HOJA MBADALA: Tuhamasishe CCM imsimamishe Membe 2015?

Mzee Mwanakijiji, red on bold umeisemea vizuri. but on the blue marked, hatuko tayari kujiunga na oic
 

Mkuu Pasco kuna tatizo hapa.

Look, to be a Print Media regulator does not guarantee someone presidency or whatever the glory. Serikali na hata CCM yenyewe ndiyo regulators wenyewe kwa sasa lakini tunaona nini kwenye media? Unataka kuaminisha kwamba, kuwa regulator basi utaamka asubuhi na kufungia magazeti yaliyo against Membe? Au utahakikisa Membe aandikwe vizuri tu? Don't forget the media indutry is much diversified in such a case it has ownership complexity with different ideological and interests stands. Sasa sidhani kama kuwa na Rugulator wa Print media basi ni guarantee ya kuwa rais.Lakini pia kama ni suala la media control hata Wagombea wengine wanaweza si Membe peke yake.

Lakini, sidhani kwa Dunia ya sasa na mabadiliko ya ICT yaliyoikumba Tanzania siku za karibuni unaweza kusimama na kupuuza nguvu ya e-media. JF tu ina members karibu 100,000, hatujazungumzia FB, Twitter, BBM, Quepassa nk. nk. Ni wazi e-democracy ni kubwa kwa sasa hapa nchini hasa baada ya simu nazo kumwagika kwa kasi. Unaweza kuzungumzia Watanzania wengi si consumers wa e-media lakini nakuhakikishia nguvu yake kwa sasa si ya kupuuza. Uchaguzi mdogo wa Arumeru East ulinipa somo kubwa sana kuhusu hili.
 
Comrade,kwa wakati huu sio wakati wa kuwa na raisi tena kutoka mabwepande. Kumbuka wasaidizi wake ni wale wale. wewe unataka kuniambia membe anaamika zaidi kuliko alivyoaminika chaguo la Mungu??????????? Si unajua chaguo la Mungu aliaminika mpaka basi, leo sijui amegeuka kuwa chaguo la shetani!!!!!! Kumbuka mabwepande wanasema wasaidizi wake ndio wanaomuangusha!!!!!!!!!!!!!!sasa kuna sababu gani kujadili hoja ya Membe wakati wasaidizi watokanao na sisiem sisiem watamuangusha? jadili namna gani wanainji watafanya mageuzi kama ilivyokuwa Zambia over yeras ago na juzi kwa Satta, Kenya na Malawi. Tumebaki Tanzania na Uganda.
 
Nina uhusiano na Membe? naomba muweke wazi ili watu wajue. You HAVE MY PERMISSION, DARING AND BLESSING.

Nadhani kwa kuwa alikuwa huko USA mtakuwa mmeonana na amekusainisha rasmi. Kwa sasa umeanza kazi kwa kuja kupima upepo hapa jamvini ili ujue wapi uanzie kibarua chako.
 
mzee mwanakijiji's independence is being impaired...
 
pasco is opposition hater from the start..hivi huyu ni mwandishi wa gazeti gani anyway,i hear stories that he is a journalist
 
Kuna ile KANUNI iliyojificha ya CCM ya kumteua mgombea URAIS wa Tanzania kutoka jamii ndogo za Kitanzania. Kama kanuni hiyo bado inatufaa katika mazingira yetu tuendelee nayo tu. Kanuni hiyo inampitisha Membe moja kwa moja kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM.

Ninaposema jamii ndogo nina maana kabila ndogo zisizo na nguvu kubwa za kiuchumi, kielimu, kidini na kitabaka. Kanuni hii imechangia vizuri kupunguza ukabila na udini nchi hii. JIrani zetu hapa Kenya linawapa taabu sana hili. Wakikuyu hawaelewi mtu wa kabila ingine kuwa Rais wa Kenya.

Sio siri kwamba baadhi ya watu hawawezi kuhimili nguvu kubwa ya makabila na dini zao. Tuwaepuke hawa kama ukoma au ukimwi.
 
You always act as if you were a lecturer in jf,always attacking members capability to analyse issues,..mr.know it all
 
Oh! please..here we go again. can you cut the bull...for once!
 
Kuna thread ambayo ilikuwa inahusu urais 2015. Mwanakijiji alichangia, sikumbuki vizuri neno kwa neno lakini alikuwa against Membe kwamba tunataka kurudia makosa tuliyoyafanya 2005.

Hapa ni kutafuta ukweli wa maoni ya watu wengine.
 
Kwani Membe anatofauti ipi na Kikwete, mbona wote ni walewale tu
 
Maoni ya Mwanakijiji kwenye thread nyingine dhidi ya Membe ni tofauti kidogo na nilichosema hapo juu.Alichokiandika
 
Naona itawasaidia sana cdm kushinda! Hizi enzi si tu mtu anabebwa na chama kama ilivyokuwa kwa Mkapa "95, bali pia mtu nae anakibeba chama kama Dr Slaa "10! Membe doesnt fit in any how!

kwanza membe ni m2 wa visasi!, hawezi kuongoza nchi. Membe ni uchochoro wa cdm kushika nchi.
 
Membe anaweza kulete maafa zaidi ya jk maana huyu jamaa sijaona msimamo wowote alionao kweli hana kasoro nyingi lakini kutokana na na kutokuwa na misimamo imara ndio kigezo kitakachoiweka tena nchi rehani mwa mafisadi kama EL, RA, AC aka gwiji la Bariadi
 
Badilisha heading iwe CCM tuhamasishe...... kwa sababu sisi tusioipenda CCM Hatuna mchango hapo kwa sababu CCM wote ni walewale hakuna wa afadhari.
 
Tutaona mengi ya wanaotafuta ulaji 2015. Watu kama MM wanapenda kuandika kwa staili inayoficha misimamo yao na kujifanya kuwa 'great thinkers' wameelewa, ila wasiyo na 'great thinking capabilities' hawajaelewa. Hakuna 'rocket science' hapa, hii iko wazi, umri umesogea na matumaini yenu yako ukingoni na hapa mnatapatapa tu.

MM na wenzako, speculation zenu ziko wazi, msifikiri hamuonekani kwa sababu ninyi hamuoni. Mmeficha vichwa vyenu kwenye nyasi na viwiliwili vyenu viko hadharani. Mnatafuta pa kushika ili 2015 kieleweke. Desperation zenu zitawapeleka kwenye 'dead end'.

Si unaona jamaa yenu WM anavyohaha, mara EA, mara DSM, uchuro tu wa kutafuta ulaji kwa kujificha kwenye maandishi. kha!!!
 
Inaonekana kwa uchangiaji wa hii mada kuna watu wanataka CCM iweke mtu ambaye atamshinda mgombea wa CHADEMA!!Hili ni Jambo la ajabu kabisa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…