2019
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 2,982
- 4,458
Kwanza natoa pale kwa upinzani hasa CHADEMA kuwa uchaguzi huu sio kama 2015 ambapo kila mtanzania alikuwa amechoshwa na CCM.
Na kila raia alikua tayari kwa lolote ikisubiriwa kauli tu kwamba sasa tuingie barabarani tukichafue.
1. Baada ya Magufuli kuingia 2015 akafuta kazi migambo wote. Hapa wale vijana wasiokuwa na ajira walijiajiri na kufanya kazi kwa uhuru bila bugdha(2015 walikuwa tayari hawa n ni wengi mno)
2. Amefanikiwa kudhibiti matumizi makubwa ya serikali na kubana matumizi.
3. Kuanzisha miradi mingi ya maendeleo. Reli,anga,kuhamia Dodoma, ujenzi wa barabara nyingi
4. Kuondoa baadhi ya urasimu katika ofisi za serikali pamoja na kuwa karibu wananchi. Hii imemfanya aonekane raisi wa wanyonge kweli kweli.
5. Kuleta heshima serikalini,hakuna tena mambo ya "unanijua mm ni nani"? Kila ofisi ya umma unayoenda unapata heshima na kuthaminiwa kuwa ww ndio boss.
6. Kuwapa watu uhuru wa kufanya biashara popote bila shida( ukikimbizwa na 🐕 rusha mifupa kwa nyuma) kwa sasa hakuna vijana wengi wasio na kazi mtaani kama zamani,kila mtu ana mishe zake utamwambia nani aandamane akusikilize?
Suala la kuandamana linahitaji watu wengi wenye hasira kweli kweli.
MY TAKE:
Magufuli sio malaika au Mungu kwa hiyo ana mapungufu yake. Mapungufu yake hayamnyimi heshima yake ya kuongoza awamu ya pili. Vijana wengi kwa sasa wako huru kufanya kazi au biashara zao bila bugdha yeyote toka serikalini kwanini wahangaike na kuandamana?
Ana mke ana majukumu mbalimbali anawaza kuhusu kesho yake akipigwa kwenye maandamano? Uhalisia wa maisha ya mtanzania ni mitaani na sio kwenye mitandao. Mtu anaishi US eti ana hasira na utawala 🤪! Umemkosea nini