Hizi tabia kwa baadhi ya wanaume mnazionaje?

Hizi tabia kwa baadhi ya wanaume mnazionaje?

Mr coffee

Member
Joined
Mar 12, 2018
Posts
74
Reaction score
34
Salam,
Wanajamvi leo hii nimekuja na mada mpya ambayo imekuwa ikinitatiza kwa kipindi kirefu sana ni moja ya tabia ya baadhi yetu sisi wanaume ambazo kiupande wangu naziona haziko poa na sijui upande wenu mnazionaje.
  1. Mwanaume mzima unakuta anamsalimia mwanaume mwenzake kwa salamu ya neno mambo uku akiwa na demu wake au laaah.
  2. Mwanaume mzima kutamka neno la mshangao Teh! Teh! Akiwa na demu wake, mke wake au laah hii ikoje maana nimeikuta miongoni mwa makabila ya wadigo imeshamiri sana.
  3. Mwanaume kutembea akiwa ameshikana na mwanaume mwenzake mikono barabara nzima wao wenyewe tu hii ikoje wanajamvi.
  4. Mwanaume kuongozana na wadada au kukaa na vikundi vya wadaa hii ikoje wanajamvi.
  5. Mwanaume kujishughulisha kwa kazi za mapambo, mapambo salooni za kike kuchekacheka ovyo hii ikoje wanajamvi
Katika hizo tabia zote ambazo kwangu naziita kama Big 5 hivi wadada ukimuona mwanaume wako anahizo tabia unajisikiaje na je, wanaume wenzangu hili vipi upande wenu?
Maana kwangu naona wanazingua kweli kweli!
 
Naanza na no 10. Mwanaume kujishughulisha na Mapambo napenda sana maana haibadilishi asili yake kwamba yeye ni mwanaume.
No 7 pia sioni shida yake kwani Teh teh huwa inatamkwa au inaandikwa?
No 6 pia haina shida salam tuu.

Ha ha ha sawa sawa dada asante kwa maoni
 
Hapo inategemea mtu au watu wenyewe sio wote wavifanyavyo wana nia mbaya au wanafanya kwa madhumuni mabaya wengine ni hulka zao tuu but still wapo normal na ni wanaume rijali
 
Hakuna jambo la ajabu hata moja kama ungesema wanaume kuongozana huku wameshikana viuno, au wanazungusha nyonga kama wanawake ningeshtuka na kukuunga mkono.
 
Labda tungejua kwanza tafsiri ya neno mwanaume nahisi ingekua bora zaidi
 
Sioni shida yoyote hapo labda kwa kuwa wewe in wa mikoani pia acha kudharau kazi ya mtu kwani kupamba or kuremba wanawake(wamasai) hufanya wapoteze uanaume wao?tena wao huwa na bahati ukamua wanawake zenu hatarii

Mleta maada naona bado una ubaguzi wa kijinsia hivi kukaa na wanawake kuna kubadilisha jinsia wakati nasoma chuo group letu loote walikuwa wanawake kasoro me na nilibamiza wote na mpaka Leo wananishangaa.

Pia kushikana mikono sioni madhara yoyote kwan wana Ebola? kuhusu kucheka hiyo ni hulka ya mtu.

NB:Tambua binadamu tunatofautiana kile ambacho wewe unaona siyo sahihi wenzako ukiona sahihi and Vic vesa iz true!!!
 
Mmh wewe tu unataka kujipa stress kwa maisha ya watu na hii ni dalili kwamba huna shughuli za kufanya umekalia kuchunguza wanaume wenzio.

Na hiyo namba mbili wacha uongo sio kabila hilo pekee wana andika hivyo. Teh teh.
 
6.kuvaa skin jeans na kujipaka lipstick shedo na marashi ya kike na kupaka make up
 
Back
Top Bottom