Naomba mchanganuo KAMA CHARITY BEGINS AT HOME nielezwe kwa miaka 25 EL akiwa mbunge wa monduli kuna upungufu wa umaskini kiasi gani au maendeleo kiasi gani ukilinganisha majimbo mengine?
Mimi sijazaliwa monduli ila nimekulia Monduli nimeishi pale kwa miaka 15.
1. Monduli barabara ni nzuri, monduli mpaka arush mjini ni mkeka mtupu... barabara za lami katikati ya wilay na nje ya wilaya. barabara nyingi zinapitika.
2. Maji. Miaka ya 90 monduli kulikuwa kuna shida kubwa ya maji. mm kipindi hicho kulikuwa na mabomba ya vijiji... yaan ilikuwa inabidi mtu atembee umbali mkubwa kwenda kuchota maji kwenye mabomba ya vijiji ambayo yalikuwa machache na kuhesabika...
Ila sasa hivi dakika hii EL amesaidia visima vya maji vimechimbwa vile vile amesaidia kapeleka maji kayatoa Meru, Meru ni mbali sana. maji hayo yanasaidia mpka maeneo ambayo yapo nje ya jimbo. sasa watu wengi wana maji mpaka majumban kwao hakuna tena matesao ya kutembea umbal mrefu.
3. Elimu. EL amekuwa mlezi mzuri wa chuo cha ualimu monduli, waliosoma pale mashahidi.
EL amewalipia ada za shule watoto wengi wasiojiweza.
EL alisaidia kuanzisha Chuo cha ufundi monduli FDC,
EL alisaidia sasa hivi kuna chuo cha CDTI
kwenye jimbo la EL kuna shule nyingi za msingi na sekondari kiasi cha kutosha kushinda majimbo mengi tu
na mengine mengi
4. umeme.. umeme sasa sio shida maeneo yote muhimu na mengi yenye makazi ya watu kuna umeme.
5. Afya. Monduli hospital zipo zahanati pia zipo za kutosha... majuzi tu hosp ya wilaya ya monduli imepandishwa hadhi na kuwa hospt ya rufaa kama KAMA SIKOSEI.. Ila nina uhakika imepandishwa hadhi.
6. Ufugaji..Monduli ni moja ya maeneo machache niliyoona maafisa mifugo wapo active kwa kiwango kikubwa.
EL amesaidia ujenzi wa mabwawa na majosho wamasai wa monduli haswa lashaine ni mashaihid wengi wamenufaika na moja ya mabwawa lililojengwa jiran na sehem nliyokua nikiishi.
mkuu kama una swali uliza ntakujibu kulingana na xperirnce yangu ya monduli chini ya uongoz wa mh. EL