Hofu, Malalamiko ya Makonda Mitandaoni yanafikirisha

Peter Stephano 809

Senior Member
Feb 29, 2020
120
162
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia mtandao wa Instagram amechapisha akilalamika kuwa kuna makundi 5 ya watu wanaopanga kumuangamiza.

Makonda amesema makundi hayo yanataka kuhakikisha anapata kesi ya uhujumu uchumi au auwawe kabisa kwa manufaa yao binafsi.

"Nafahamu pia juu ya mbinu zinazoandaliwa ili kuniuwa kwa faida a familia zao pamoja na kutengeneza mashaidi wa uongo ili mnipe kesi ya uhujumu uchumi" Makonda ameandika.

Aidha makonda amebainisha makundi hayo yanaundwa na wauza madawa ya kulevya, mashoga, mafisadi, wanufaika na madawa ya kulevya na kundi la mwisho ambalo hakuliweka wazi. Ameandika kuwa licha ya kazi nzuri aliyoifanya wakati akiwa ofisini lakini bado kuna watu wanataka kumpoteza.

Hakika ukiwa mtumishi mwaminifu unaetetea haki za wanyonge tena ukitokea kwenye familia masikini haya ndivo malipo yake?, mtu aliejenga hospital , aliejenga ofisi za CCM, magari ya police ofisi za walimu, vituo vya polisi, shule za secondari na msingi, kutibu wagonjwa mpaka meli kuja Tanzania, kuhudumia makundi mbalimbali mpaka kuiunganisha serikali na viongozi wa dini leo hii naonekana eti natakiwa kunyongwa?" amehoji.

Sio mara ya kwanza Makonda kulalamika ingawaje hapo awali alisema kuwa kuna watu wana muhujumu kutaka kupora mali zake kwa maksudi.

Malalamiko haya ya Makonda yanaibua hisia na maswali mengi ambayo mtu anaweza kujiuliza ni nini kinamsibu Makonda?
Alipo sema kuwa wanataka kumnyang'anya mali ikaonekana ni jambo dogo lakini kufika kuhofia uhai wake ni jambo kubwa linalohitaji kujulikana.

Kama kweli kuna watu wanataka kumdhuru makonda ni akina nani hao na kwanini wasichukuliwe hatua?

Makonda anadai hayo makundi 5 ya watu wanootaka kumpoteza yanajulikana kwanini asipeleke malalamiko kwenye vyombo vya dora Mahakama na polisi kwa hatua za kisheria zaidi?

Tuseme kwamba Makonda haviamini vyombo vya dora hadi anakimbilia mitandaoni kulalamika ili apate huruma ya raia wa kawaida?

Hatuwezi kufikiria kuwa Makonda aliyetatua migogoro lukuki akiwa mkuu wa Mkoa hajui taratibu za kufuata ili kuripoti matukio kama haya?

Hapana kabisa bado kuna maswali mengi tunapaswa kujiuliza ili tupate kujua makonda ana hofu gani inayomtafuna na kumfanya alalamike kila kukicha.

Hatuwezi kujua ukubwa wa madaraka ya watu hao alio wataja katika makundi matano pengine ni wakubwa kimamlaka anohofia hawezi kupata haki, lakini mahakama na polisi ni vyombo huru anaogopa nini?

Bila shaka serikali ina miongozo yake katika kuwasaidia viongozi wake wastaafu kwanini Makonda hajatumia nafasi hiyo kulalamika?
Malalamiko ya Makonda Mitandaoni yanafikirisha na yanahitaji majibu.

Peter Mwaihola

1649695588086.jpg
 
Makonda aka Bashite anajihami tu kuhusu madhambi aliyowafanyia watu enzi ya Magufuli. Kama kweli anahisi kuna watu wanamuwinda na anawafahamu hana sababu ya kulalamika kwenye mitandao; jambo analotakiwa kufanya ni yeye kwenda kutoa taarifa kwa polisi ambao anawajua kwani alikuwa afande wao na wao watafanya kazi yao. Makonda kuja kulia lia mitandaoni ni ishara kuwa mabaya yake yamegundulika na sasa anatafuta huruma kutoka kwa wananchi.

Makonda hiyo janja janja yako ya Nyani imegundulika wala haitakusaidi, tulia ucheze mchiriku!!
 
Makonda aka Bashite anajihami tu kuhusu madhambi aliyowafanyia watu enzi ya Magufuli. Kama kweli anahisi kuna watu wanamuwinda na anawafahamu hana sababu ya kulalamika kwenye mitandao; jambo nalotakiwa kufanya ni yeye kwenda kutoa taarifa kwa polisi ambao anawajua kwani alikuwa afande wao na wao watafanya kazi yao. Makonda kuja kulia lia mitandaoni ni ishara kuwa mabaya yake yamegundulika na sasa anatafuta huruma kutoka kwa wananchi.
Naye anaogopa kama watu aliokuwa anawawinda walivyokuwa wanaogopa enzi zake.
Haya maisha bwana.
Sijui mshikaji wake le mutuz anasema nini kuhusu hili
 
Kuna vidume naona wanataka kuchukua roho yakeView attachment 2184199
"Waliowai kuwa sehemu ya......" Sehemu ya nn? Mbona anatoa taarifa kioga.

mtu aliejenga hospital , aliejenga ofisi za CCM, magari ya police ofisi za walimu, vituo vya polisi, shule za secondari na
msingi, kutibu wagonjwa mpaka meli kuja Tanzania, kuhudumia makundi mbalimbali mpaka kuiunganisha serikali na viongozi wa
dini
Hapa sijaelewa inamaana yeye ndio alifanya hayo yote Ama alikuwa msimasizi tu? Maana naona kama anataka kutafta sifa kwa njia ya uongo
Hiv mkuu wa mkoa ufanye ayo yete kwa ela gani uliyonayo? Yan had vilivyofanywa kwa kodi zetu mnafanya kama vile vimefanyika kwa ela zenu binafsi
 
Hivi kwanini ni msahaulifu kiasi hiki?? Amesahau alichomtendea Jaji Warioba?? Amesahau alichomtendea Lowassa kupitia yule binti feki??

Hata basi atuambie alikwenda kufanya nn Dodoma siku chache kabla ya Lissu kushambulia Kwa risasi??

Laana na damu za watu zilizijaa mikononi mwake ndiyo inayomtesa. Na hakika asipopata toba yakweli mauti lazima yamwandame.
 
HOFU
kuna ndoto mbaya za kujirudiarudia
Kuna damu zinamnukia
Kuna vivuli vinamfuata
Kuna marehemu wanamtokea
Kuna sauti zinamwambia mambo ya kutisha sana

Anakaribia kuwa kwenye denial state.. Ama kuwehuka.. Ushingae aanze hata kukikimbia kivuli chake mwenyewe.. Na wala si ajabu ukasikia kajinyonga...

Anaota yuko Segerea gerezani halafu anastuka na kuhema sana kumbe yuko kwake anajabu kulala tena
Mara kinapita kivuli dirishani anadhani ni wauaji wameshamfikia kumbe ni mbwa wake
Akijaribu kulala tena anaota yuko kizimbani anahukumiwa kunyongwa
Anaota anapigwa risasi, anaota anakufa.. Anaona sura za wale wore aliowadhulumu haki ya kuishi zikimlaki ama zikimkibiza na silaha mbalimbali

Amejifungia kwenye ma grill
Ana CCTV camera
Nyumba ina uzio mtefu wenye waya live za umeme
Getini kuna kampuni ya ulinzi na silaha za moto
Ana bastola na bunduki
Ana hirizi
Ana Bible nknk lakini bado hajiamini ana woga, ana hofu ana sononi
 
Back
Top Bottom