souljah meditater
JF-Expert Member
- Oct 15, 2012
- 2,146
- 2,103
Mkuu mshana mi niliota nakimbia ila hatua nilizokuwa napiga zilikuwa ndefu sana yaani napaa kama natembea mwezini
View attachment 421080Ni usiku mwingine tena tunapojiandaa kupumzika vitandani mwetu ( hata kama ni ugenini gesti house au barabarani kuna dakika chache utalala kidogo na kuota)
Ndoto njozi na kuota ni hitaji la kawaida la mwanadamu, shida ipo ni je unaona ndoto za aina gani?
-unaota ndoto za kawaida kutokana na harakati za kawaida za kimaisha kutokana na fikra mawazo matendo na maono?
-Ama la unaota ndoto taarifa au ndoto ujumbe au ndoto maono? Ndoto zenye ujumbe maalum?
- Au je unaota zile ndoto zile ambazo si ndoto bali ni matendo ya giza? Ndoto za
Kuota umelazwa kwenye jeneza
Kuota unazama/unazamishwa baharini
Kuota unakula/unalishwa nyama
Kuota unang'atwa na mdudu na unapata maumivu mpaka asubuhi
Kuota unakimbizwa au kufukuzwa
Kuota umefungiwa kwenye kiota chupa nk
Ndoto zote hizi huwa live mpaka asubuhi au unapostuka na unakumbuka kila kitu saa nyingine hata uchovu maumivu na Ladha....!
Ndoto za namna hii si ndoto za kawaida na huambatana na mambo yako mengi kuharibika! Hizi ni ndoto za kufanyiwa mambo mabaya na watu wabaya
Ukiweza jitahidi kuchunguza ndoto zako leo na siku zijazo utagundua kitu View attachment 421088
Mshana jr, mie tokea mama yangu alivyofariki huwa kila mara namuota tena ndoto za Enzi nilivyokuwa mdogo, na weza kuongea naye kama vile yupo na hata kumueleza yanayonisibu au hata furaha yangu yaani ANAKUWA KAMA VILE YUPO TU
Hizi ndio zile ndoto taarifa au ndoto maono! Kama ungejaribu kuwaambia ungeambulia kuambiwa una mdomo mbayaMimi jaman nikiota ndoto hua inatokea kweli niliahawah kuota mtt wa dada yangu amefarik kwel baada ya cku3 akafarik...niliwah kuota mama mdogo amefarik kwel baada ya mwez akafarik..Wa mwsho nilishawah kuota mama yangu amefarik nikalia mpaka nmezimia na kwel akafarik nilivyoota kwny ndoto ndivyo ilivyotokea kwa kwel mpaka naogopa.
Hizi ndio zile ndoto taarifa au ndoto maono! Kama ungejaribu kuwaambia ungeambulia kuambiwa una mdomo mbaya
Yaaani mimi hadi nafurahi, maana naongea naye, namweleza jambo lolote linalonisibu ananishauri, yaani tunaongea utadhani kweli yuko hai! Yaani kuna wakati huwezi kuamini hadi ananiambia hapo unakosea fanya hivi fanya hivi.Sio ww peke yako hata mm tena mama yangu naongea nae akiwa amevaa mavaz meupe na anaonekana bado msichana huku anatabasamu
Yaaani mimi hadi nafurahi, maana naongea naye, namweleza jambo lolote linalonisibu ananishauri, yaani tunaongea utadhani kweli yuko hai! Yaani kuna wakati huwezi kuamini hadi ananiambia hapo unakosea fanya hivi fanya hivi.
Mwee Jamani mama yangu upumzike kwa amani, alikatika kama glass ghafla eti moyo valvu ziliachia🙁🙁🙁🙁
Ni fikra zilitengeneza uhalisia halafu zikawa ndotoMkuu mtani nilikua nasoma hadithi usiku inayohusu joka chatu afu usiku huo nikaota amenigonga maeneo ya mgongoni na nilipata maumivu sana akaniachia sumu nyingi niliposhtuka nilikua nimechoka sana sasa nashindwa kuelewa je ni mawazo ya ile hadithi au nini nisaidie hapo mtani mshana
Shukrani mtaniNi fikra zilitengeneza uhalisia halafu zikawa ndoto
Habari,ni Mara ya kwanza kukuona nimefurahi kwakuwa ktk watu wanaoongoza kwa kuota nahisi naongoza duniani:Nina maswali Mengi ambayo sijawahi kupata ufumbuzi:kwa Leo naomba nisaodie kutafsiri hii ndoto:kuna siku niliota nipo shule ya msingi ambayo nilisoma miaka mingi sana,nipo kwenye uwanja Fulani hv sasa ghafla nikamuona Simba dume nikaogopa sana,nikajitengenezea fensi zile za seng'enge haraka nikawa ndani ya fensi Simba nje,ghafla àkaja Mdogo wangu wa kiume ameshikilia bahasha ya kaki mkononi akaruka fensi akaingia ndani,nikashangaa amepitaje huko nje wkt kuna Simba?View attachment 421080Ni usiku mwingine tena tunapojiandaa kupumzika vitandani mwetu ( hata kama ni ugenini gesti house au barabarani kuna dakika chache utalala kidogo na kuota)
Ndoto njozi na kuota ni hitaji la kawaida la mwanadamu, shida ipo ni je unaona ndoto za aina gani?
-unaota ndoto za kawaida kutokana na harakati za kawaida za kimaisha kutokana na fikra mawazo matendo na maono?
-Ama la unaota ndoto taarifa au ndoto ujumbe au ndoto maono? Ndoto zenye ujumbe maalum?
- Au je unaota zile ndoto zile ambazo si ndoto bali ni matendo ya giza? Ndoto za
Kuota umelazwa kwenye jeneza
Kuota unazama/unazamishwa baharini
Kuota unakula/unalishwa nyama
Kuota unang'atwa na mdudu na unapata maumivu mpaka asubuhi
Kuota unakimbizwa au kufukuzwa
Kuota umefungiwa kwenye kiota chupa nk
Ndoto zote hizi huwa live mpaka asubuhi au unapostuka na unakumbuka kila kitu saa nyingine hata uchovu maumivu na Ladha....!
Ndoto za namna hii si ndoto za kawaida na huambatana na mambo yako mengi kuharibika! Hizi ni ndoto za kufanyiwa mambo mabaya na watu wabaya
Ukiweza jitahidi kuchunguza ndoto zako leo na siku zijazo utagundua kitu View attachment 421088
Nyoka alikuwa wa rangi gani? Na hao wadudu wengine walikuwa ni wadudu wa namna gani?Mimi niliwahi kuota hivi,kuna jirani yetu alikuwa na kijana wake sasa yule kijana ile siku ikatokea akawa anampiga sana mtumishi wao wa ndani na yule mtumishi akawa anapiga kelele sana,ikanibidi nitoke kwenda kumsaidia ila nkiwa njian nkapita sehemu palikuwa na wadudu wengi sana na miongoni mwao walikuwa ni nyoka na hapo ndipo nyoka mmoja akaniuma mguuni na katika ndoto ile wala mimi sikujali nikaendelea na safari yangu ila nkiwa na kumbukumbu kwamba nyoka kaniuma!!
Mpaka nilipostuka nilikuwa bado naikumbuka ndoto hiyo japo ckuwa na maumivu yoyote,je inawezakuwa ilimaanisha nini!?@Mshana jr