Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,899
Mimi si mpenzi wa jukwaa hili, lakini katika pitapita zangu macho yangu yamekutana na uzi huu, Re: "Mademu wakichaga wazuri kisura mapenzi ni sifuri;" nimebaki kuduwaa na kushika tama, kwa vile naona inagusa haki fulani za wastaarabu na heshima kijamii bora nichangie kidogo.
Kitu cha kwanza maana ya mapenzi watu wanachanganya na ufuska. Kwa mtazamo huo wasichana wachaga si wafuska ila wanamapenzi kwa wampendao. Maana yangu ni kwamba fuska huridhika na mpenzie au mumewe kwa masuala ya sex badala ya moyo kupenda. Fuska asiporidhika atahangaika na kutangatanga huku na kule hadi aridhie tamaa zake kwa kiwango anachotaka, na atakayempata anampenda au la si hoja kwake ili mradi azime kiu ya silika mwilini mwake.
Upendo wa kweli kwanza kuwa pamoja na ampendaye ni shibe tosha, na mengine ni viungo kwenye pilau. Hata kitabu cha wimbo ulio bora kinasema: "upendo una nguvu kama mauti; maji mengi hayawezi kuzimisha upendano; mpendwa wangu ni wangu na mimi ni wake; nk." Huu ndio upendo tunaouzungumzia ambao hujengeka kati ya wawili na kushamiri katika mengi, kwani mapenzi si ufuska ambo mlengo wake ni sex tu, kwani sex ni sehemu tu ya mapenzi kwa vile mapenzi ni mlolongo wa mambo mengi yanayowafikisha watu kufikia huko kwenye kilele. Ole ukijenga mapenzi katika sex tu mapato yake ni kutodumu na mara baada ya kutimiziana misukumo ya silika kila mmoja anaondoka na njia yake bila kukabidhiana hati za talaka, why? haina mizizi, na maungo yameridhia yaliyotaka wamelipua kazi. Maana maridhiano yenu ni kuridhishana sex si kupendana kati yenu.
Kwa wenye uelewa wa Maandiko matakatifu kuna aya zisemazo: "Iheshimuni miili yetu, je, hamjui kama miili yenu ni mahekalu ya Roho Mtakatifu?" Kwa mtazamo huo wapenzi kitu muhimu cha kwanza ni heshima kwa miili yao wenyewe. Ufuska ni kujichosha bila kujali afya ya mtu , upendo wa kweli, na nguvu ya afya ya mtu kubaki na nguvu za kuitumikia familia na jamii yake. Hii kazi ya mabao mengi ndio ufuska, na kuchoshana, na kutwishana lawama zisizo za lazima, lakini kwa wenye kujali upendo kamili katika maisha yao na kujali afya zao wataelewa maana ya ninayoongelea. Hii ndiyo sababu ya baadhi ya madhehemu ya dini kabla ya ndoa kuna semina ya kuwafunda maana yamaisha ya ndoa, namna ya kulinda heshima za ndoa, namna ya kulinda afya yao, mapenzi yafanyike kwa kujali afya zao na namna ya kujenga familia bora katika maisha yao ya ndoa.
Wasiojali na kuheshimu miili yao na kuona ufuska ndio msingi wa mapenzi ndio wale wanaofikia hata kufanya mapenzi kinyume cha maumbile kitu ambacho hata mnyama hayawani anayetumia silika hafanyi. Sijapata kuona mnyama atafanya sex kwa kutumia viungo vya mdomo au haja kubwa, lakini wafanya ufuska ndio wanavyojirithia kufanya hivyo wakati wana akili zao na utashi. Huu ni utumwa katika kuitumikia miili na silika bila self control.
Kwa walioleta mada ya kuwakandia wasichana wa kichaga kwamba hawajui mapenzi, wamekosea, mimi nimewaona hawa wanajua sana maana ya mapenzi na kujali afya zao na imani zao, na kwa maneno mengine hawapendi kufanya ufuska ila kuridhia upendo wa kweli. Nilipoishi katika nchi fulani nje ya nchi nilipata kuwafahamu vizuri wasichana wa kichaga kuliko nilipoishi na ninapoishi Tanzania. Wasichana wa kichaga wengi wao walikuwa best friends na kuniomba niwape lift niwapeleke kanisani siku za jumapili, tofauti na baadhi ya wasichana wa makabila mengine baada ya kufika nchi za nje tu ilionekana dini ni kama walilazimishwa walipokuwa bongo, kufika nje wanajisikia huru zaidi.
Binafsi nawatete wasichana wa kichaga ingawa mie si mchaga. Ni wavumilivu sana wakimpenda mwanaume, wana heshima na ustaarabu ambao wanamjali rafiki kama kaka yake. Katika urafiki wasichana wa kichaga wanatanguliza ustaarabu tofauti na baadhi ya wasichana wengine ambao kuwa marafiki maana yake mahusiano ya sex, na wakiona mwanaume huna maelekeo ya sex basi wanaanza kumtelekeza, hii ni kasoro, tujifunze kwa wasichana wa kichaga. Mapenzi mazuri kwa wapendanao si idadi ya mabao kwa mkupuo ila moyo wa upendo wa kweli na kujali future ya maisha yao kimaisha. Sex za mabao mengi hazitujengei maisha mazuri, uchumi mzuri, nguvu za kutosha kufanya kazi nk, bali hudhoofisha nguvu na kufikiria mapenzi ni sex na starehe badala ya maana pana ya upendano wa wapendanao.