Hizi ndizo Ibada 3 za Kingono zinazofanywa Kimila barani Afrika

Mcanada

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
982
1,904
Habari zenu wanakijiji cha Jamii Forums leo bhana nimewasogezea Ibada 3 za kingono zinazofanywa kimila na baadhi ya jamii barani Afrika.. lengo la hii thread si kwa nia ya kuchafua jamii hizo au waafrika bali lengo ni kujifunza tu maana kujifunza hakuna mwisho ..haya twende kazi...

1. IBADA YA KUPIMA UBIKIRA (Virginity Testing)
1 Sex-rituals.jpg

Hii ni ibada ya kimila Inayojulikana kama Umhlanga(Kwa lugha ya kizulu), kupima ubikira ni utamaduni maarufu nchini Afrika Kusini, hasa miongoni mwa kabila la Wazulu ambao wanaishi hasa katika jimbo la KwaZulu Natal. Licha ya majaribio mengi ya serikali ya Afrika Kusini kuharamisha ibada hii, Ibada ya Umhlanga bado ni sherehe maarufu inayofanyika kila mwaka katika jamii ya Kizulu na jamii zingine.

Ili msichana yeyote ashiriki katika ibada hii, ubikira wake lazima upimwe na mpimaji ubikira aliyehitimu mafunzo maalumu(a qualified virginity tester) na upimaji huo unafanywa katika chumba maalumu kilichotengwa ambapo Msichana anayepimwa ubikira hulala chali na miguu yake kuiweka wazi. Kisha mpimaji hufungua uke wake kwa mikono yote miwili na kutazama ndani, ili kuona kama kizinda(hymen) chake kiko sawa . Ikiwa kila kitu kiko sawa, msichana anapewa cheti maalumu cha ubikira.

Watu wa jamii inayofanya Ibada hii wanadai kuwa mila hii inasaidia kukabiliana na kuenea kwa VVU/UKIMWI kwa sababu ibada hiyo ni sehemu ya kuwashinikiza wasichana wadogo kujiepusha kushiriki hovyo vitendo vya ngono katika umri mdogo hata watakapofika kwenye umri wa uzee.

Hata hivyo ibada hiyo imekosolewa sana na mashirika mbalimbali ya haki za binadamu na mashirika ya kutetea haki za wanawake, huku baadhi ya watu wakisema kuwa ni ibada ya kimila barani Afrika inayodhalilisha wanawake.

2. IBADA YA UTAKASO WA KINGONO (Sexual Cleansing)
2bb.png

Ibada hii kwa lugha ya kitamaduni inajulikana kama "Kusasa Fumbi," ni ibada maarufu ya kimila inayofanywa katika nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Malawi, Zambia, Kenya, na n.k

Wakati wa tambiko wa ibada hii mwanamke anatakiwa kufanya mapenzi na mtaalamu wa ngono wa kiume (professional male sex worker) ambaye kitamaduni anajulikana kama "fisi." (“hyena.”)

Ibada hii hufanyika wakati ambao msichana anavunja ungo (anapata hedhi ya kwanza ya ubinti), mwanamke aliyeolewa amepoteza mume wake(kwa kufariki), au baada ya msichana au mwanamke kutoa mimba.

Kwa mwanamke Mjane Ibada hii inafanywa na mwanaume aliyechaguliwa na mkwe wa mjane. Na wakati wa ibada hii Fisi hawatakiwi kutumia aina yoyote ya kinga wanapofanya ngono jambo ambalo ambalo limekuwa sababu kubwa ya kuenea kwa VVU, mimba zisizotarajiwa na magonjwa mengine ya zinaa.

3. IBADA YA KUIBA MKE (Wife Stealing)
3 chad-wodaabe-girl-selects-man-retreats.jpg

Wizi wa mke ni tambiko au ibada inayofanyika kila mwaka na kabila la Wodaabe, kikundi kidogo cha kabila la Fulani linalopatikana katika eneo la Sahel. Wanawake kutoka jamii hii wanaruhusiwa kuwa na waume wengi kadri ya wanavyotaka.

Wakati wa sherehe ya ibada hii ambayo hufanywa kwa siku kadhaa, wanawake wanatakiwa kuchagua wenzi wao wanaowapendelea kutoka kwenye kikundi cha wanaume ambao hucheza ngoma kwa mitindo ya kuvutia kwa matumaini ya kuchaguliwa ili waweze kujamiiana na mwanamke husika.

Mwanamke anaweza kuchagua wenzi wengi apendavyo na kufanya nao ngono kwa wakati mmoja kabla hajapatana na mmoja kati ya hao ambao amefanya nao ngono ambaye yeye ndiye atakayekuwa mwenzi wake mpya wa maisha.

Jambo la ajabu kuhusu ibada hii ni kwamba haijalishi mwanamke huyo aliyeshiriki ibada hii ameolewa kwa muda gani; mara anapomchagua mwanamume mmoja katika wengi aliofanya nao ngono watu wa kabila hilo hukubali muungano huo mpya na kuuchukulia kama ndoa ya kweli.

Kutoka Finland mji usiojulikana ni mimi Mcanada..
 
Hiyo ya kuiba mke hatari embu fikiria mnamwibia Raisi mke! First lady anaibiwa na Mshana Jr
 
mbona mnaonyanduana wanaume kwa wanaume na mnaoana kabisa hamsemi kama ni ujinga? kwa mtazamo wangu wa kawaida sana nasema kuna mila za kishenzi kuliko hizo, inawezekanaje mwanamke anaoa mwanamke mwingine ama janaume linaolewa na janaume lingine, wazungu ndio majibwa kabisaaaaa
 
Back
Top Bottom