Hoja: Ufisadi na matumizi ya rasilimali za umma au sarakasi za watuhumiwa?

LAT,
Fuatilia historia yangu si mtu wa kupotezea huwa najibu kile ninachokijua na kuamini. Mpaka nikaingia humu kwa jina langu inatosha kukwambia mie mtu wa namna gani.....

Hivi leo inahitaji elimu gani kujua kwanini Porokwa anasema aliyosema? nani tuchukue kauli yake? Aliyeanzisha chama mwenyekiti wa CCJ au Porokwa anayedai alishawishiwa akakataa? Ndo maana nikauliza tuendelee kujadili sarakasi za watuhumiwa wa ufisadi au jinsi rasilimali za nchi zitakavyotumika kuondoa matatizo yetu?

Mkuu Nape.
1. Kuhama chama siyo kosa, ni kwa sababu dhamira yako ilikuwa inakwambia kuwa ccm na ufisadi wake was not your home. Kumbuka wasira, guninita na wengine wote walikuwa wapinzani. Wewe kubali na jamii itakukubali kuwa hukukubaliana na ufisadi unaofanywa na akina JK na rafiki zake wa kutuanagamiza watanzania.
2. Najua kabisa hufurahishwi namna nchi hii navyoongozwa, hasa undumilakiwili wa M/kiti wenu. Ni mtu asiyeelweka, hana maamuzi, ni mbinafisi, mpenda sifa sizizo waletea tija watanzania. I warn you young man, be very careful with Jk. He will use you and reject you as he did to his friends RACHEL.
3. Watu wengi tunakuchukia kwa sababu umeshindwa kusimamia kile ulichokisema badala yake umejiingiza kwenye siasa za maji taka kumshambulia Dr. Slaa kuwa anapata allowance 7millions. Huku ni kukosa kazi ya kufanya. Ungetuambia Mukama anakomba ngapi, je wewe, jk, chilligati nk. Young man, huenda hizi zisingekuwa mambo ya kusema kwa sababu 7m is peanut and Mr Mbowe has always clarified this to the public. Bahati mbaya umejiingiza kwenye mambo amabayo hayana maslahi kwa watanzania. Dogo, ungejikita kuimbia serikali na chama chako wakome kupora maliasili na fedha za watanzania kifisadi na mikataba ya hovyo yanayofanya nchii hii iwe mbaya kuliko jana. Mshauri JK apunguze safari zisizokuwa na tija. Fufua issue ya Richmond, Dowans, Meremeta (Shimbo 3 trillion), Deep green, kagoda Agriculture, EPA, watu wanazunguka migodi wanavyoteseka (resource curse) mfano nyamongo, geita, kahama nk, UDA, Ubungo, Pembe za ndovu (Kinana) na mengineyo. Shughulika kuona kuwa wananchi wanapata umeme na siyo porojo kam za jk kuwa yeye siyo Mungu aagize mvua inyeshe.
4. Kumbuka adui yako siyo chadema, ni ccm vs ccj
5. Alafu siku hizi watu wanakuita mnafiki wa ccj
 
Mkuu Nape,
Lengo la chama chochote cha siasa ni kutafuta ridhaa ya wananchi ili kushika dola na kutatua matatizo ya wananchi waliokipa nguvu chama husika. Hili la ufisadi, rushwa na uchafu mwingineo linachangia sana kwa CCM kupoteza mvuto kwa wananchi. Hili umelianza vizuri sana na umerudisha mvuto kwa kiasi fulani pamoja na kwamba sasa una-sua-sua kidogo. Kwa jukumu hili kubwa ulilonalo ambalo linaonekana kukuelemea, sidhani kama utapata muda wa kufuatilia CCJ ilianzaje, ilikuwaje na imekufaje. Na kwa mtu yeyote mwenye akili anayefuatilia kwa ndani ataelewa CCJ ni Sarakasi dhaifu sana. Na kwa kucheza sarakasi dhaifu kiasi hicho inaonyesha wewe uko mtu safi sana.

Kumbuka wananchi wana-machungu sana, na ndio maana kuna wengine wanadiriki hata kukuuliza mambo ya Bulyanhulu, about 15 years ago, ukiwa sijui sekondari. Sidhani kama utatatua kila kitu leo, ila CCM kama ugonjwa, unaweza kuwa umeingia haraka sana, neoliberal shock therapy' ila kupona kwake kutachukua muda, na saa nyingine msiogope tu-damu kama gamba ni gumu
 
Aaah baada ya kupata kama simu ya nane toka kwa waandishi wa habari juu ya sarakasi za watuhumiwa wa ufisadi(hasa hoja ya CCJ) nikajiuliza, tuzungumzie ufisadi ambao kimsingi ni namna rasilimali za nchi yetu zinavyotumika katika kushughulikia matatizo ya wananchi au nasi tucheze sarakasi hizi?

Hapo nakuunga mkono. Mimi nadhani kwa sasa hivi wananchi wanahitaji kusikia ni jinsi gani mafisadi hasa waliopo ndani ya CCM wanavyoshughulikiwa, vile vile namna ya kukabili matatizo ya wananchi. Kuongelea kuwa ni nani ana kadi ya ccm au nani hama hakusaidii lolote maana ni Watanzania wengi tu wana kadi za CCM. Ikumbukwe kuwa miaka ile ya nyuma tulilazimishwa kuwa na kadi za CCM vinginevyo usingeweza kuendelea na masomo au kupata kazi fulani bila ya hiyo kadi. Wengine tunazo tunawawekea kumbukumbu wajukuu wetu.
 
Back
Top Bottom