MM naomba nichakachue
thread yako kama inavyoendelea kuchakachuliwa.
Mara nyingi natatizika sana kila ninaposoma habari za fulani ni best
candidate.
Hapa ndipo nakubaliana na Mkandara kuwa elimu ya uraia bado ni tatizo
kubwa sana.
Wenzetu wanaojua kuchagua viongozi huangalia kigezo kimoja hadi kingine:
Maadili ya mtu, misimamo yake kisiasa, anasimamia nini, mahusiano na
wenzake, mahusiano na chama chake, ushiriki katikashughuli za kijamii,
maadili yake, mahusiano kati yake na wananchi, mtazamo wake kuhusu nchi,
historia ya utendaji wake, maamuzi aliyowahi kuayafanya huko nyuma,
uthubutu katika kusimamia anachokiamini n.k.
Tunatakiwa twende mbali zaidi ya hapa pa kusema fulani atatusaidia.
Labda nitoe mifano kidogo, ni Membe aliyetuambia kuwa tumeibiwa katika
Radar, ni Membe aliyekataa kutuambia nani ni wezi. Alichotaka ni
ku-score political point kuwa pesa zimerudi! Sasa huyu mtu kimaadili
unamweka kundi gani?
Nina nani miongoni mwetu anayejua misimamo ya Membe kuhusu masuala ya
kitaifa?
Mfano wa pili, ni Lowasa huyu aliyetuambia hakuna wizi Richmond, ni
Lowasa huyu aliyejiuzulu kwa dhambi anayosema hakuitenda, ni Lowasa huyu
anayesema alifanya hivyo kuilinda serikali, ni Lowasa huyo asiyetuambia
nani alibofoa Richmond hadi leo tunapata hasara. Ushujaa wa kusema huyu
ni best candidate unakuwa katika misingi gani?
Ni nani anayeweza kunishawishi kuhusu uadilifu wa Lowasa hadi apewe
ofisi kubwa kiasi hicho?Ni nani anayeweza kutumia vigezo ilivyoweka
kumpa pasi Lowasa japo 60%?
Kama ni suala la kusema tu fulani anafaa basi mimi nasema Sophia Simba
anafaa kama best candidate.
Msiniulize kwa vigezo gani kwasababu lengo ni kutaja tu.