Hofu, Malalamiko ya Makonda Mitandaoni yanafikirisha

Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia mtandao wa Instagram amechapisha akilalamika kuwa kuna makundi 5 ya watu wanaopanga kumuangamiza.
Makonda amesema makundi hayo yanataka kuhakikisha anapata kesi ya uhujumu uchumi au auwawe kabisa kwa manufaa yao binafsi.
"Nafahamu pia juu ya mbinu zinazoandaliwa ili kuniuwa kwa faida a familia zao pamoja na kutengeneza mashaidi wa uongo ili mnipe kesi ya uhujumu uchumi" Makonda ameandika.
Aidha makonda amebainisha makundi hayo yanaundwa na wauza madawa ya kulevya, mashoga, mafisadi, wanufaika na madawa ya kulevya na kundi la mwisho ambalo hakuliweka wazi.
Ameandika kuwa licha ya kazi nzuri aliyoifanya wakati akiwa ofisini lakini bado kuna watu wanataka kumpoteza.
Hakika ukiwa mtumishi mwaminifu unaetetea haki za wanyonge tena ukitokea kwenye familia masikini haya ndivo malipo yake?, mtu aliejenga hospital , aliejenga ofisi za CCM, magari ya police ofisi za walimu, vituo vya polisi, shule za secondari na
msingi, kutibu wagonjwa mpaka meli kuja Tanzania, kuhudumia makundi mbalimbali mpaka kuiunganisha serikali na viongozi wa
dini leo hii naonekana eti natakiwa kunyongwa?" amehoji.
Sio mara ya kwanza Makonda kulalamika ingawaje hapo awali alisema kuwa kuna watu wana muhujumu kutaka kupora mali zake kwa maksudi.
Malalamiko haya ya Makonda yanaibua hisia na maswali mengi ambayo mtu anaweza kujiuliza ni nini kinamsibu Makonda?
Alipo sema kuwa wanataka kumnyang'anya mali ikaonekana ni jambo dogo lakini kufika kuhofia uhai wake ni jambo kubwa linalohitaji kujulikana.
Kama kweli kuna watu wanataka kumdhuru makonda ni akina nani hao na kwanini wasichukuliwe hatua?
Makonda anadai hayo makundi 5 ya watu wanootaka kumpoteza yanajulikana kwanini asipeleke malalamiko kwenye vyombo vya dora Mahakama na polisi kwa hatua za kisheria zaidi?
Tuseme kwamba Makonda haviamini vyombo vya dora hadi anakimbilia mitandaoni kulalamika ili apate huruma ya raia wa kawaida?
Hatuwezi kufikiria kuwa Makonda aliyetatua migogoro lukuki akiwa mkuu wa Mkoa hajui taratibu za kufuata ili kuripoti matukio kama haya?
Hapana kabisa bado kuna maswali mengi tunapaswa kujiuliza ili tupate kujua makonda ana hofu gani inayomtafuna na kumfanya alalamike kila kukicha.
Hatuwezi kujua ukubwa wa madaraka ya watu hao alio wataja katika makundi matano pengine ni wakubwa kimamlaka anohofia hawezi kupata haki, lakini mahakama na polisi ni vyombo huru anaogopa nini?
Bila shaka serikali ina miongozo yake katika kuwasaidia viongozi wake wastaafu kwanini Makonda hajatumia nafasi hiyo kulalamika?
Malalamiko ya Makonda Mitandaoni yanafikirisha na yanahitaji majibu.

Peter Mwaihola
View attachment 2184198
Mie nashauri apigwe tu maana hakuna namna
 
HOFU
kuna ndoto mbaya za kujirudiarudia
Kuna damu zinamnukia
Kuna vivuli vinamfuata
Kuna marehemu wanamtokea
Kuna sauti zinamwambia mambo ya kutisha sana

Anakaribia kuwa kwenye denial state.. Ama kuwehuka.. Ushingae aanze hata kukikimbia kivuli chake mwenyewe.. Na wala si ajabu ukasikia kajinyonga...

Anaota yuko Segerea gerezani halafu anastuka na kuhema sana kumbe yuko kwake anajabu kulala tena
Mara kinapita kivuli dirishani anadhani ni wauaji wameshamfikia kumbe ni mbwa wake
Akijaribu kulala tena anaota yuko kizimbani anahukumiwa kunyongwa
Anaota anapigwa risasi, anaota anakufa.. Anaona sura za wale wore aliowadhulumu haki ya kuishi zikimlaki ama zikimkibiza na silaha mbalimbali

Amejifungia kwenye ma grill
Ana CCTV camera
Nyumba ina uzio mtefu wenye waya live za umeme
Getini kuna kampuni ya ulinzi na silaha za moto
Ana bastola na bunduki
Ana hirizi
Ana Bible nknk lakini bado hajiamini ana woga, ana hofu ana sononi
🤣🤣🤣🤣 kama muvi vile, action after action. Shida ni ndoto zikiwa kweli ndo hapo kitaumana
 
Kuna sehemu nimesema naenda kumjaribu bwashee?
Au unaota mwambie aliyekaribu nawe akuamshe bwashee.
Maoni yako ya kwanza yanaonyesha unachofikiria kuhusu Makonda yani "Muoga" kindiga flani tu hivi ambaye wana mmudu wengi maana sisi tu wananzengo tunamtukana mbaya mbovu.
 
Hao uliowataja waliishi bongo hapahapa?
Unadhani makonda ni nobody kwenye nchi unayoishi kama ulivyo wewe?

Thubutuuu
natamani kukujibu ila akili yako ya kitoto sana refer bashiru,polepole,sabaya wa enzi hizo and now days.By then who is bashite?kayafa mwnyewe alimpiga chini sababu ya low mindset ya mission.kina kirefu kikimbie kusiko julikana hili jambo hutakiw kutumia akili kubwa kutambua mkuu.media zisharipoti anahitajika mahakamani over
 
Wewe dogo ACHA UJINGA.
Kajifunze kuandika kwanza pumbavu
 
Wewe dogo ACHA UJINGA.
Kajifunze kuandika kwanza pumbavu
nilijua utaanza matusi sababu akili yako inahakisi ulivyo,aya kama mi mdogo shikamoo makonda .sasa sijui ningeandika kizungu ingekuaje?Ngoja nikuache uendelee na deep pond za bashite
 
Acheni utani…..mnamaanisha ni Makonda huyu huyuuu anayekula bata kuliko watu wote duniani…ndo analalamika now au ni mwingine? Kweli madaraka hulevya na pesa hujenga kiburi
 
Maoni yako ya kwanza yanaonyesha unachofikiria kuhusu Makonda yani "Muoga" kindiga flani tu hivi ambaye wana mmudu wengi maana sisi tu wananzengo tunamtukana mbaya mbovu.
Angekuwa haogopi angepambana kimya kimya au angewaface hao anaowasema moja kwa moja bwashee.
Kifo kisikie tu hata mnyongaji anaogopa kunyongwa bwashee.
 
nyie chadema mnamchukuliaje makonda kama myonge au dhaifu hamumjui huyo. kwanza ulinzi wake unashinda ulinzi wa mbowe. soma kwenye maelezo yake chini ameandikaje: (ukiona maji yametulia jua kina kirefu) kama hamjui maana yake mtamjua.yeye katoa maelezo yake sio kuwa anaogopa anataka mjue ili akianza kupambana nao msije mkasema makonda mbaya
 
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia mtandao wa Instagram amechapisha akilalamika kuwa kuna makundi 5 ya watu wanaopanga kumuangamiza.
Makonda amesema makundi hayo yanataka kuhakikisha anapata kesi ya uhujumu uchumi au auwawe kabisa kwa manufaa yao binafsi.
"Nafahamu pia juu ya mbinu zinazoandaliwa ili kuniuwa kwa faida a familia zao pamoja na kutengeneza mashaidi wa uongo ili mnipe kesi ya uhujumu uchumi" Makonda ameandika.
Aidha makonda amebainisha makundi hayo yanaundwa na wauza madawa ya kulevya, mashoga, mafisadi, wanufaika na madawa ya kulevya na kundi la mwisho ambalo hakuliweka wazi.
Ameandika kuwa licha ya kazi nzuri aliyoifanya wakati akiwa ofisini lakini bado kuna watu wanataka kumpoteza.
Hakika ukiwa mtumishi mwaminifu unaetetea haki za wanyonge tena ukitokea kwenye familia masikini haya ndivo malipo yake?, mtu aliejenga hospital , aliejenga ofisi za CCM, magari ya police ofisi za walimu, vituo vya polisi, shule za secondari na
msingi, kutibu wagonjwa mpaka meli kuja Tanzania, kuhudumia makundi mbalimbali mpaka kuiunganisha serikali na viongozi wa
dini leo hii naonekana eti natakiwa kunyongwa?" amehoji.
Sio mara ya kwanza Makonda kulalamika ingawaje hapo awali alisema kuwa kuna watu wana muhujumu kutaka kupora mali zake kwa maksudi.
Malalamiko haya ya Makonda yanaibua hisia na maswali mengi ambayo mtu anaweza kujiuliza ni nini kinamsibu Makonda?
Alipo sema kuwa wanataka kumnyang'anya mali ikaonekana ni jambo dogo lakini kufika kuhofia uhai wake ni jambo kubwa linalohitaji kujulikana.
Kama kweli kuna watu wanataka kumdhuru makonda ni akina nani hao na kwanini wasichukuliwe hatua?
Makonda anadai hayo makundi 5 ya watu wanootaka kumpoteza yanajulikana kwanini asipeleke malalamiko kwenye vyombo vya dora Mahakama na polisi kwa hatua za kisheria zaidi?
Tuseme kwamba Makonda haviamini vyombo vya dora hadi anakimbilia mitandaoni kulalamika ili apate huruma ya raia wa kawaida?
Hatuwezi kufikiria kuwa Makonda aliyetatua migogoro lukuki akiwa mkuu wa Mkoa hajui taratibu za kufuata ili kuripoti matukio kama haya?
Hapana kabisa bado kuna maswali mengi tunapaswa kujiuliza ili tupate kujua makonda ana hofu gani inayomtafuna na kumfanya alalamike kila kukicha.
Hatuwezi kujua ukubwa wa madaraka ya watu hao alio wataja katika makundi matano pengine ni wakubwa kimamlaka anohofia hawezi kupata haki, lakini mahakama na polisi ni vyombo huru anaogopa nini?
Bila shaka serikali ina miongozo yake katika kuwasaidia viongozi wake wastaafu kwanini Makonda hajatumia nafasi hiyo kulalamika?
Malalamiko ya Makonda Mitandaoni yanafikirisha na yanahitaji majibu.

Peter Mwaihola
View attachment 2184198
KulalMika Hvo...
Kama kajua watu wafanyaje...
Anahisi kujua kwake ndio kutawazuia watu kufanyia walichopanga ... labda hawajui Binadamu vzur ..hapana ni ameusahau ubinadamu wake kpind yuko madarakan

Vitu VIWILI VYa KuVIEPUKA MAiShaNi MwaKO

2. KUJIFANYA MJUAJI.. bnadam hatupend Sisi tunakuloga tu ... ukijfanya we ndo wewe..

1. KuzBA LIZIKI YA MTU... ndugu yang hata kama mtu anakula kula kwa magendo ww pita Mbali usicheze na sehem ya mtu anayopatia ugali wake... utauwawa

Nawasilisha...

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
 
natamani kukujibu ila akili yako ya kitoto sana refer bashiru,polepole,sabaya wa enzi hizo and now days.By then who is bashite?kayafa mwnyewe alimpiga chini sababu ya low mindset ya mission.kina kirefu kikimbie kusiko julikana hili jambo hutakiw kutumia akili kubwa kutambua mkuu.media zisharipoti anahitajika mahakamani over

mbona hajafika mahakani mpaka leo ila mbowe alipelekwa kama kuku. makonda ni mtu mwingine tofauti na bashiru polepole sabaya
 
HOFU
kuna ndoto mbaya za kujirudiarudia
Kuna damu zinamnukia
Kuna vivuli vinamfuata
Kuna marehemu wanamtokea
Kuna sauti zinamwambia mambo ya kutisha sana

Anakaribia kuwa kwenye denial state.. Ama kuwehuka.. Ushingae aanze hata kukikimbia kivuli chake mwenyewe.. Na wala si ajabu ukasikia kajinyonga...

Anaota yuko Segerea gerezani halafu anastuka na kuhema sana kumbe yuko kwake anajabu kulala tena
Mara kinapita kivuli dirishani anadhani ni wauaji wameshamfikia kumbe ni mbwa wake
Akijaribu kulala tena anaota yuko kizimbani anahukumiwa kunyongwa
Anaota anapigwa risasi, anaota anakufa.. Anaona sura za wale wore aliowadhulumu haki ya kuishi zikimlaki ama zikimkibiza na silaha mbalimbali

Amejifungia kwenye ma grill
Ana CCTV camera
Nyumba ina uzio mtefu wenye waya live za umeme
Getini kuna kampuni ya ulinzi na silaha za moto
Ana bastola na bunduki
Ana hirizi
Ana Bible nknk lakini bado hajiamini ana woga, ana hofu ana sononi
Nakuaminia mdogo wangu. Kama fasihi umepitiliza na kama Saikologia basi wakupe phd ila siyo ya wale wenzetu. Hongera kwa hili na akisoma arudie tena Bashite akumbuke mateso ya Roma mkatoliki na wenzake na wengine wengi akina Mo wakiwemo. Damu ya mtu siyo maji.
 
Back
Top Bottom