Nshomile wa Muleba
JF-Expert Member
- Dec 5, 2015
- 2,165
- 5,551
Habarini?
Mpaka sasa kuna kadirio la almost 100,000 graduates wa vyuo vikuu na vya kati nchini Tanzania KILA MWAKA, jambo ambalo linapelekea idadi ya watu ambao hawajaajiriwa kuwa kubwa “jobless”
HOJA YANGU INATOKEA HAPA
Mfano mdogo tu;
Mtu anaajiriwa serikalini kama afisa ugavi lets say akiwa na miaka 25, Huyu mtu atakaa kazini mpka miaka 65(kustaafu) hapo nimeondoa dhana za kujiuzulu, kifo na kutenguliwa.
Unakuja kupiga hesabu unaona NAFASI MOJA IMEKALIWA NA MTU MMOJA KWA MIAKA 40.......MIAKA 40 guys, ndipo huyu mtu atoke na nafasi yake ijazwe na mwingine, sasa rejea chuoni
Kwa mwaka wanao-graduate vyuoni kozi ya “Afisa ugavi ni wangapi? ( tuweke mfano kuwa wanagraduate 1000 kila mwaka)
chukua hao graduates zidisha na miaka 40 ambayo yule mtumishi aliajiriwa, unapata watanzania 40,000 ( nimechukulia mfano wa nafasi moja )
uone how much tunatengeneza majobless nchini kwetu.Je? nchii hii inakwenda wapi.
Naweza nsieleweke na watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri ila wale wenye upeo mpana washajua nini kinaongeleka.
HITIMISHO
Nashauri ajira serikalini ziwe za mkataba wa muda maalum ili baada ya kumaliza muda wake awapishe wengine walau na wao waje wapate ajira hiyo,
zifuatazo ni faida ambazo tunaweza kuzipata;
(i) itamfanya muajiriwa wa serikali asibweteke muda mrefu na muda wote akili yake itakuwa inawaza njia mbadala za kipato.
(ii)itapunguza wizi na ubadhilifu serikalini kutokana na waajiriliwa kukosa muda wa kutosha kutengeneza mianya ya kuiba pesa za umma.
(iii)itatoa “equal opportunities” kwa watanzania wote kupata nafasi hiyo kwa “different intervals”
(iv) keki ya taifa italiwa na kila mtu na siyo mtu mmoja miaka kibaaooo.
(v) Waajiriliwa watatengeneza mitaji ili wanaopoondoka wakajiajiri kupitia kilimo,biashara na n.k kupitia mishahara yao wakati wapi ajirani.
(vi) Itapunguza jeuri za baadhi ya waajiriwa kujiona “MIUNGU WATU” na itajengeka dhana kuwa nafasi ya ajira serikalini ni KUTUMIKIA UMMA na si kunyanyasa raia.
(vii) Tutatengeneza dhana ya kuwa elimu si kuajiriwa tu bali hata kujiajiri toka mashuleni kutokana na ajira za mikataba
zingine mtajazia
USHAURI
Nafahamu mfumo kama huja na changamoto nyingi ila naamini faida ni nyingi kuliko changamoto zake.
(PIA DHANA HII HATA KWA WANASIASA ITAKUWA NZURI MFANO UBUNGE KUGOMBEA IWE MIAKA 10 KAMA UKOMO BAADA YA HAPO APISHE VIJANA WENGINE).
Mwalimu wa walimu
Nawasilisha