tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 25,826
- 25,116
Bila kuchoshana na maneno mengi, naomba niingie kwenye mada moja kwa moja. Kwa maoni yangu, nadhani hoja zifuatazo ndizo zitakuwa ajenda kuu kipindi viongozi wa vyama vya siasa wakikutana na Rais Samia Hassan ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, kama Rais mwenyewe alivyoahidi kukutana na wanasiasa hao ili kuzika tofauti na chuki za kisiasa zilizoshamiri nchini kwa kipindi cha miaka 6 ya utawala wa hayati Dr Magufuli:
1. Katiba mpya
Hoja ya Katiba mpya imekuwa mwiba mkali sana kwa siku za hivi karibuni, hasa baada ya kufariki kwa Dr Magufuli. Katiba mpya ndilo litakuwa suluhisho la kudumu kwa matatizo mengi yanayolikumba taifa hili. Kwa kuwa mama Samia Hassan alikuwa makamu mwenyekiti wa bunge la katiba, nina imani kuwa atawapatia watanzania katiba mpya kuanzia pale mchakato ulipoishiwa endapo atashauriana vizuri na viongozi wa vyama vya siasa pindi watakapokutana naye Ikulu ya Chamwino. Nakumbuka mbunge wa Makambako, Deo Sanga, alidemka bungeni kisawasawa ile siku ambayo katiba ya wananchi ilipigwa chini rasmi baada ya kundi la UKAWA kujitoa na kuwaacha wachumiatumbo bungeni peke yao. Mama SSH ndiye tumaini pekee la watanzania kuwarejeshea katiba yao (Katiba ya Wananchi).
2. Kikokotoo
Bila shaka hiki kikokotoo kilianzishwa na Rais Magufuli, hasa baada ya kuifilisi mifuko ya hifadhi ya jamii. Mifuko hii ilifilisiwa na serikali ya Magufuli kwa namna mbili: Mosi, serikali inapaswa kupeleka michango yake kwenye mifuko kila mwezi lakini, kwa makusudi mazima, haipeleki michango yoyote. Pili, pamoja na kuwa serikali haichangii chochote, serikali ya Magufuli ilichota pesa nyingi sana kutoka kwenye mifuko hii kwa sababu mbalimbali kama vile ujenzi wa SGR, Stiglier’s Gorge, Uchaguzi Mkuu, barabara, nk. Haya ni matumizi mabaya ya mifuko kwa kuwa haikuanzishwa kwa makusudi ya kutoa fedha za kujengea miradi bubu ya serikali.
3. Tume Huru ya Uchaguzi
Sote ni mashahidi jinsi uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ulivyochezewa na serikali ya Magufuli. Uliofanyika sio uchaguzi bali ni uchafuzi. Kukiwa na Tume Huru ya Uchaguzi yenye misingi imara isiyoweza kuchezewa na mtawala yeyote, haki na uwazi itatawala katika chaguzi na hakutakuwa na uingiliaji wa kinajisi wa wanasiasa wachumiatumbo kama ilivyotokea katika uchaguzi uliopita.
4. Covid 19 wa JPM (na Ndugai)
Kule mjengoni kuna wabunge 19 ambao hawatokani na chama chochote cha siasa na hata wao wenyewe wameishajikana lakini Job Ndugai na JPM waliamua kuwachomeka mle kwa lengo wanalolijua wao wenyewe. Mpaka sasa fedha kibao za wananchi zimeishatumika kuwalipa “wabunge” hawa. Tunaomba wanasiasa wamshauri vizuri mama Samia awafukuze bungeni hawa covid-19 ili kuokoa fedha za umma zinazopotea bila sababu na pesa walizokwishalipwa hadi sasa wazirejeshe mara moja.
5. Mitihani ya ku-BET
Elimu ya wanafunzi wetu imeharibiwa kwa kiasi kikubwa sana kipindi cha utawala wa hayati JPM. Ni katika kipindi hiki tumeshuhudia mitihani ya ku-BET iliyopelekea wanafunzi kujiunga sekondari wakiwa hawajui kusoma, kuandika au kuhesabu. Hii hoja ni nyeti sana kwa sababu watoto wanaolemazwa na hizi siasa uchwara za JPM ni wale wa “wanyonge” wanaosoma shule za Kata huku watoto wa vigogo wakisomeshwa shule za Academies. Nina imani mama Samia akishauriwa vizuri ataifuta mitihani yak u-BET na hata kumfuta kazi waziri wa elimu aliyekubali uwepo wa hii mitihani haramu.
Kwa mtazamo wangu, hizi ndizo hoja kuu 5 ambazo viongozi wa vyama vya siasa watakaokutana na mama Samia hawatakosa kuzizungumzia. Nawe mchangiaji unaweza ukaongezea hoja yoyote ambayo unadhani ni muhimu kupenyezwa kwa Rais SSH kupitia kwa viongozi wa siasa.
Nawasilisha.