Hizi ni hoja zilizoibuka mara tu baada ya Kikwete kumaliza hotuba yake! Wewe una hoja gani?

Acha kudanganya watu sisi watanzania tunataka serikali mbili,wewe na kina Waioba ndio mnataka serikali 3 ili mvunje muungano wetu na kutuletea shida na taabu ambazo hatujawahi kuzipata.Watu waliohojiwa hawazidi 400,000 sisi watanzania tuko milion 45 sasa msitupeleke kubaya kwa ajili ya tamaa zenu.Mmeshindwa na mtashindwa.

Walioleta muungano wa serikali mbili walikuwa wangapi?
 
Tutakwenda bungeni jumatatu na rasimu ya Jaji Warioba. Lakujadiliwa ni rasimu ya warioba. Mulimsikia jaji Amos Wako kutoka Kenya alivozungumza?. Aliwaeleza kuhusu ugumu na matatizo ya chama tawala kupania uongozi.Wakijaribu kushindana, katiba haitopita halafu tutaanza upya lazima wakubali maoni ya wanachi.
 
Acha kudanganya watu sisi watanzania tunataka serikali mbili,wewe na kina Waioba ndio mnataka serikali 3 ili mvunje muungano wetu na kutuletea shida na taabu ambazo hatujawahi kuzipata.Watu waliohojiwa hawazidi 400,000 sisi watanzania tuko milion 45 sasa msitupeleke kubaya kwa ajili ya tamaa zenu.Mmeshindwa na mtashindwa.

Unahofia kuvunjika muungano wa Tembo na sisimizi! By the way ni Wazanzibar wengi ndio wasioutaka muungano na ndio maana Watanganyika hawatakiwi Zanzibar. You have nothing to lose or gain my friend. Unless uwe ni Mzanzibar...
 
Umeongea vizuri ila kuna sehemu ndogo umeharibu maana nzima ya mawazo yako neno dikiteta nyerere hakuwa dikiteta onndoa hiyo ila ni mawazo ya wakati ule usije ukatukana ww unaweza mwambia baba yako kwamba baba ungechelewa kunizaa ningekuzaa mimi ni hivyo tu
 
Rais kikwete wananchi tulishamaliza kutoa maoni kwa tume.usiturudishe nyuma.rasimu iliyopo ina maoni ya wananchi.nashangaa leo unatudharau wananchi.na dharau za wana ccm zinakera sana.kama jimbo la chalinze lililotoa rais leo huko hamna amburance tulisikia mwanao anaahidi unategemea ccm mna nia ya dhati na sie?.pitisheni serikali 2 muone mziki wake.leo hautaki ukomo wa ubunge kwa kuwa unataka mwamao riz awe mbunge wa maisha chalinze.hatukubali.
Wewe ni zuzu, nitajie ni watu wangapi huku Kigoma,Rukwa,Mbeya na Ruvuma walipendekea serikali tatu?
Hao wananchi wa kufikirika wa warioba wako wapi?

Hata kijijini kwake Nyamuswa Bunda hakuna hata mmoja aliyetaka serikali tatu.
 
Acha kudanganya watu sisi watanzania tunataka serikali mbili,wewe na kina Waioba ndio mnataka serikali 3 ili mvunje muungano wetu na kutuletea shida na taabu ambazo hatujawahi kuzipata.Watu waliohojiwa hawazidi 400,000 sisi watanzania tuko milion 45 sasa msitupeleke kubaya kwa ajili ya tamaa zenu.Mmeshindwa na mtashindwa.

Tumia akili ndg yangu si miguu kufikiria.watanzania waliojiandikisha kupiga kura ni milion 21,waliomchagua jk mbali na kuiba ni milion 4,je utasema si rais wetu?milion kama 13 hawakupiga kura.
 
Lakini unawezaje kuwa na rais wa muungano asiye na ardhi? Anapo kwenda bara anakua mgeni, akifika visiwani alkadharika

hapana hawezi kuwa mgeni kwa sababu madaraka yake yatakuwa kama mwanaume mwenye wake wawili bi mkubwa na bi mdogo..so akienda tanganyika au znz pote kwake..
 
Nakubaliana na JK! Watu wanataka Katiba iwaletee maisha bora ndio maana wengi hawakuzungumzia juu ya Muungano! Washabiki wakuu wa Muungano wa Serikali 3 ni wale walafi tu wa madaraka, hawana lolote!

Tatizo JK kuna mambo haileweki,mbona Wakulima wanaotaka Maisha bora wametoa maoni kuhusu ruzuku ya mbolea na masoko,JK kaona itakua mwisho wa Ahadi zao kila siku,"eti Nchi haitoi pepo,ila kuwalubuni kuwa pepo itakuwepo siku moja ni jambo jema"
 
Acha kudanganya watu sisi watanzania tunataka serikali mbili,wewe na kina Waioba ndio mnataka serikali 3 ili mvunje muungano wetu na kutuletea shida na taabu ambazo hatujawahi kuzipata.Watu waliohojiwa hawazidi 400,000 sisi watanzania tuko milion 45 sasa msitupeleke kubaya kwa ajili ya tamaa zenu.Mmeshindwa na mtashindwa.
hivi unafahamu maana ya sampling ungekuwa unajua usingeadika uharo hapa unatujazia server
 
Serikari 2 ndiyo maoni yangu sababu itakuwaje tujitenge ndugu wa kihistoria. Mfano nenda visiwani kule wakazi walio wengi ni. WANYAMWEZI WANDENGELEKO, WANYAGATWA, WASUKUMA, WAMASAI, sasa hawa ndugu zetu tunawavua ubara na kuwapa visiwani. Alafu ukija huku bara wengi tu watu wa Zanzibar na wanamiliki raslimali nyingi tu. Kwa hiyo tukiwa serikali 2 undugu utakuwepo na muungano utakuwepo. Serikali 3 ina maana kila nchi itakuwa na wakazi wake kwa hiyo yule ambae si mwananchi wa upande husika itabidi aondoke mara moja. Na kuacha mali zoote alizochuma kwa jasho lake. Na hakuna NCHI SERIKALI 3 UTAIFA MMOJA AU URAIA MMOJA HAKUNA DUNIANI KOOOTE
 
Serikali tatu ndo jibu. Kuanzia jana nimehitimisha kwamba JK hana jipya na anazidi kuiharibu nchi yetu.

Naomba amalize tu muda wake aende ajuapo.
 
Hivi hata Rais wetu hajui kama kuna Tanganyika mpaka anahoji kuwa imezuka kutoka wapi! Kweli kuna Tanzania bila Tanganyika? Tusidanganyane. Yale tunayoyabaini kuwa yanaweza kuhatarisha Muungano, Bunge maalum liyafanyie kazi. Lakini hakuna muungano wa Tanzania bila Tanganyika, ni uongo.
 
Tatizo Muda Mwingi Ameutumia Kuvunja Na Kuikosoa Hoja Ya Serikali 3!! Na Kuifanya Ionekane Haina Mashiko Kabisaaa!! Pia Kutaka Wajumbe (Wabunge) Kuipuuza!! Nazidi Kupata Shaka Zaidi, Hata Pale Alipojaribu Kuzivunja Zile Hoja Za Ukomo Wa Vipindi Vya Ubunge! Na Ile Ya Mawaziri Wasitokane Na Wabunge!! Eti Wananchi Wamezoea Kuwaona Mawaziri Wakiwa Mjengoni, Wakijibu Na Kuhenyeshwa Kwa Maswali!! Hoja Ambazo Hazina Mashiko Kabisa! Ukomo Wa Ubunge Nao Utafanya Hao Viongozi Wataokosa Uzoefu!!
 
Mie nafikiri hawa wanafiki wa ccm wakiipitisha rasimu ya serikali mbili, hawatakuwa tena na dhamana ya kuchaguliwa viongozi 2015.

Haiezekani wananchi tutoe maoni halafu yapuuzwe kiasi hiki tena na kiongozi mkubwa wa nchi.

Rais jana kaja akiwa na majibu, tena kadesa yale alosema warioba. Ni wazi hana jipya huyu na maccm wenzake
 
Back
Top Bottom