Hoja: Ufisadi na matumizi ya rasilimali za umma au sarakasi za watuhumiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja: Ufisadi na matumizi ya rasilimali za umma au sarakasi za watuhumiwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Honey K, May 22, 2011.

 1. H

  Honey K JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2011
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Aaah baada ya kupata kama simu ya nane toka kwa waandishi wa habari juu ya sarakasi za watuhumiwa wa ufisadi(hasa hoja ya CCJ) nikajiuliza, tuzungumzie ufisadi ambao kimsingi ni namna rasilimali za nchi yetu zinavyotumika katika kushughulikia matatizo ya wananchi au nasi tucheze sarakasi hizi?
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  tuzungumzie unafiki wako kwanza ..... usipotezee jibu alichosema Porokwa
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nape play it safe boy, I can see that the way ur palying it ......in that political arena......ur creating enemies which is not healthy for ur political carrier. hope u know what i mean.
   
 4. Mkasika

  Mkasika JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [​IMG]

  Nape, husijitoe fahamu. Jibu kwanza tuhuma za mwenzako hapo juu kabla ya hiyo thread!
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nadhani cha maana ni sisi wanajamii kujibu hoja ya Nape na sio kuanza kumshambilia kwa hoja nyingine.... Na kama tunataka kuendeleza ya hoja nyingine basi tumuulize kwenye hizo threads

  Let JF be a arena where we dare talk openly in an understanding way....

  Back to topic... Nawaona kama watotow adogo kwa kuja kutudanganya mara magamba, mara tuzungumzie ufisadi mara tuangalie accountability nk

  Nadhani majibu yahoja yako yote ni moja tu... msizungumzie wala msicheze sarakasi, fanyeni tulichowatuma, muda wa sarakasi na kuzungumza ulishapita

  CCM FANYENI KAZI YA KUJENGA TAIFA NA SIO KUPEANA KEKI YA TAIFA KAMA HAKUNA MUNGU
   
 6. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nadhani sarakasi ulianzisha wewe ulipotuhumu Uchaga n.k.
   
 7. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mambo ya CCJ si ya muhimu kwenye maisha yetu, no matter ulikuwa ni mwanzilishi au la hilo halitusaidii. Wewe kama miongoni mwa watu mlio na madaraka tendeni (sio kuzungumza tu, we want action) kwa maslahi ya nchi.

  Nchi hii ina 50yrs age (japokuwa wewe have little impact kwa umri wako) maendeleo hayaridhishi kabisa ukilinganisha na raslimali tulizonazo.

  Lakini kubwa hapa linaloonekana ni ombwe la uongozi tuliokuwa nao. You are a young generation hebu jitofautishe na hao wazee waliotufikisha hapa.

  Huenda wakawa wamefanya kwa makusudi au kwa kutokuelewa. So Play you role ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hawa mafisadi wanakufilia mbali.

  We know Lowasa aka Monduli president still dreaming to be Tanzania mbunge aka president. Better he know early it is real impossible.

  We want clean people with clean image from appearence to his/her actions.

  That is all.
   
 8. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2011
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  "The healthy and strong individual is the one who asks for help when he needs it. Whether he's got an abscess on his knee or in his soul."Rona.:A S 103:

  Kiongozi Nape, kuna watu hapa ambao huwa tu wasomaji zaidi, wachambuzi na wapimaji wa mambo kabla ya kuandika neno.

  Mimi nikiwa mwana CCM damu nakupa feedback yangu na natoa ushauri wangu waziwazi bila kumungúnya maneno kama ifuatavyo:

  1. Nilishangilia na kupiga moyo konde na kuanza kupangusa vumbi ya kadi yangu ya CCM juu ya Kuchaguliwa kwako katika nafasi ya Ukuu wa Idara Taifani. Ilinitia moyo sana kama kijana mwenye mawazo mapya na pia kama mtu niliyekuchukulia kuwa na msimamo usiopindika katika kutetea maslahi ya umma (rejea skata la jengo la UVCCM n.k).

  2. Nilifarijika sana ulipoanza kuongea pasipo kumungúnya maneno juu ya maazimio lya vikao vya juu vya chama likiwemo MAFISADI KUPIMA WENYEWE NA KUJIONDOA VINGINEVYO BAADA YA SIKU 90 CHAMA KITAWAWAJIBISHA!

  3. Nilishutushwa na kutetemeka kukusikia mbele ya Luninga ukikana suala la deadline kwa Mafisadi kupewa siku 90. Na ukaanza kudefine dhana ya kuvua gamba in a very philosophical & theoretical manner kama vile: 'tumetawala miaka mingi sasa tumezeeka na hivyo inabidi tutoke ki upya' wakati kila mtu hata mtoto anajua kuwa hiyo dhana ya kujivua gamba ilianza kwa msisitizo wa kuondoa (gamba baya) wale wambao wametuchafulia chama ikiwa ni sehemu ya kujisahihisha na kurejesha heshima na matumani kwa mamilioni ya Watanzania.

  4. Hili lisemwalo la wewe kuwa miongoni mwa waanzilishi wa CCJ ni jambo nyeti sana na hivyo linatakiwa kuli handle kwa uangalifu mkubwa.

  Sikiliza, kama kweli kutoka moyoni unajua kuwa ulishiriki kwa namna moja au nyingine kutokana na ama kutoridhishwa kwako na mambo yalivyokuwa (kitu ambacho si ajabu ndio maana hata Chama chenyewe kufikia kuona kivue magamba!) au pia kama uliingizwa kimtego bila kujua kibinadamu, ni vyema useme wazi kuwa ni KWELI na kwamba sasa uko CCM na si CCJ kutokana na kile unachokiona kuwa CCM inaelekea kujirekebisha na kurejesha imani kwa Wananchi katika kusimamia masilahi yao kama mwanzo. Na useme waziwazi kuwa, kama kuna mtu anataka kukuadhibu kwa hatua uliyokuwa umeidhamiria basi uko tayari kupokea adhabu hiyo endapo itaamuliwa na vikao husika vilivyowekwa kihalali na CCM.

  Mbona kuna wengi walikuwa Upinzani na leo wako CCM (wengine wamepewa uongozi) na hawasemwi? Siri ni kuwa walikuwa wazi! Kujiunga au kuondoka katika chama cha siasa ni kutokana na kile unachoamini na kwamba lazima ukione kinatekelezwa!

  5. Kama utaendelea kukana kuwa hukuhusika na CCJ wakati ni kweli ulihusika (nasema kama ndivyo ilivyo, maana Mungu wetu, wewe mwenyewe na mashahidi wa kweli mnajua ukweli) hilo sasa ndilo
  KOSA KUBWA KULIKO YOTE na hakuna hatakayekuamini tena. Kumbuka, sema kweli nayo itakuweka huru au sema uongo na uendelee kuwa mtumwa na kukosa heshima na kutokubalika milele!

  6. Kama kweli hukuhusika, basi shikilia msimamo wako wa kukataa, lakini suala la kupambana na Mafisadi waziwazi kwa kushirikiana na Katibu MKuu na wengine wote kwa kuwataja majina yao hadharani, kuwapa deadline na kulisimamia lazima lilejewe bila kusuasua. Matendo kama hayo ndiyo yanaweza kufyonza propadanda zote za U-CCJ, Ubaba n.k mara moja. Maana huwezi kuwafanya Watz wajinga kujadili mtu kujiunga na chama cha siasa ambapo ni uhuru wake wa kikatiba akaacha kujadili na kumsifu mtu anayeamua kwa ujasiri kumshughulikia fisadi pasi kumwangalia usoni ambaye anaathiri vibaya mlo, makazi, nishati, biashara, elimu, miundombinu yetu, rasilimali zetu na utu wetu.

  Vinginevyo bado mtaonekana mnapwaya sana (hamna afya wala nguvu) katika hizo nafasi na kama ni hivyo nasema, Tanzania ni kubwa sana mtutafute sisi tuwasaidie tupasue majipu na kutumbua usaha ili tupone!

  Kamwe sikubaliani na kuendelea kupaka mafuta jibu na kubadilisha mikao na mitembeotukifikiri kuwa siku moja jipu linazama lenyewe!
   
 9. GodfreyTajiri

  GodfreyTajiri JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 846
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 60
  ili hoja yoyyote iwe na mshiko inabidi vinara wa hoja hiyo
  waaminiwe na wachangiaji na wafuatiliaji wa hoja hiyo.
   
 10. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Bwana Nape,
  Nilikuwa mwanaCCM na bado ni kiongozi katika ngazi ya Wilaya ingawa sina kadi kwa sasa.
  Chama kimepoteza mwelekeo na ulitoa matumaini makubwa sana ya kujivua gamba lakini utekelezaji wa mnachokisema na mnachokifanya ni tofauti kabisa.

  Watanzania wengi walitegemea kuona mabadiliko katika utendaji wa serikali na CCM. Watu walitegemea kuona mnatoa kauli zenye kutekelezeka lakini hakuna tofauti kati yenu wapya na waliowatangulia (Makamba and his team). Bado mnazungumza mipasho kama ya Hadija Kopa isiyo na effect. Bado tunaona akina Kagasheki wanadanganya Umma bila kuwakemea. Bado tunaona matumizi mabaya ya fedha za Umma bila chama kuchukua hatua. Bado tunaona mnaendelea kulindana na kupongezana kwa kutugandamiza watanzania na kutunyonya.

  Bwana Nape, Tutajadili ufisadi na matumizi ya rasilimali za taifa baada ya ninyi kuonesha umakini na weredi katika mwerekeo wenu. Utendaji kazi wenu ulivyo kwa sasa hakuna haja ya kujadili jambo hili kwani ni hesabu za kuzidisha kwa mtoto wa vidudu. Tujadili sarakasi za watuhumiwa wa ufisadi kwanza maana hiyo ndo level yenu.........
   
 11. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Bado sijakupata hoja yako kamanda.

  BTN
  Ebe tumbie tatizo la mgao wa umeme kwa MIPANGO ya CCM na serikali yake litakiwisha lini ? Maana kwangu sijui ndo hizo sarakasi?

  Otherwise haya ndo maoni yangu


  katika moja ya matatizo ni mgao wa umeme. Tatizo hili limesababishwa na mambo mengi ikwemo ufisadi na kutowajibika kwa watendaji na viongozi

  Hivi watendanji walio Chini ya CCM wanafanya nini.

  Kila wizara ina vitengo na watendaji na watu wa MIPANGO. Iweje kwenye hotuba za rais wetu tunasikia anasema mgao wa umeme ama changamoto?????!!!!!

  Binafsi naamini changamoto inakuja mara moja tu. Kama si mara moja basi matukio ya kuuitwa changamoto ni matetemeko ya ardhi, mafuriko na natural disaster. Sio mgao wa umeme. Sarakasi za mgao wa umeme ni moja ya FAILURE not CHALLENGE kwa serikali ya CCM na watendaji wake wakuu

  Kukosekana kwa MIPANGO na PRIORITY sahihi ndo kunachochea UFISADI matumizi holeala na mabaya ya rasilimali za umma . Mfano mmoja ndo huu kwenye Nishati

  Failing to plan is planning to fail
   
 12. F

  FredKavishe Verified User

  #12
  May 22, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Umekuja eeh was kindly waiting for u nape'hivi kijana mwezangu tuongee kirafiki tu unaweza kweli kuwafukuza mapacha watatu baada ya siku 90.halafu kitendo cha kuzunguka kujidai mnajivua gamba baada ya kueleza sera na ugumu wa maisha.halafu acha kukurupuka unasema hukutaka kujiunga na chadema eti wewe sio mchaga kwahiyo cdm ni cha wachaga kina zitto na mnyika na wengineo ni chaggas'kwahiyo na mimi nikisema ccm ni cha kifalme nitakuwa wrong wewe bila mbeleko za baba yako(marehemu) ungekuwa hapo'usikimbie jibu
   
 13. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  We sema NDIO au ni HAPANA.

  naona unaogopa kuwa UKIKUBALI NCHALE na UKIKATAA NCHALE ,

  LAKINI UNGEKUBALI TOKEA WAKATI ULE SA HIZI TUSINGEWASIKIA HAWA WANAOSEMA SASA HIVI NAAMINI YAPO MENGI, KUBALI MAPEMA YAHISHEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  May 22, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nape,
  Kwanza nikusifie sana kama kweli ulitaka kujiengua CCM kwa sababu, mtu yeyote mwenye akili timamu asingeweza kubakia ktk chama ambacho kilipoteza mwelekeo kabisa wa mafundisho ya kiitikadi..Na hata kama mimi ningekuwa mwanachama wa CCM ningetafuta njia ya kutokea au makazi mapya.

  Sasa tukiacha hizi sarakasi iwe kweli ulitaka kujiengua au laa maadam bado ni mwanachama halisi wa CCM na umepewa nafasi kubwa ya kukirudisha chama ktk nafasi yake ya awali, basi mkuu wangu fanya ulokabidhiwa. Ifanye kazi yako na sii kulumbana na Chadema ambao wanifanya kazi yao kama chama cha Upinzani.

  Kama umewaahidi wanachama wa CCM kuwaondoa Mafisadi, kuhakikisha chama chako kinapiga vita Ufisadi na wizi wa rasilimali zake mimi sioni sababu kabisa ya wewe kujiingiza ktk malumbano wakati makabrasha ya chama kuhusiana na mafisadi yamejaa mezani kwako...

  Kurudisha itikadi pasipo kufuatilia ibada zake ni sawa na mhuni tu aliyetaka kupata madaraka ili naye apate kujineemesha, na hili ndio tunaloliona sisi wananchi. Kisha basi huyo Lowassa, Rostam na Chenge wameisha chuma vya kutosha mkuu wangu hawa siii wana siasa ila ni mabwanyeye wanaotumia siasa kujineemesha.

  Nijuavyo mimi hamuwezi kuwaondoa watu uanachama kwa sababu imani ya itikadi ni haki na uhuru wa mtu kuchagua chama. Mtu anapoomba kadi ya chama hapitii mtihani fulani kwa sababu hii ni imani ambayo mwanachama mwenyewe ndiye mwenye malmlaka ya kujitoa. Hivyo, sidhani kama ni kazi kubwa sana kuwaondoa hawa mafisadi Uongozi ngazi zote za chama kwa sababu ndivyo mwongozo wa chama chochote unavyosema..

  Kulea watu wanaokiuka miiko na maadili ya chama kisha mkaendelea kutumikia gospel ya RACHEL ni kusaliti nafsi zenu wenyewe ktk imani ya chama. Mnapoteza au mtapoteza wanachama na kuharibu kabisa imani ya wananchi ktk mwelekeo wa chama hiki.

  Nakumbuka miaka michache iliyopita Mama Sophia Simba alimkashifu Mama Kilango kwa kupokea mchango wa Jeetu Patel ambaye kwa mdomo wake alisema ni FISADI asijitambue kwamba yeye ndiye kiongozi mwenye jukumu la kupambana na Mafisadi akiwa ofisi ya rais..

  Huu sio uongozi mkuu wangu hata kidogo..Hatutaki viongozi kama Mama Simba ambaye anachukua maswala kuwa sarakasi badala ya yeye kuifanya kazi alokabidhiwa akielewa kwamba Jeetu Patel ni FISADI lakini akachagua kulumbana na mchango wa harusi huku Fisadi linaendelea kukabidhiwa tender za serikali chini ya ulinzi wake..

  Hivyo mkuu wangu , mfano huo wa Mama Simba ndio tunauona ukiendelea hasa mnapotaka sana kulumbana na Chadema hali mafisadi wakitamba ndani ya chama. Mnawajua na bado mnawalea mkitafuta mchawi nje ya ukweli huo...

  Mkuu wangu, umekabidhiwa kazi ifanye! Navyomjua JK kakupa huo wadhifa makusudi kwa sababu waswahili wanasema siku zote - Mchawi mpe mwanao amlee!. na ndicho kinachokupata wewe...
   
 15. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nimeipenda hii, Nape kama kweli ni wewe chukua huu ushauri!! Pia nakushauri achana na wale wanaokupa SIFA kubwa hawakutakii mema ni Opportunistics tu!! Kama uliamua kujiunga CCJ si kosa si upo CCM sasa? Mbona Guninita alikuwa Chadema? au Wassira alikuwa NCCR? Si ni viongozi wakubwa tu sasa??

  Acha kudharau watu, jitahidi kuwapenda wasiopenda CCM na sikiliza nini sababu ya wao kutoipenda CCM itakusaidia kwenye kazi yako.
   
 16. GodfreyTajiri

  GodfreyTajiri JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 846
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 60
  Naungana nawe katika ushauri huu. Kama kweli yeye ni mwanzilishi wa CCJ itamsaidia sana. Iwapo atasema kweli ila akiendelea kukana na ikaja thibitishwa kwamba ni kweli ni mwanzilishi basi atapata taabu sana kuwaaminisha watu kile atakachosema siku za usoni
   
 17. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kaanzisha mada halafu kaingia mitini sasa tunashauriani kitu gani maana sijaona ukijibu hata hoja ndogondogo na mie nasepa!
   
 18. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
   
 19. H

  Honey K JF-Expert Member

  #19
  May 22, 2011
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  LAT,
  Fuatilia historia yangu si mtu wa kupotezea huwa najibu kile ninachokijua na kuamini. Mpaka nikaingia humu kwa jina langu inatosha kukwambia mie mtu wa namna gani.....

  Hivi leo inahitaji elimu gani kujua kwanini Porokwa anasema aliyosema? nani tuchukue kauli yake? Aliyeanzisha chama mwenyekiti wa CCJ au Porokwa anayedai alishawishiwa akakataa? Ndo maana nikauliza tuendelee kujadili sarakasi za watuhumiwa wa ufisadi au jinsi rasilimali za nchi zitakavyotumika kuondoa matatizo yetu?
   
 20. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #20
  May 22, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,557
  Trophy Points: 280
  Nape, siasa safi huzaa utawala bora.hili la CCJ si jepesi.najua umesoma threads nyingi humu kukushauri.usipuuze mwanakwetu!
   
Loading...