Hizi sekta/Wizara ya Afya na Elimu zimekumbwa na nini siku hizi za karibuni..?

Zekoddo

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
1,831
4,498
Habarini za wakti Wana JF,
On the point, nimekuwa napigwa na mshangao sana kwa haya yanayoendelea katika Wizara zetu hizi nyeti ambayo ni Afya na pacha wake pia Elimu.

Nianze kuzungumzia sekta ya Afya ambayo imekuwa muhanga wa hii kadhia,, hivi karibu kumekuwa na mambo mbalimbali ya ovyo ambayo yanayonajisi hii sekta hasa yanajihusisha na utumiaji mbovu wa mitandao ya kijamii(naweza Kusema sekta hii ndio muhanga nambari moja wa athari zinatokana na mitandao ya kijamii.)

Kumekuwa na matukio ya watu kutuma video, clips, picha mbovu kwa mambo mambo mbalimbali yanaendelea huko mahospitalini au vituo vya Afya, turejee kule Tabora, Dada Debora(Afisa muuguzi) na yule Bwana(jina nimelisahau).

Juzi pia Kuna muhudumu wa Afya huko Dar-es-salaam tumeona video yake akifanya majukumu yake kwa muktadha unaonekana ni kinyume na taratibu, Jana pia tumeona Taasisi ya Mifupi(MOI) mgonjwa na muuguzi(Mpenziwe) wakikulana denda😁 wodini na matukio kama hayo kedekede kwenye sekta hii ya Afya.

Hali kadharika sekta ya elimu kumekuwa na matukio kama hayo ya walimu kurekodiwa na kutupiwa mitandao kwa mambo ya kipuuzi.

Najiiuliza kwanini ni sekta hizi tu kuu 2, ina maana sekta/Wizara zote nchi hii hakuna madudu kama haya na kama yapo kwanini hatuyaoni..? Na nini sababu ya wahusika(Recorders & Transfers) kufanya hivyo hali ya kuwa Kuna matukio mengine ni ya kawaida tu Hadi kufikia kuhatarisha ajira za watumishi hao tena kwa vitu vidogo sana(hii ndo furaha yao kuona watu wanafutiwa vibarua vyao..?)

Naona Kuna shida sehemu Fulani kwenye sekta hizi hasa kuhusiana na masuala ya kimitandao kwa watumishi wa Afya na Elimu maana inaonesha dhahiri watumishi wenyewe kwa wenyewe ndio wanaofanyiana haya mambo
Ni wakati Sasa wa mamlaka husika kutibu hii homa kwani huko mbele itafikia pabaya zaidi.
 
Huyo mpenzi wake aliekulana denda una uhakika ni muuguzi ? nguo ya kijani mbona kila mtu anavaa ,na ukiangalia nguo ya chini ina rangi nyingine
 
Huyo mpenzi wake aliekulana denda una uhakika ni muuguzi ? nguo ya kijani mbona kila mtu anavaa ,na ukiangalia nguo ya chini ina rangi nyingine
Muuguzi(mtu anayeuguza mgonjwa) na Wala sio Afisa Muuguzi au vinginevyo.. wewe ukiumwa then ukapelekwa hospital Kuna ndugu/rafiki/ jamaa atakayekuwa anakucare hospital kwa mambo mbalimbali licha ya kutokuwa na Professional na uuguzi.. ndo maana kwenye mabano nikaweka(Mpenziwe)
 
Muuguzi(mtu anayeuguza mgonjwa) na Wala sio Afisa Muuguzi au vinginevyo.. wewe ukiumwa then ukapelekwa hospital Kuna ndugu/rafiki/ jamaa atakayekuwa anakucare hospital kwa mambo mbalimbali licha ya kutokuwa na Professional na uuguzi.. ndo maana kwenye mabano nikaweka(Mpenziwe)
huyo ni muuguzaji sio muuguzi
 
Back
Top Bottom