Hofu ya kufa imeifanya Afrika itumikishwe?

Hofu ya kufa imeifanya Afrika itumikishwe?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,842
Reaction score
50,556
Nimewaza tangu enzi za utumwa mpaka Sasa, katika vitu waafrika wanaogopa Sana ni kifo.

Ukichunguza kwa makini waafrika tunawaza zaidi kufa na baada ya kifo kuliko kuishi kabla ya kifo.

Tunawaza tukifa kitatokea nini badala ya kuwaza tunavyoishi kabla ya kufa maisha yetu yana thamani ipi!

Mababu zetu waliingizwa utumwani kwa kuwa waliwaza wakipingana na waarabu/wazungu basi wao watauawa. Matokeo yake walifanywa watumwa kwa hofu ya kuuawa.

Fikiria Mwarabu/mzungu mmoja aliwezaje kuwafanya mamia ya waafrika watumwa? Hofu ya kifo.

Watu kama Mkwawa au Kinjekitile na wengineo waliishia kufa na bila ya kuheshimiwa na watu wao lakini kina mangungo wa msowero waliishi kwa amani lakini wakiwa utumwani!

Hata Leo Afrika vita zote zilizopo zinatokana na harakati za baadhi ya watu kuogopa kufa na siyo kupigania thamani ya maisha yao wanayoishi kwa Sasa.

kwa ivo hofu ya kifo ndiyo inayozuia waafrika kuwaza jambo jingine lolote lile zaidi ya kusubiri kufa.
 
Mkuu karibu kila jamii imepitia utumwa, si kwamba walikuwa wanaogopa kifo. Unakutana na adui mwenye nguvu nyingi kiasi kwamba hakuna matumaini yoyote hata ukipigana. Kuna watu makatili, wataua wanaume wote na kubeba wanawake na watoto utumwani.
 
Lakini Afrika Kuna nchini inaitwa Ethiopia, unadhani hao makatili wauaji hawakupita kwenye nchi hiyo!?
 
Mababu zetu walizidiwa kwasababu hawakuwa na silaha bora mikuki mapanga na mishale haikufua dafu kwenye Bunduki na mabomu.
Wenzao wana bunduki wao wanakuja na uchawi wa maji' kwamba ikipigwa risasi itageuka maji.
The same miaka hii wenzetu wako maabara wanatafuta tiba za magonjwa mbalimbali, sisi tunasubiria miujiza.
 
Mababu zetu walizidiwa kwasababu hawakuwa na silaha bora mikuki mapanga na mishale haikufua dafu kwenye Bunduki na mabomu.
Bado maelezo mengi ya usaliti yalitokana na hofu ya kuuawa. Ethiopia walikataa kutawaliwa na waitaliano na waliweza.

Leo Afrika imekuwa omba omba kwa kuwa wananchi wanashindwa kupambana na viongozi wahalifu, mafisadi, walafi na wabinafsi kwa kuwa Wana hofu ya kuuawa.

Ulaya iliendelea pale watu wake walipoachana na hofu ya kufa.
 
Waethiopia walisaidiwa na Mwingereza baada ya Mtaliani kulishinda Jeshi la Mfalume wa Ethiopia na kuitawala Ethiopia kwa kipindi kifupi, Kenya MAU MAU walipigana kwa miaka kadhaa dhidi ya Mwingereza, Wasomali walipigana kwa miaka 20 ishirini dhidi ya Wakoloni wa Mwingereza Mtaliani na Mfaransa.

Tanganyika pia kulikuwa na resistance kama Majiamaji Rebellion.

Babu zetu walipigana hawakuogopa kufa sema walizidiwa teknolojia ya silaha, AngloZulu war Waingereza walipigwa kwenye mapigano ya Isandlwana mpaka ikabidi waongeze Askari kutoka kwenye British Empire.

Babu zetu hawakuwa waoga bali walizidiwa hata Wachina walizidiwa hata Waarabu walizidiwa kwahiyo ukizidiwa jifunze kwa waliokuzidi kama leo wenzetu wa Asia.
 
Hakika mkuu hiyo ni Mindset mbaya sana inaweza kukufanya usifanye maendeleo ukakaa unawaza sasa kesho nikifa inakuwaje acha nisifanye tu.
Na huu ndiyo mtego uliotunasa na kututofautisha sisi na wengine. Mtu anastaafu anapata milioni mia. Ukimwambia awekeze kwenye Kilimo Cha miti anakwambia "Leo Nina miaka 60 hadi miti ifike muda wa kuvunwa nitakuwepo"?

Lakini mtu huyo ana watoto na wajukuu. Leo hii walioanzisha kampuni ya Pepsi au coca-cola wapo? Lakini vizazi vyao vinakula matunda ya uwekezaji wa Babu zao.
 
Afrika imejaa mipango ya muda mfupi na wa Kati, watu hawataki mipango ya muda mrefu. Kila mtu ana hofu kuwa akipanga mipango ya miaka 30 ijanyo hawezi kuwepo kwa kuwa atakuwa amekufa.

Halafu kinachoshangaza wengi wao kwa siku za hivi karibuni wenye hofu ya kufa, ni vijana!
 
Mkuu karibu kila jamii imepitia utumwa, si kwamba walikuwa wanaogopa kifo. Unakutana na adui mwenye nguvu nyingi kiasi kwamba hakuna matumaini yoyote hata ukipigana. Kuna watu makatili, wataua wanaume wote na kubeba wanawake na watoto utumwani.
Suala la waafrika kutokuwa na umoja halikuanza Leo.
Umoja ni nguvu
 
Back
Top Bottom