Hofu ya kufa imeifanya Afrika itumikishwe?

Hofu ya kufa imeifanya Afrika itumikishwe?

Nimewaza tangu enzi za utumwa mpaka Sasa, katika vitu waafrika wanaogopa Sana ni kifo.

Ukichunguza kwa makini waafrika tunawaza zaidi kufa na baada ya kifo kuliko kuishi kabla ya kifo.

Tunawaza tukifa kitatokea nini badala ya kuwaza tunavyoishi kabla ya kufa maisha yetu yana thamani ipi!

Mababu zetu waliingizwa utumwani kwa kuwa waliwaza wakipingana na waarabu/wazungu basi wao watauawa. Matokeo yake walifanywa watumwa kwa hofu ya kuuawa.

Fikiria Mwarabu/mzungu mmoja aliwezaje kuwafanya mamia ya waafrika watumwa? Hofu ya kifo.

Watu kama Mkwawa au Kinjekitile na wengineo waliishia kufa na bila ya kuheshimiwa na watu wao lakini kina mangungo wa msowero waliishi kwa amani lakini wakiwa utumwani!

Hata Leo Afrika vita zote zilizopo zinatokana na harakati za baadhi ya watu kuogopa kufa na siyo kupigania thamani ya maisha yao wanayoishi kwa Sasa.

kwa ivo hofu ya kifo ndiyo inayozuia waafrika kuwaza jambo jingine lolote lile zaidi ya kusubiri kufa.
Uko sahihi. Kama Tanzania ndiyo kabisaa.
 
Na huu ndiyo mtego uliotunasa na kututofautisha sisi na wengine. Mtu anastaafu anapata milioni mia. Ukimwambia awekeze kwenye Kilimo Cha miti anakwambia "Leo Nina miaka 60 hadi miti ifike muda wa kuvunwa nitakuwepo"?

Lakini mtu huyo ana watoto na wajukuu. Leo hii walioanzisha kampuni ya Pepsi au coca-cola wapo? Lakini vizazi vyao vinakula matunda ya uwekezaji wa Babu zao.
Hapo tunafeli sana, ni heri ufanye tu hata ukifa utaacha faida kwa utaowaacha.
 
Afrika imejaa mipango ya muda mfupi na wa Kati, watu hawataki mipango ya muda mrefu. Kila mtu ana hofu kuwa akipanga mipango ya miaka 30 ijanyo hawezi kuwepo kwa kuwa atakuwa amekufa.

Halafu kinachoshangaza wengi wao kwa siku za hivi karibuni wenye hofu ya kufa, ni vijana!
Maisha magumu, ajira hakuna ndiyo maana vijana tunakata tamaa
 
Hapo tunafeli sana, ni heri ufanye tu hata ukifa utaacha faida kwa utaowaacha.
Huwezi kuwa na mawazo ya kufanya kitu endelevu kama unaogopa kifo. Ndiyo maana tunasema tunazaa watoto wengi ili wengine wakifa wengine wabaki.

Yaani mtu anapata mtoto badala ya kuwaza kuwa ataishi yeye anawaza kuwa atakufa.
 
Huwezi kuwa na mawazo ya kufanya kitu endelevu kama unaogopa kifo. Ndiyo maana tunasema tunanzaa watoto wengi ili wengine wakifa wengine wabaki.

Yaani mtu anapata mtoto badala ya kuwaza kuwa ataishi yeye anawaza kuwa atakufa.
Hii ni mbaya sana aisee tunaweza kuepuka kweli
 
Afrika imejaa mipango ya muda mfupi na wa Kati, watu hawataki mipango ya muda mrefu. Kila mtu ana hofu kuwa akipanga mipango ya miaka 30 ijanyo hawezi kuwepo kwa kuwa atakuwa amekufa.

Halafu kinachoshangaza wengi wao kwa siku za hivi karibuni wenye hofu ya kufa, ni vijana!
Mkuu kweli hili ni tatizo kubwa sana kwetu. Ni wachache wanaona mbali. Na kadiri miaka inavyosonga ndo watu wenye mipango ya muda mrefu wanavyopungua. Kwa mfano usishangae stendi ya mabilioni pale Mbezi miaka 20 ijayo ikavunjwa na kuhamishiwa tena kwingine kama ilivyokuwa Ubungo.
 
Waafrika tumeumizwa psychologically. Ndio maana mpaka leo unakuta Chama kinatawala miaka hata zaidi ya 50
Au unakuta Rais anaanguka anguka na wengine wakijikojolea ila bado wanaongoza mamilioni ya watu

Uoga ni kama ugonjwa tu na huu ugonjwa upo nchi nyingi sana za kimasikini

Unatawaliwa kwa kuambiwa thubutu uandamane
 
Waafrica wanaogopa kila kitu unakuta mtu mzima anashindwa hata kuamua jambo linalomuhusu yeye binafsi unakuta anaranda randa kusaka ushauri. Kifo kinaonekana kama kitu kisichofaa kujadiliwa mzungu anaambiwa kabisa umebakisha miezi kadhaa na ndugu wanaarifiwa huku kwetu ukisema utaambiwa mchimvi au una una mchuria mgonjwa mabaya.
 
Kama maarabu.
Tunayaona maarabu hapo Gaza yakiua kila kitu kuanzia majengo mpaka waliomo na vilivyomo ndani ya majengo sio wanamke sio wanaume sio wazee wala sio vichanga haya maarabu hayachagui wala hayabagui.

Nayakubali kweli haya maarabu yanayoua hapo Gaza kama Mungu wetu alivyo agiza tuendelee kuyaombea na kuya bariki haya maarabu hapo Gaza na Mungu wetu ata tubariki na ata yabariki ili yaue kila takataka hapo Gaza maana hazina thamani mbele za Mungu wetu.

Na sote tuseme jina la bwana aliyejuu muumba wa mbingu na nchi ahimidiwe Ameeen
 
Tunayaona maarabu hapo Gaza yakiua yakiua kila kitu kuanzia majengo mpaka waliomo na vilivyomo ndani ya majengo sio mwanamke sio mwanaume sio wazee wala sio vichanga haya maarqbu hayachagui wala hayabugui.

Nayakubali kweli haya maarabu yanayoua hapo Gaza kama Mungu wetu alivyo agiza tuendelee kuyaombea na kuya bariki haya maarabu hapo Gaza kama Mungu wetu ili yaue kila takataka hapo Gaza maana hazina thamani mbele za Mungu.

Na sote tuseme jina la bwana aliyejuu muumba wa mbingu na nchi ahimidiwe Ameeen
Pamoja na kuipindisha mada lakini hiyo vita ya Waisraeli na Hamas Ina jambo la sisi waafrika kujifunza.

Fikiria ni wapalestina wangapi wameshauawa Kwa miaka na miongo kadhaa. Jee wapalestina wamevunjika. Moyo? HAPANA.

Afrika hofu dhidi ya kifo na kufa hutufanya tukatishe mapambano ya kimaisha matokeo yake tumekuwa ni wateja na mateja wa mabara mengine!
 
Leo Kuna maelfu ya waafrika wamekufa. Lakini hao waliokufa inawezekana 80% waliacha kufanya mambo ya msingi kisa kuogopa kufa.

Kuna watu wanaogopa kuanzisha biashara eti kwa kuwa ikitokea wamekufa hiyo biashara italeta mzozo.

Kuna watu walikataa kusoma masomo ya sayansi kwa hoja kuwa yanachukua muda mrefu hiyo walihofia kufa kabla ya kufaidi matunda ya usomi wao.

Hofu ya kifo imetanda Afrika.
 
Back
Top Bottom