Hizi taarab zenu zimejaa matusi mno!

Hizi taarab zenu zimejaa matusi mno!

Kama wew si mpenzi wa taarabu waachie wahusika kwani lazima tupende vitu unavyopenda
mkuu, mimi nawatetea watoto wadogo wanaoharibiwa na hiyo mitusi ya taarab zenu za kipuuzi.
 
Kumbuka na mwanaume ana nyama ,roho kama ya mwanamke kwa hiyo ana kila aina ya kitu kukipenda kama wanavyopenda wanawake
kwa hiyo kwa kuwa wanaume nao wana roho ndio wavae sketi, mikufu, hereni na kusuka nywele kama wanawake wanavyoshobokoa taarab ama?
 
ivi sio paka nipagawe?? au mi nackiaga vibaya? maana huku uswaz ukpta mtaani tu utazckia
 
Teh tehh. Hata mimi sio mpenzi lakini nimejikuta nacheka. Jana mimemsikia mzee yussuf anasema kitu kama kwishnei ----. Nikastuka. Anyway nikasema na baridi hii nisije kuwa naskia kitu roho inapenda kimbe sio.
Pole ila ungenijulisha tu ningekuja kukurescue
 
Ijapokuwa mimi sio mpenzi wa haya manyimbo ya taarab lakini nimepata kusikia kipande kwenye mashairi ya mzee yusuf ambayo yamenisikitisha sana.

Mzee yusuf (MY) alikuwa akiimba huku akiitikiwa na dada (DD) mmoja:

MY: Mpenzi wangu nipe rahaaaa!

DD: Nipe raha mpaka nikojoeeee!

Ndugu zangu, hii maana yake ni nini? Kwa nini jamii inalazimishwa kusikilizishwa matusi huku vyombo vinavyohusika na sanaa nchini (BASATA na/au COSOTA) vikiwa kimya?

Na ni bahati mbaya kwamba wadau wakubwa wa hizi taarab ni kinamama na watoto. Tunawafundisha nini watoto wetu kwa hizi nyimbo za matusi?

MAJANGA!
yani avatar yako tu inaonyesha.. umekerwa
 
Mmmmh, huo wimbo mbona hauna tabu kabisa..... Sema wewe umetafsiri hivyo. Lakini ukiisikiliza nyimbo yote hayo mashairi yana mafumbo mengi ambayo kila hadhira itatafsiri kivyake. Ndio kukua kwa lugha huko mkuu. Unakumbuka ile nyimbo inasema, "ukifika gonga mbele mara tatu...... na ukichoka au kushindwa gonga nyuma mara tatu, na ukishindwa mwaga mzigo hapo hapo utakuwa umefika....." Upo hapo..?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom