Hoja kuwa wanawake wa kichaga wazuri kisura mapenzi ni sifuri - Napingana nayo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja kuwa wanawake wa kichaga wazuri kisura mapenzi ni sifuri - Napingana nayo!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Candid Scope, Jan 18, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mimi si mpenzi wa jukwaa hili, lakini katika pitapita zangu macho yangu yamekutana na uzi huu, Re: "Mademu wakichaga wazuri kisura mapenzi ni sifuri;" nimebaki kuduwaa na kushika tama, kwa vile naona inagusa haki fulani za wastaarabu na heshima kijamii bora nichangie kidogo.

  Kitu cha kwanza maana ya mapenzi watu wanachanganya na ufuska. Kwa mtazamo huo wasichana wachaga si wafuska ila wanamapenzi kwa wampendao. Maana yangu ni kwamba fuska huridhika na mpenzie au mumewe kwa masuala ya sex badala ya moyo kupenda. Fuska asiporidhika atahangaika na kutangatanga huku na kule hadi aridhie tamaa zake kwa kiwango anachotaka, na atakayempata anampenda au la si hoja kwake ili mradi azime kiu ya silika mwilini mwake.

  Upendo wa kweli kwanza kuwa pamoja na ampendaye ni shibe tosha, na mengine ni viungo kwenye pilau. Hata kitabu cha wimbo ulio bora kinasema: "upendo una nguvu kama mauti; maji mengi hayawezi kuzimisha upendano; mpendwa wangu ni wangu na mimi ni wake; nk." Huu ndio upendo tunaouzungumzia ambao hujengeka kati ya wawili na kushamiri katika mengi, kwani mapenzi si ufuska ambo mlengo wake ni sex tu, kwani sex ni sehemu tu ya mapenzi kwa vile mapenzi ni mlolongo wa mambo mengi yanayowafikisha watu kufikia huko kwenye kilele. Ole ukijenga mapenzi katika sex tu mapato yake ni kutodumu na mara baada ya kutimiziana misukumo ya silika kila mmoja anaondoka na njia yake bila kukabidhiana hati za talaka, why? haina mizizi, na maungo yameridhia yaliyotaka wamelipua kazi. Maana maridhiano yenu ni kuridhishana sex si kupendana kati yenu.

  Kwa wenye uelewa wa Maandiko matakatifu kuna aya zisemazo: "Iheshimuni miili yetu, je, hamjui kama miili yenu ni mahekalu ya Roho Mtakatifu?" Kwa mtazamo huo wapenzi kitu muhimu cha kwanza ni heshima kwa miili yao wenyewe. Ufuska ni kujichosha bila kujali afya ya mtu , upendo wa kweli, na nguvu ya afya ya mtu kubaki na nguvu za kuitumikia familia na jamii yake. Hii kazi ya mabao mengi ndio ufuska, na kuchoshana, na kutwishana lawama zisizo za lazima, lakini kwa wenye kujali upendo kamili katika maisha yao na kujali afya zao wataelewa maana ya ninayoongelea. Hii ndiyo sababu ya baadhi ya madhehemu ya dini kabla ya ndoa kuna semina ya kuwafunda maana yamaisha ya ndoa, namna ya kulinda heshima za ndoa, namna ya kulinda afya yao, mapenzi yafanyike kwa kujali afya zao na namna ya kujenga familia bora katika maisha yao ya ndoa.

  Wasiojali na kuheshimu miili yao na kuona ufuska ndio msingi wa mapenzi ndio wale wanaofikia hata kufanya mapenzi kinyume cha maumbile kitu ambacho hata mnyama hayawani anayetumia silika hafanyi. Sijapata kuona mnyama atafanya sex kwa kutumia viungo vya mdomo au haja kubwa, lakini wafanya ufuska ndio wanavyojirithia kufanya hivyo wakati wana akili zao na utashi. Huu ni utumwa katika kuitumikia miili na silika bila self control.

  Kwa walioleta mada ya kuwakandia wasichana wa kichaga kwamba hawajui mapenzi, wamekosea, mimi nimewaona hawa wanajua sana maana ya mapenzi na kujali afya zao na imani zao, na kwa maneno mengine hawapendi kufanya ufuska ila kuridhia upendo wa kweli. Nilipoishi katika nchi fulani nje ya nchi nilipata kuwafahamu vizuri wasichana wa kichaga kuliko nilipoishi na ninapoishi Tanzania. Wasichana wa kichaga wengi wao walikuwa best friends na kuniomba niwape lift niwapeleke kanisani siku za jumapili, tofauti na baadhi ya wasichana wa makabila mengine baada ya kufika nchi za nje tu ilionekana dini ni kama walilazimishwa walipokuwa bongo, kufika nje wanajisikia huru zaidi.

  Binafsi nawatete wasichana wa kichaga ingawa mie si mchaga. Ni wavumilivu sana wakimpenda mwanaume, wana heshima na ustaarabu ambao wanamjali rafiki kama kaka yake. Katika urafiki wasichana wa kichaga wanatanguliza ustaarabu tofauti na baadhi ya wasichana wengine ambao kuwa marafiki maana yake mahusiano ya sex, na wakiona mwanaume huna maelekeo ya sex basi wanaanza kumtelekeza, hii ni kasoro, tujifunze kwa wasichana wa kichaga. Mapenzi mazuri kwa wapendanao si idadi ya mabao kwa mkupuo ila moyo wa upendo wa kweli na kujali future ya maisha yao kimaisha. Sex za mabao mengi hazitujengei maisha mazuri, uchumi mzuri, nguvu za kutosha kufanya kazi nk, bali hudhoofisha nguvu na kufikiria mapenzi ni sex na starehe badala ya maana pana ya upendano wa wapendanao.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,401
  Likes Received: 414,710
  Trophy Points: 280
  huu uongo umeanza lini...........ufuska hauna kabila uko mahali pote kwa sababu ya malezi bomu na kutafuta riziki ya bwerere....
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Japo hii inatupendelea was it necessary? Maana nnachoana ni majadala kuelekea kule kule tulipokua kwenye ile thread nyingine.

  Mara moja moja watu wawe wanaongelea makabila yao nayo yauze jina, sie tushatambulika vya kutosha.
   
 4. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  wasamehe!!
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,401
  Likes Received: 414,710
  Trophy Points: 280
  m'metambulika vipi?
   
 6. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Minashanga mtu kusema kabila flani mapenzo zero au kabila flani kwamapenzi wanaongoza yani mnataka kusema kawajaribu kabila nzima ya wachanga na jeuri hiyo anaitoa wapi? au yeye anaewambia wenzie mapenzi Zero yeye shahada ya mapenzi anayo? sio tabia nzuri kabisa kusema pumba.....
   
 7. s

  shalis JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  thnks lizz, upo sawa
  muwape heko hata na wagogo, wandengeleko, wafipa na wengine wengi tu sio kila siku sisi bana mtatupotezea test wenzenu lol
   
 8. bht

  bht JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  ungeandike tu kutukumbusha ''miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu''
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Uasherati ni mapenzi?
  Uchangudoa ni mapenzi?
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Waulize wasiochoka kutujadili.
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tunahitaji kueleza ukweli, tukinyamazia tu maana yake tunakubaliana na yaliyosemwa.
   
 12. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Mkuu Candid Scope ni kweli maelezo yako kuhusu mapenzi, mapenzi ya kweli yana heshima yake na ndilo nionalo kwa wasichana wa Kichaga!!!!!!!!! Wachaga hawajipeleki faaa, ua kujirahisisha mara nyingi ingawa si wote wanaangalia mtu aliye serious kwenye huo uhusiano wa mapenzi!!! Ni wakarimu lakini wanajijali wanajiheshimu sio limbukeni wanachagua ni makini, coz uhusiano wa mapenzi matokeo yake sahihi ni kuoana sikufanya umalaya kulalana ovyo!!!!! Tabia hizo za wasichana Wakichaga zinawapatia wanaume waliotayali kuoa na si vinginevyo!!!!!!!!

   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Utawaweza basiii. . .
  Wakikosa cha maana cha kututambia basi ndo wanakuja na hayo madai ili waonekane angalau nao wamewahi pata hata msichana.
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Jan 18, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sisi tumenyamaza, hatujali wanachoamini tunajali tunachofahamu. Kama wanayosema yangekua ya maana tungeshakosa wachumba siku nyingi.
   
 15. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #15
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Si ni tabia zenu Lizzy ndizo zinazo fanya muongelewe saana ili na wengine wajifunze!!!! Ila kuna dosali fulani in along way lazima watu wawe makini kwenye swala la ndoa!!!!!!!!!!!

   
 16. u

  utantambua JF-Expert Member

  #16
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mwanachuo ukitaka bumu lipukutike bila kujua date mangi
  Mfanyakazi ukitaka kamshahara kakwanguliwe ubaki na kikaratasi tu cha salary slip date mangi hahahahaha
   
 17. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #17
  Jan 18, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  Tatizo mtoa mada anaonekana ana hasira! namshauri anywe maji kwanza ndo aende akasome vizuri kilichopostiwa kwenye uzi alou-refer.
  Ushauri wangu kwa wote - tuache kujadili watu, tujadili mambo yanayohusiana na mahusiano, urafiki, mapenzi n.k.
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Jan 18, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hayo makabila mengine hayana TABIA? Hata kama ni nzuri, watuletee mada zao ili wengine wajifunze.
   
 19. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #19
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Katu hana hasira, mpenda kutoa ushauri, kutahadharisha watu wanapokuwa mno nje ya uringo, mpenda kujali balance sio kuegemea mno upande mmoja, lakini hayuko tayari kuyahalalisha yaliyo kinyume cha maumbile, malezi bora na maendeleo ya binadam na taifa.
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Yangekuwepo mazuri yangeongelewa, kwa sasa yanaonekana mengine ni kigugumizi kuyaanika ndio maana walio wazi katika tamaduni wao wanaanikwa hadharani.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...