Hivi kwanini "Bongo fleva" zimejaa mashairi yanayoashiria matusi, uzinzi na uasherati?

Son of Gamba

JF-Expert Member
Oct 26, 2012
3,248
2,000
Siku hizi imekuwa kero kuzisikiliza baadhi ya nyimbo nyingi za muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania kwani nyimbo hizi zimejaa mashairi yaliyobeba maudhui yenye matusi. Mbaya zaidi nyimbo hizi zinapigwa tu kwenye vituoa mbali mbali vya redio, na kila mtu anasikiliza bila kujali kuna watoto au la.

Kuna huu muziki wa Harmonize na Diamond unaitwa "Kwangwaru", baadhi ya mashairi yake yanatia kichefuchefu; kuna mahali anasema;

"nipatie vya kitandani, nipe mpaka kwenye kiti,........ kitandani nikoleze kwa mauno ya Kingoni....weka mate niteleze kama nyoka pangoni"

Hayo ni matusi matupu, sasa hebu ona na huyu naye anavyosema kwenye muziki wake. Huyu anaitwa Aslay akiwa na Nandy, na wimbo unaitwa "Mahabuba";

"weka shuka na kitanda tuje tulale mama, tena ulale na khanga maana nimekumiss sana"

Ukiwa umekaa na mkeo na watoto, unaona aibu kabisa kuusikiliza huu wimbo. Wimbo mwingine ni ule wa Diamond na Rayvanny, unaoitwa "Salome", umejaa mashairi machafu sana, mfano;

"tukimbizane nini Salome wangu hiyo ni michezo ya jogoo, mbona watizama chini Salome wangu ukimwona jongoo, inama kidogo shika magoti, mimi nimesimama kama ngongoti, mtoto jojo siyo roboti, chumbani mbigili mbigili kama somersault..... unantekenyaga ukinyonga Salome...... utamu kolea aprokoto, ting'ali ting'ali ndani kwa moto...... miye bebi kwenye msambwanda, huwa siendagi ngenge ni ngangangaaaa"

Haya yote ni matusi; matusi kabisa. Hivi ukiwa umekaa na mtoto wako na akakuuliza nini maana ya "msambwanda" utamjibu nini??

Kuna wengi tu wanaimba nyimbo za aina hii zilizojaa tungo tata zenye viashiria vya matusi, mfano mwingine ni huu wimbo wa The Mafik unaoitwa "Passenger"; kuna mahali wanasema;

"unanikosha salaleh, unavyonyumbulika nyumbulika on bed eeh....... ukinitazama jicho lako la maringo, mimi ninachapa fimbo, ukiinama ukiinuka fimbo, mimi ninachapa fimbo"

Jamani hakuna mtu asiyeelewa hapa wanamaanisha nini??, ni ngono na matusi na uasherati. Zipo nyingi sana siwezi kuziandika zote na wasanii wanaotunga haya mashairi ni wengi sana. Mimi siyo mzee wala sijapitwa na wakati lakini kwa kweli hali ilivyo sasa hivi inatia kinyaa sana, na inakera sana hasa kama umekaa mahali na watu mnaoheshimiana nao, inakuwa ngumu sana kuvumilia kuzisikiliza hizi nyimbo.

Huu siyo utamaduni wetu kabisa sisi Watanzania, haya ni mambo yaliyokuwa yanafanywa na Wanamuziki hasa wa USA ambao kwenye mashairi ya nyimbo zao, matusi ni kawaida, lakini siyo kwetu sisi, hapana.

Inashangaza kuona BASATA wao kazi yao ni kufungia video chafu na wanasahau hata mashairi pia yamejaa matusi na ngono. Watoto wetu wanajifunza maneno machafu yasiyofaa wakiwa kwenye umri mdogo sana. Tunajenga taifa liliporomoka kimaadili na siyo ajabu miaka 10 ijayo tukawa na kizazi kibovu kabisa katika historia ya taifa hili. Mbaya zaidi ni vigumu sana kuwazuia watoto wasisikilize hizi nyimbo kwani zinapigwa kwenye kila kituo cha redio na Tv, na watu wanaona ni sawa tu.

Binafsi nakerwa sana tena sana, sijui kwa wengine. Sisemi hizi nyimbo ni mbaya, hapana; kwa kweli midundo yake ni mizuri sana, hata zikipigwa unaweza ukashawishika kucheza au hata kutikisa mguu, lakini sasa ukianza kusikiliza mashairi yake, hapo ndipo unachefuka.

Wasanii badilikeni na Serikali nayo iwe makini zaidi katika kukagua mashairi ya hizi nyimbo za siku hizi.
 

niachiemimi

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
3,004
2,000
Hawa jamaa nyimbo zao huwezi kuzitazama au kusikiliza na vijana wako au watu wa heshima. Zina mashairi ambayo ni matusi matupu. Fid q angalau anajitahidi kutunga nyimbo nzuri ambazo hata kama ni za mapenzi lakini hazina matusi.
 

coscated

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
2,750
2,000
Bora matusi ya weusi yameenda shule kidogo kwa akili Ndogo ya mtoto hawezi kustukia
 

RGforever

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
6,895
2,000
Kuna Nyimbo za Kina Rose Muhando...bahati bukuku... Unaweza Ukageukia Huko

Usilalamike sana wakati wewe ndo unaonekana una Tatizo badala ya Nyimbo za Bongo flava
 

Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
8,083
2,000
Kuna ule wimbo wa Dogo Janja..Ngarenaro kuna sehemu anaimba..
"Unanipaga mpaka mambo ya uwani".. Sasa najiuliza mambo ya uwani ndio yapi hayo kama sio kuchezea tope..
 

Son of Gamba

JF-Expert Member
Oct 26, 2012
3,248
2,000
Kuna ule wimbo wa Dogo Janja..Ngarenaro kuna sehemu anaimba..
"Unanipaga mpaka mambo ya uwani".. Sasa najiuliza mambo ya uwani ndio yapi hayo kama sio kuchezea tope..
Sawa kabisa mkuu, hayo mambo ya "uwani" ni yepi hayo kama siyo ule mchezo mchafu uliolaaniwa? Mbaya zaidi nyimbo hizi zimeruhusiwa kuchezwa tu kwenye vyombo vya habari, ni kama vile BASATA hawana masikio.
 

Son of Gamba

JF-Expert Member
Oct 26, 2012
3,248
2,000
Kuna Nyimbo za Kina Rose Muhando...bahati bukuku... Unaweza Ukageukia Huko

Usilalamike sana wakati wewe ndo unaonekana una Tatizo badala ya Nyimbo za Bongo flava
Tatizo langu nini mkuu? Au wewe unaona ni sawa tu waendelee kuimba "matusi"?
 

Son of Gamba

JF-Expert Member
Oct 26, 2012
3,248
2,000
Ndio AKILI nyingi za wabongo zilipolalia. Ndo mana SIKINDE imekufa. MSONDO imekufa! ZIlikuwa haziimbi huu ujinga!
Kweli kabisa mkuu, mimi huwa najiuliza hivi hizi bongo fleva zinafaa kweli kufundishia "fasihi" kama zilivyokuwa nyimbo za kina "Marijani"? Miaka 30 inayokuja vijana wetu watajifunza nini kutokana na hizi bongo fleva?
 

goldie ink

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
5,656
2,000
Mkuu....
Umenena vyema lakini hatuwezi kubadilika kulingana na teknolojia na utandawazi kwa sasa, acha vijana waimbe nyimbo zenye kufikisha ujumbe katika jamii.
 

Darmian

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
10,044
2,000
Sawa kabisa mkuu, hayo mambo ya "uwani" ni yepi hayo kama siyo ule mchezo mchafu uliolaaniwa? Mbaya zaidi nyimbo hizi zimeruhusiwa kuchezwa tu kwenye vyombo vya habari, ni kama vile BASATA hawana masikio.
Kuna moja tena ya msanii anaitwa motra the future na yeye anasema msambwanda mara nipe mpaka tope..sasa mtu unawaza tope si ndo anamaanisha ndogo..kwa kweli miziki ya bongo fleva mingi ni ushetani waziwazi,hakuna kitu kabisa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom