Hoja kuu ya maridhiano ya Kitaifa

Hoja kuu ya maridhiano ya Kitaifa

Mkandara

Platinum Member
Joined
Mar 3, 2006
Posts
16,156
Reaction score
9,723
Wakuu zangu leo mimi nataka kuelewa kuhusu haya maridhiano ya Kitaifa yanayozungumzwa ili kuliponya Taifa letu.

Hivi maaridhiano haya ni baina ya nani na nani? Kama ni ya Kitaifa swali langu "Kwani kuna mgogoro au kutoelewana kupi na baina ya nani na nani?"

Je, Serikali haielewani na Wananchi?,
Je, ni baina ya Dola na Wananchi?
Je, ni Vyama vya siasa?
Je, ni baina ya Viongozi wa nchi na kina nani?

Mpaka leo hii mimi sielewi tunataka kuridhiana juu ya kitu gani na kwa nini? Na Maridhiano hayo yanatokana na tatizo gani linalolianhaniza Taifa? Kipi kimeajiri Maridhiano haya yanayodaiwa?

Tumewahi kuona maridhiano baina ya CCM na Chadema, na wakawekeana masharti. Yalofuata tulisikia kuna Wasaliti wamelamba Asali? Je, safari hii kuna tofauti gani na ile ya mwanzo?

Pia tumeshuhudia maridhiano ya ACT na Serikali ya Zanzibar wanajua wao hoja na madai yalokuwepo. Na pengine huo ndionulikuwa msungi wa maridhiano, wamefikia muafaka baada ya kugawana madaraka.

Huko nje tumeona maridhiano baina ya Marekani na Iran kwa sababu kuna vita baina yao, wakitafita suluhu Vita isimame na wanawekeana masharti. Huu ndio msingi wa Maridhiano yao

Sisi Tanzania tunataka maridhiano ya Kitaifa kufuatia nini na kwa matumaini gani? Kuna jambo au mgogoro gani unaohitaji maridhiano baina ya wahusika?

Je, hoja kuu ni kupata Katiba Mpya? yahusu kamata kamata na Utekaji?
Ni kutokutambua matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2025?
Ni Uchochezi wa Kisiasa unaotutenganisha?
Ni Mauaji ya October 29? Ni wapi na kitu gani haswa tunapokosana?

Au ni yote kwa Ujumla wake! Na katika yote haya nani mkosa ambae yuko tayari kukiri kufanya makosa hayo anataka kuyamaliza kiistarabu!.

Mimi sielewi naomba kuelimishwa.

Maasalaam
 
..Kwa maoni yangu maridhiano yanapaswa kuzingatia hoja zifuatazo

1.Waliotekwa warudishwe

2.Waliouwawa miili yao ipatikane.

3.Waliotekwa, walioumizwa, na ndugu za waliouwawa, walipwe fidia ya kifuta machozi.

4.Waliohusika na utekaji na mauaji waondolewe kutoka ktk vyombo vya dola.

5.Sheria ya uundaji wa Polisi na Usalama wa taifa iandikwe upya na kupiga marufuku kujihusisha na siasa.

6.Sheria mpya ya uchaguzi iandikwe.

7.Katiba Mpya iandikwe.
 
Shukran sana, lakini kwa yote hayo inaonyesha haya sio maridhiano bali Matakwa (Masharti) ambayo Serikali inatakiwa kuyafanya. Ni sawa na andiko langu la mwisho kabisa hapo chini.

Je, unaamini Serikali ipo tayari kukiri kuyafanya yote hayo kinyume cha Sheria ama UTU na wapo tayari kuyamaliza?

Pili ili kufikia muafaka wa hayo kwa madai hayo, ni kina nani watahusika na kikao ama vikao vya kuitaka Serikali ikubali na kutimiza madai haya yanayo tugawa kama Taifa.

Mwisho, Upi hasa msingi wa maridhiano yetu? Je, Upande wa pili yaani Serikali nayo inakwazika wapi? na itaweka masharti gani maana maridhiano huja na pande mbili zikiweka masharti yao ili kufikia Muafaka wa pamoja. Serikali inadai vitu gani vifanyike ili tupate makubaliano ya pamoja na yenye tija na ya Kudumu.
 
Je, Serikali haielewani na Wananchi?, Je, ni baina ya Dola na Wananchi?

Hizo ni 'Siasa' tu za kujisafisha na ukatili wa Oktoba 29,2025.
 
..Kwa maoni yangu maridhiano yanapaswa kuzingatia hoja zifuatazo

1.Waliotekwa warudishwe

2.Waliouwawa miili yao ipatikane.

3.Waliotekwa, walioumizwa, na ndugu za waliouwawa, walipwe fidia ya kifuta machozi.

4.Waliohusika na utekaji na mauaji waondolewe kutoka ktk vyombo vya dola.

5.Sheria ya uundaji wa Polisi na Usalama wa taifa iandikwe upya na kupiga marufuku kujihusisha na siasa.

6.Sheria mpya ya uchaguzi iandikwe.

7.Katiba Mpya iandikwe.
ongezea na wahusika wa ukatili na mauaji ya raia kabla na baada ya Uchaguzi wachukuliwe hatua za kisheria.
 
Niliweka Mauaji ya October 29. Pengine hukunisoma vizuri, Je, Unadhani hii ndio sababu kuu ya Maridhiano yajayo, kuitaka Serikali kwanza Tundu Lissu aachiwe huru?
Je, tutakuwa tumeponya hizo Siasa za Kujisafisha au mustakabali wa Taifa hili unahusiana na Haki na Usalama wa Watu.
Nikielewa haswa tatizo ni nini na tunaanzaje ili kufikia hayo maridhiano. Mtakuwa mmenisaidia sana kuelewa chanzo na matarajio ya hayo Maridhiano.
 
Shukran sana, lakini kwa yote hayo inaonyesha haya sio maridhiano bali Matakwa (Masharti) ambayo Serikali inatakiwa kuyafanya. Ni sawa na andiko langu la mwisho kabisa hapo chini.

Je, unaamini Serikali ipo tayari kukiri kuyafanya yote hayo kinyume cha Sheria ama UTU na wapo tayari kuyamaliza?

Pili ili kufikia muafaka wa hayo kwa madai hayo, ni kina nani watahusika na kikao ama vikao vya kuitaka Serikali ikubali na kutimiza madai haya yanayo tugawa kama Taifa.

Mwisho, Upi hasa msingi wa maridhiano yetu? Je, Upande wa pili yaani Serikali nayo inakwazika wapi? na itaweka masharti gani maana maridhiano huja na pande mbili zikiweka masharti yao ili kufikia Muafaka wa pamoja. Serikali inadai vitu gani vifanyike ili tupate makubaliano ya pamoja na yenye tija na ya Kudumu.

..serikali haina jinsi ya kujinasua.

..wamelikoroga lazima walinywe.

..kuendelea hivihivi nchi inazidi kuvimba.

..kuwapeleka mahakamani genge lao la utekaji na mauaji ni jambo lisilowezekana.

..genge hilo linaweza kuanza kuwashughulikia Ccm na nchi ikasambaratika.
 
Lakini mkuu wangu mbona unazidi kunipeleka nje kabisa? Kama unasema Serikali haina jinsi ya kujinasua, sasa haya maridhiano yanahusu kina nani kama sio Serikali yenyewe.

Kisha hilo genge la Utekaji na Mauaji ni sawa na kusema ni genge la watu wasiojulikana. Mnawezaje kukaa meza moja na genge hilo!

Unajua, mimi Nikiwasoma Wanasheria, Wanaharakati viongozi wa vyama vya Siasa na baadhi ya mijadala nakutana na hoja nyingi tofauti sielewi haswa tunataka maridhiano katika mambo gani haswa?

Hapa ndio napata shida kuelewa maana kuna leo nimemsikia Lema akisema agenda ya Chadema wanataka Tundu Lissu kwanza aachiwe huru bila masharti ndio wataweza kushiriki Maridhiano!

Lissu anahusikaje na maridhiano hayo ya Kitaifa? ana wakilisha kundi gani la jamii au kama ni Chadema, Je, kuna tofauti gani kati ya sasa hivi na wakati ule wa Mbowe?

Je, akitoka kwa njia hiyo na akashiriki maridhiano, hatasemwa kalamba Asali? Kifupi, msingi wa kutaka hayo maridhiano mpaka sasa hivi bado siuelewi kabisa japo naelewa kuna fitna na unafiki mkubwa nyuma ya pazia.
 
..kundi la wasiojulikana litawakilishwa na serikali na Ccm, maana wao ndio walioulinda, na kulitumia.

..yasipofanyika mabadiliko ya Tume ya Uchaguzi, na Katiba Mpya, Lissu anaweza kuingia lawamani, na kutupiwa virago kama ilivyomtokea Mbowe.

.
 
kundi la wasiojulikana litawakilishwa na serikali na Ccm, maana wao ndio walioulinda, na kulitumia.

..yasipofanyika mabadiliko ya Tume ya Uchaguzi, na Katiba Mpya, Lissu anaweza kuingia lawamani, na kutupiwa virago kama ilivyomtokea Mbowe.

.

Kwa hiyo msingi hasa wa haya maridhiano unatokana na madai pamoja na matukio ya Kisiasa baina ya CCM na Chadema?

Kama ndio kwa nini basi watu wengine tunashirikishwa na maridhiano ilihali haya ni maswala baina ya Vyama hivi vya Siasa. Na huko CCM wao wanataka nini (masharti yao) kwenda upande wa Chadema?
 
..Ccm na Cdm wanachukua kundi kubwa ktk siasa za Tanzania.

..Wasipoishi vizuri ni hatari kubwa hata kwa wasio na chama.

..Na OCT 29 Ccm wakati wakiwalenga Chadema wakauwa maelfu ya Watanzania wakiwemo watoto.

..Mahusiano ya haki na usawa baina ya Ccm na Chadema yana maslahi kwa nchi nzima.

..Ccm wanatakiwa kuhakikishiwa usalama wao pamoja na kwamba wana DAMU za Watanzania mikononi mwao.

..CCM ni sawa na ilivyokuwa kwa Makaburu wa Afrika Kusini. Makaburu walifika mahali wakawa wameelemewa na mauaji na damu walizomwaga.
 
Ok, niseme nakubaliana na wewe. Unadhani Chadema hawana makosa ambayo hata wao wanalazimika kuyaacha kulinhana na mtazamo wa CCM.

Maana kwa vitendo vya CCM dhidi ya Chadema vinavyodaiwa sasa hivi lazima kuna sababu zinazo sababisha wao CCM wachukue hatua mbaya kama hizo.

Je, CCM wao wanadai kitu gani kibaya Chadema walikifanya ama wanakifanya maana Chadema ilikuwepo toka 1993 kwa nini sasa?

Tukielewa undani wa chuki na hasada zao ni rahisi hata sisi kutoa Ushauri kulingana na madai yao. Na juzi tu nimewasikia ACT nao wakitoa masharti yao kufikia ushiriki wao katika hayo maridhiano. Wao wanaingiaje?
 
..Tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe mwaka 1993 Ccm hawajawahi kujitokeza na wakidai jambo au mambo fulani toka kwa chama chochote cha upinzani.

..kinachoendelea ni hila na udhalimu tu wa genge fulani ndani ya Ccm dhidi ya Watanzania wenzetu walioko ktk vyama vya upinzani.

..Na ukichimba ndani zaidi utakuta kwamba kuna baadhi ya wana Ccm nao wamekumbwa na matukio mabaya kama yaliyowakuta wana Chadema, au wanaharakati.

..Wana Ccm wenye mapenzi mema na nchi wanatakiwa wakikomboe chama toka mikononi mwa genge la wadhalimu waliolifikisha taifa ktk mauaji ya OCT 29.
 
Kwa hiyo unarudi pale pale aliposema Polepole kuna kundi la Wahuni na aliwataja kuwa ni JK na mtandao wake.
Je, unadhani kweli JK anaweza kuwa kiangozi wa genge la WAHUNI? Na kama ndio, kwa nini asifanye UBAYA huu wakati yeye akiongoza nchi?

Mimi naona leo hii cha mtoto kabisa ukilinganisha madongo alikuwa akitupiwa JK, tena wakati ule kuna kundi jingine ndani ya CCM la Lowassa nao wakimpiga vita.

Tena wakati wake tulimshambulia sana hapa JF mpaka Kina Maxence walipewa kesi lakini hawakutekwa. Na kama sio JK nani Kiongozi wa genge hili maana Siamini pia kama ni rais Samia ambae kwa lugha nyepesi naweza sema alikaimu kwanza nafasi ya Urais baada ya kifo cha Magufuli ambae pia hakuwa na nguvu ya Kisiasa ndani ya CCM.

Unless mnaamini pasipo shaka henge hilo ni la rais Samia na mnawajua hao wasojulikana. Nje ya hapo, sioni maridhiano yakifanyika kwa madai ambayo Samia nina hakika atakana kuwa ndiye kiongozi wa genge la Utekaji na Mauaji.

Kwa hiyo, tunapotaka maridhiano ni lazima kiongozi ajulikane na yeye ndio awe mhusika mkubwa toka upande huo katika hayo Maridhiano.

Ndivyo ilivyokuwa wakati ule wa Katume na Maalim Seif (Zanzibar), Mbowe na Samia (Bara) Trump na Khamenei (Marekani) na hata majuzi Mwinyi na Masoud (Zanzibar). Na tutegemer kabisa hayo maridhaino hayatakuwa ya siku 2, mwezi pengine hata mwaka mzima.

Pasipo kujua msingi wa maridhiano na yatakuwa baina ya viongozi gani tutaendelea kusubiri maridhiano yasokuwa na maana kwa Mastakabari wa Taifa bali kqa manufaa na interest za watu fulani ..
 
Mkuu Mkandara , maswali yako ymaeuliulizwa miezi 12 iliyopita hapa jamvini. Hakuna mtu wa CCM au Serikali anayeeleza, maridhiano yanayuhusu nini, ni kati ya nani na nani na wamekoseana nini, lini na wapi.
Ikiwa maswali yako na wengine hayana majibu, maridhiano hayahitajiki kwasababu hayana msingi wala sababu

Wanaotakiwa kujibu ni CCM na Serikali yake ili ku set agenda. Tukumbuke pia CCM kupitia ilani na mgombea wao walisema ndani ya siku 100 wataanzisha maridhiano! Yalihusu nini? na kwanini kati ya nani na nani! hawajesema!

Kuhusu CHADEMA, hawakushiriki uchaguzi hivi wanahitajika katika maridhiano ya nini!

Kuna vyama 16 rafiki na CCM hao ndio wakae na CCM waeleze umma maridhiano wanayofanya ni ya nini kuhusu nini , kati ya nani na nani na wamekoseana nini!

Nilivyowaelewa CHADEMA ni kwamba watashiriki maridhiano yanayosemwa kama kundi jingine ikiwa yatakuwa chini ya ''mtu neutral'' baada ya kuelezwa yanahusu nini, akina nani wamekosena nini! wapi na lini
 
Kwa hiyo tunahubiriwa maridhaliano katika mambo ambayo Wananchi hawayajui na wala haijulikani ni baina ya nani na nani na kwa nini!

Daaah Siasa hizi, Kaazi kweli kweli...
 
Yup! Ndo maana yake.

We umeona wapi watu ‘walioshinda’ uchaguzi kwa 98% kutaka maridhiano?

Unaambiwa turnout ya uchaguzi ilikuwa watu milioni 32!

Kati ya hao, milioni 31 wakamchagua Samia.

Maridhiano ya nini hapo?
 
Wakuu zangu leo mimi nataka kuelewa kuhusu haya maridhiano ya Kitaifa yanayozungumzwa ili kuliponya Taifa letu.

Hivi maaridhiano haya ni baina ya nani na nani? Kama ni ya Kitaifa swali langu "Kwani kuna mgogoro au kutoelewana kupi na baina ya nani na nani?"

Je, Serikali haielewani na Wananchi?,
Je, ni baina ya Dola na Wananchi?
Je, ni Vyama vya siasa?
Je, ni baina ya Viongozi wa nchi na kina nani?

Mpaka leo hii mimi sielewi tunataka kuridhiana juu ya kitu gani na kwa nini? Na Maridhiano hayo yanatokana na tatizo gani linalolianhaniza Taifa? Kipi kimeajiri Maridhiano haya yanayodaiwa?

Tumewahi kuona maridhiano baina ya CCM na Chadema, na wakawekeana masharti. Yalofuata tulisikia kuna Wasaliti wamelamba Asali? Je, safari hii kuna tofauti gani na ile ya mwanzo?

Pia tumeshuhudia maridhiano ya ACT na Serikali ya Zanzibar wanajua wao hoja na madai yalokuwepo. Na pengine huo ndionulikuwa msungi wa maridhiano, wamefikia muafaka baada ya kugawana madaraka.

Huko nje tumeona maridhiano baina ya Marekani na Iran kwa sababu kuna vita baina yao, wakitafita suluhu Vita isimame na wanawekeana masharti. Huu ndio msingi wa Maridhiano yao

Sisi Tanzania tunataka maridhiano ya Kitaifa kufuatia nini na kwa matumaini gani? Kuna jambo au mgogoro gani unaohitaji maridhiano baina ya wahusika?

Je, hoja kuu ni kupata Katiba Mpya? yahusu kamata kamata na Utekaji?
Ni kutokutambua matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2025?
Ni Uchochezi wa Kisiasa unaotutenganisha?
Ni Mauaji ya October 29? Ni wapi na kitu gani haswa tunapokosana?

Au ni yote kwa Ujumla wake! Na katika yote haya nani mkosa ambae yuko tayari kukiri kufanya makosa hayo anataka kuyamaliza kiistarabu!.

Mimi sielewi naomba kuelimishwa.

Maasalaam
Maridhiano ya Nini??
 
Back
Top Bottom