUJUMU UCHUMI, kosa ambalo kikatiba halina muda wa kujiengua ila kukamatwa mara moja na kuswekwa ndani..

Mkuu mnacheza na uhai wa nchi yetu na hakika sijui pengine JK anapenda malumbano ya kiswahili swahili wakati maisha ya wananchi yanazidi kuwa mabaya na wamefikia gubu la unyama maanake wanaweza mchinja binadamu kama kuku kwa makosa madogo kabisa. Na msifanye mchezo kabisa na maisha ya wananchi ikiwa chama chako kunaendelea kudai hakina ushahidi wa Ufisadi hali mnaamini na kuwatangazia kwamba wapo mafisadi ndani ya chama..

Hii akili kweli mkuu wangu yaani mnao ushahidi mkubwa dhidi ya kina Rostam kuliko wa kina Yona na Mramba lakini kila siku mnadai hakuna makosa yametendeka ila mnakubali ati hawa jamaa ni mafisadi watuhumiwa..Well, court will decide their fate na sio NEC ktk swala zito kama hili mbona haikuwa hivyo kwa kina Mramba?..

Na haya maandamano ya Chadema ni kipimo na ashirio kubwa sana kwa viongoziwetu kwamba wananchi wamechoka!...Bora yanafanyika maandamano na mnaona jinsi walivyo na jazba, kuliko kesho kuwakuta na mapanga wakiwasubiri mabarabarani..Mnawalea Mafisadi kisha mnadai mtachukua hatua ati NEC itakapo kaa tena kwani NEC imekuwa mahakama..
 
Mkandara hizi nondo zako utasababisha Nape asirudi tena humu ndani.
sijawahi kumuona akitengua hoja yoyote humu zaidi ya kukimbia, may be kwa haya mawe yako he gonna come back as Nape
 
Ni muda sasa,

Naona umekuwa unajishughulisha na mitandao ya kijamii (karibia yote). Sio nongwa ila najua ndio mambo ya kwenda na wakati na siasa hizi za kisasa. Ila bado kuna vitu najiuliza!

Unafanya kwa manufaa ya nani hasa?
Je, yako binfsi? Chama? au taifa?

Kwa mapana kupitia uelewa wangu wa mambo kulingana na hali ya kitaifa ya kisiasa, ni wazi sana kuwa huwezi kuokoa chama chako wala taifa hili hasa kwa upande uliosimamia (chama).

Hivi Jr, ni kweli kabisa toka chini kabisa ya uelewa wa ubongo wako, unaweza kuwaambia watz waendelee kungoja?

Hicho unachokiita sarakasi wala sio kipya Jr, huo ndio umekuwa mchezo ambao serikali za CCm imekuwa ikikifanya..! Tunaweza kuorodhesha kila aina ya sarakasi ambazo zimekuwa zikichezwa na kila awamu ya utawala wa CCM.

Jr, kweli unataka watz waongeze miaka mingine 50 ya kuendelea kuangalia hizo sarakasi za serikali zenu? Hivi Jr, kweli unawajua watz ni watu waliochoka kiasi gani?

Nadhani una uzoefu sasa, kupitia kujiunganisha kwako na hii mitandao ya kijamii... fukuto jipya la vijana wa kitz! Rejea maongezi yako na wazee wako wa pale Bagamoyo University.

Jr, acha kucheza siasa nyepesi na za mazoea. Hii nchi ilipo, haihitaji siasa za namna unayojaribu kujenga hapa. Huu umaarufu binafsi unaojaribu kuufikiria, hautaacha "Legacy" yoyote ya maana kwa watoto na wajukuu wako japo utawaachia pesa/mali.

Ni dhambi isiyomeheleka kwa wewe kuja kucheza sarakasi huku kwenye mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari ili uonekane kama kijana unaeleta muafaka mpya wakati unajua fika gharama za huo mufaka hata Mwenyekiti wako hawezi kuziingia na kuzibeba.

Ni wazi sana kuwa hatima ya Tanzania haipo CCM. Hivyo si hekima kuendelea kuaminisha watu kuwa eti waendelee kuisubiria "sekretarieti mpya" iwashugulikie "mafisadi" afu ndio serikali itaanza kushughulika na kero za watu.
Mgogoro wa kimaslahi ndani ya chama chenu, hauwezi ukawa kwa gharama za maisha ya watu ambao tayari ni masikini sana.

Hivyo unavyokuja na hoja zaako hapa eti "...au tuendelee na sarakasi hizi..." wakati hizi nazo ni sarakasi sababu kati watu wanaoujua ukweli ni pamoja na wewe kwamba unachofanya ni sarakasi.

Ndio maana hamna kada (mtiifu) wa CCM anayeweza kueleza "kwanini Tanzania ni masikini sana pamoja na miaka 50 ya utajiri wake?"

Usihangaike kujibu "hoja" zangu ila jibu ilo swali tu Jr. Then tutaendelea na mjadala.​
 
Mi naona tuendelee na sarakasi za CCJ maana la kupambana na ufisadi mmeshindwa kabla hamjaanza. Yaani watu strategic kama EL na RA mnawapa miezi 4 ya kujipanga? Mi sitashangaa kama baada ya hiyo miezi 4 ukaondolewa wewe na wao mapacha watatu wakabaki. You were supposed to be decisive and brutal, sio kuuma na kupuliza.

Mwisho,Nnape unatakiwa u-focus, usirushe risasi kila upande, sidhani cheo chako ni cha msema chochote, diplomacy ni muhimu sana-hasa kipindi hiki ambacho chama chako kimepoteza ladha kwenye ndimi za watu. Comment yako kuhusu kwanini huwezi kujiunga na chadema lilikuwa ni kosa lako kubwa la kwanza kama mwenezi. Jiulize kwanini wakamtoa T. Hizza wakakupa ww.
 
Kama kweli ulishiriki kuanzisha CCJ na tayari umekana basi endelea kukana tu maana ukisema tena ulishiriki utaonekana ni kigeugeu na ni muongo huna msimamo, ila ujifunze tena kukubali kama itatokea mbeleni ukaambiwa jambo lingine na si hili la CCJ.

Halafu achana na CHADEMA, mbona una kazi kubwa tu na ni nyingi za kufanya chamani? Ondoa Lowassa, Chenge (mzee wa vijst), Karamagi, Mramba (mzee wa nyasi), Rostam na wengine kibao mnawajua hata kama kwa sasa si viongozi ila bado ni wanachama kwa kuwa waliwahi wakati fulani kuwakera watanzania basi pigeni chini wote.

Lakini nyie mnaendeleza taarabu za Makamba na Tambwe, sasa nyie kimkakati mna tofauti gani na kina Makamba?
 
Kuna tatizo gani kutaka kuhamia chama kingine halafu ukaghairi ni kosa? Sasa mbona imekuwa nongwa kwani kina mwakyembe wamekosa nini? Ina maana wao wamekosa zaidi ya mafisadi wanaoinyonya nchi yetu bila huruma!!!. Au ni danganya toto ya kuwasakama ili kupotezea ufisadi?
 
Nape mimi ni swali jepesi
kulikuwa na umuhimu gani kuwapa mafisadi siku 90, halafu baada ya hapo manakwenda kwenye vyombo vya habari kulialia kwamba mafisadi wanatumia vyombo vya habari kumchafua raisi na familia yake?

lakini pia mkaenda mbali zaidi na kusema wanaifadhili CHADEMA, sasa hapa ndipo kwenye utata, ina maana wewe Nape/ccm vita zidi ya hali ngumu ya maisha na ufisadi wanayopigana chadema huoni kama ni vita ya ukombozi mpaka wapate ufadhili wa hao mafisaid?

kama mafisadi wanafadhili CHADEMA ninyi CCM mnashindwa nini kuwanyang'anya kadi/uanachama?

mwisho nini msimamo wako kuhusu uteuzi wa Mrindoko kwenda wizara ya maji?

zingatia utendaji wake wa kazi huko NISHATI NA MADINI (RICHMOND) pamoja na human resource iliyotapaka nchi hii kuna nini kina mfanya raisi kumrudia mtanzania moja mchafu?

naomba husiweke siasa please, nadhani hapo tutapata mjadala mzuri wa ufisadi na maendeleo ya nchi.
 
Issue si mjadala ni vitendo, uwajibikaji, uaminifu na uwazi kwa kila tulifanyalo sio hoja za majukwaani tu ufisadi uifasdi tumechoka hadi lini? chukueni hatua kwa matendo.
 
Aaah baada ya kupata kama simu ya nane toka kwa waandishi wa habari juu ya sarakasi za watuhumiwa wa ufisadi(hasa hoja ya CCJ) nikajiuliza, tuzungumzie ufisadi ambao kimsingi ni namna rasilimali za nchi yetu zinavyotumika katika kushughulikia matatizo ya wananchi au nasi tucheze sarakasi hizi?

Kijana Nape

Swala la CCj halina mvuto hata kama ulikuwa mwanzilishi au sio mwanzilishi sio hoja
Hoja kuu ni suala la ufisadi na maisha ya Watanzania walio wengi ambao ni maskini wa kutupa.

Tuzungumzie raslimali zetu zinavyoporwa na wanaojiita wawekezaji wakati ukweli halisi ni wahamishaji wa rasilimali hizo maana hakuna lolote wanalolifanya katika uwekezaji wao.Kutudanganya na ujenzi wa madarasa mawili matatu ya shule ya msingi au secondary au kisima cha maji au barabara ya changarawe wakati wanavuna mamililioni ya pesa sio kitu ni unyonyaji uliopindukia. Kutudanyanya na kununua asprin kwenye hospitali zetu wakati wanavuna mamilioni kweney mbuga za wanyama na migodi yetu ni kutuibia wakati tunaona tena mchana. tuzungumzie ni nini tumefaidi kutokana na kuwepo kwa mbuga za wanyama au migodi ya madini. tuiangalie Shinyanga na utitiri wa migodi ya madini na kuzungukw ana mbuga za wanyama na urithi wa dunia kama serengeti. tuizungumzie Mara na utitiri wa migodi na mbuga ya serengeti na ziwa victoria lakini wananchi wana maisha duni kupindukia. Tuongelee utajiri wa rasilimali na ni nani anafaidi uwepo wake katika nchi yetu tuachane na masuala ya CCJ na uchagga wa CDM
 
Jamani nimemuona Nape humu ndani, naona alisahau hii issue.

BTW hii ndio hasa anatakiwa atueleze kuna habari za watanzania wenzetu waliokuwa wamefukiwa miaka 15 iliyopita atwambie wao kama chama wanafanya nini kuweka tume huru ya uchunguzi kuhusu kufukiwa kwa raia?
 
@Nape mnauye

inawezekana vipi tukawa na chama cha siasa kinachodai kinafuata misingi ya ujamaa wakati kukiwa na mambo yafuatayo

1.taifa kupata kipato cha chini ya 4% ya faida inayotokana na madini yetu

2.taifa kushindwa kukusanya kodi ipasavyo kwenye kampuni za simu na kusingizia hatuna teknolojia ya kujua ni kiasi gani wanapata

3.bandari kuwa chini ya watu wasioweza kuiendesha

4. gesi yetu kutonufaisha taifa letu....tunalia na mafuta wakati gesi yetu ingekuwa jibu sahihi kuendesha magari yetu

5.bunge kuwa kijiwe cha wazee wa chama chako

6.Hakuna sera za nini future za vijana wetu

7.kijana kama wewe uliyepewa nafasi kutumika kama spika ya wakuu bila kujua nini unafanya

8. Jamii ya kitanzania kuuwawa kwa sumu zinazotokana na migodi isiyo na tija bila serikali kuchukua hatua muhafaka


tuanze na hayo
 
Naamini hii hoja aliianzisha lakini baadae akajuta!, maswali ya msingi na hoja za uhakika alizopewa humu alizikimbia kwa kasi sana!, Cha kushangaza hata wakereketwa wa CCM na wapenda Mafisadi kama FAIZAFOXY walisoma tu wakaondoka kimya kimya! Kweli ni rahisi ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko kumtetea fisadi! Asalaaam alleykum Faizafoxy na Nape
 
Back
Top Bottom