S.M.P2503
Platinum Member
- Nov 25, 2008
- 3,688
- 7,145
Wewe ni Platinum member humu ndani, maana yake uko humu kitambo Kwa zaidi ya miaka 10. Hivi ni kwa nini unagoma kujishughisha na kujua Jambo moja tu… yote yanayo endelea nchini , likiwemo hilo la kuyataka maridhiano ni ili tu ccm ibaki madarakani milele… hilo unalijua au hulijui?Kwa hiyo tunahubiriwa maridhaliano katika mambo ambayo Wananchi hawayajui na wala haijulikani ni baina ya nani na nani na kwa nini!
Daaah Siasa hizi, Kaazi kweli kweli...
CDM wao hilo hawalitaki…
Sasa toa suluhisho, nini kifanyike tuondoke kwenye mkwamo huo?
Jibu lake ni rahisi tu na wewe kama Platinum unalijua. Ni usawa ktk mambo ya uchaguzi na kuifuata katiba tuliyo jiwekewa ktk mambo yote likiwemo la uongozi wa nchi.
Kinachoendelea kwa sasa, ni janja janja ya kujimilikisha nchi Kwa kutumia uchaguzi na waendelee kufisadi nchi na kujilimbikizia mali kutokana rasilimali lukuki tulizo nazo…
Keki ya taifa iliwe kwa usawa sio janja janja ya ulaghai ili wengine ndio wawe wanaila miaka nenda rudi hadi Yesu arudi.
Tukikubaliana usawa kwa vitendo, haki itatamalaki, na ndipo nchi itatulia. Hayo ndio maridhiano Kwa maoni yangu.