Uchaguzi 2020 Hizi ndiyo sababu zilizompa Dkt. Magufuli ushindi wa kishindo

2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,982
4,457
Kwanza natoa pale kwa upinzani hasa CHADEMA kuwa uchaguzi huu sio kama 2015 ambapo kila mtanzania alikuwa amechoshwa na CCM.

Na kila raia alikua tayari kwa lolote ikisubiriwa kauli tu kwamba sasa tuingie barabarani tukichafue.

1. Baada ya Magufuli kuingia 2015 akafuta kazi migambo wote. Hapa wale vijana wasiokuwa na ajira walijiajiri na kufanya kazi kwa uhuru bila bugdha(2015 walikuwa tayari hawa n ni wengi mno)

2. Amefanikiwa kudhibiti matumizi makubwa ya serikali na kubana matumizi.

3. Kuanzisha miradi mingi ya maendeleo. Reli,anga,kuhamia Dodoma, ujenzi wa barabara nyingi

4. Kuondoa baadhi ya urasimu katika ofisi za serikali pamoja na kuwa karibu wananchi. Hii imemfanya aonekane raisi wa wanyonge kweli kweli.

5. Kuleta heshima serikalini,hakuna tena mambo ya "unanijua mm ni nani"? Kila ofisi ya umma unayoenda unapata heshima na kuthaminiwa kuwa ww ndio boss.

6. Kuwapa watu uhuru wa kufanya biashara popote bila shida( ukikimbizwa na 🐕 rusha mifupa kwa nyuma) kwa sasa hakuna vijana wengi wasio na kazi mtaani kama zamani,kila mtu ana mishe zake utamwambia nani aandamane akusikilize?

Suala la kuandamana linahitaji watu wengi wenye hasira kweli kweli.

MY TAKE:
Magufuli sio malaika au Mungu kwa hiyo ana mapungufu yake. Mapungufu yake hayamnyimi heshima yake ya kuongoza awamu ya pili. Vijana wengi kwa sasa wako huru kufanya kazi au biashara zao bila bugdha yeyote toka serikalini kwanini wahangaike na kuandamana?

Ana mke ana majukumu mbalimbali anawaza kuhusu kesho yake akipigwa kwenye maandamano? Uhalisia wa maisha ya mtanzania ni mitaani na sio kwenye mitandao. Mtu anaishi US eti ana hasira na utawala 🤪! Umemkosea nini
 
KWA Sasa tunamuitaji mtia nia wa ccm moshi, aliehaidi kufunika mlima kilimanjaro na pazia alafu akawambia wajumbe wote wacheke hahahaaaaa kwa pamoja,maana alijua anadanganya Sasa na wewe mkuu.

Kwanza twambie tucheke hahahaaaaa ,maana unadanganya Sana ,uongo siku kizuri naomba ujicheke kwa kicheko kimoja Kama Cha mzee wakuweka pazia mlima kilimanjaro
 
Kuapishwa kwake sio kwamba ataongoza taifa kama Mfalme wa miaka 5 iliopita, kashikashi ya vikwazo na vitimbi vipo "LOADING".

Msione wapinzani na mabeberu wapo kimya, wanatunga sheria za kuujeruhi vibaya huu utawala wa kifalme.

Kwa mwenye akili timamu lazima atambue, mabeberu kamwe hawapotezei "DHARAU na DHIHAKA" wanapofanyiwa, hasa kwa nchi hohehae. So kitakacho fuata ni "VIKWAZO" mpaka bei ya chumvi ifike hata elfu sabini au tisini. Ili sisi wananchi akili itusogee tutambue makosa yetu.

1) Upumbavu wetu wa kutokudai "TUME HURU NA KATIBA".

2) Nyinyi wana lumumba mtambue makosa yenu ya "KUUNGA MKONO KILA KITU". Maana hata mgeambiwa mtoe wake zenu sadaka au mvue suruali, mgeunga mkono.
 
Kawakosea nini hao mabeberu mpaka wampe kikwazo? Hii ni tofauti na Zimbabwe bob. Tuna mali nyingi sana nchii ambazo mabeberu wanazitaka,waweke vikwazo tukimbilie China na Urusi.
 
Usitudanganye bwana. Sababu zilizompa ushindi wa kishindo ni wizi na kuingiza mabox ya Kura vituoni tayari yameshapigwa Kura kwake. Na pia sababu nyingine ni kuwaengua au kuwatoa mawakala almost asipimia tisini vituo vya kupigia kura na kuwaacha mawakala pekee wa ccm. Tatu sababu nyingine ni kuzima mitandao ya kijamii ili wizi ufanyike kirahisi bila watu kujua kinachoendelea. Nayo mwabhatama.
 
Haya sawa baada ya kujua ni wizi wa kura umechukua hatua gani? Kulalamika kwako huku kunasaidia nini?
 
Aya ameiba kwa kishindo fanya unachotaka sasa
Kikubwa umejibiwa hoja yako ambayo kwa sababu ya kudanganywa uliileta bila kujua au ulikua unajua ulitaka kujaribu kudanganya watu. Ni vizuri umejua kwamba watu wanajua lakini hawana namna zaidi ya kuacha maisha yaendelee tu. Shangilieni ushindi wa kishindo, wakati wengine wakilia na machozi yao ni machozi ya samaki yanaenda na maji.
 
Kwanza natoa pale kwa upinzani hasa CHADEMA kuwa uchaguzi huu sio kama 2015 ambapo kila mtanzania alikuwa amechoshwa na CCM.

Na kila raia alikua tayari kwa lolote ikisubiriwa kauli tu kwamba sasa tuingie barabarani tukichafue.

1. Baada ya Magufuli kuingia 2015 akafuta kazi migambo wote. Hapa wale vijana wasiokuwa na ajira walijiajiri na kufanya kazi kwa uhuru bila bugdha(2015 walikuwa tayari hawa n ni wengi mno)

2. Amefanikiwa kudhibiti matumizi makubwa ya serikali na kubana matumizi.

3. Kuanzisha miradi mingi ya maendeleo. Reli,anga,kuhamia Dodoma, ujenzi wa barabara nyingi

4. Kuondoa baadhi ya urasimu katika ofisi za serikali pamoja na kuwa karibu wananchi. Hii imemfanya aonekane raisi wa wanyonge kweli kweli.

5. Kuleta heshima serikalini,hakuna tena mambo ya "unanijua mm ni nani"? Kila ofisi ya umma unayoenda unapata heshima na kuthaminiwa kuwa ww ndio boss.

6. Kuwapa watu uhuru wa kufanya biashara popote bila shida( ukikimbizwa na 🐕 rusha mifupa kwa nyuma) kwa sasa hakuna vijana wengi wasio na kazi mtaani kama zamani,kila mtu ana mishe zake utamwambia nani aandamane akusikilize?

Suala la kuandamana linahitaji watu wengi wenye hasira kweli kweli.

MY TAKE:
Magufuli sio malaika au Mungu kwa hiyo ana mapungufu yake. Mapungufu yake hayamnyimi heshima yake ya kuongoza awamu ya pili. Vijana wengi kwa sasa wako huru kufanya kazi au biashara zao bila bugdha yeyote toka serikalini kwanini wahangaike na kuandamana?

Ana mke ana majukumu mbalimbali anawaza kuhusu kesho yake akipigwa kwenye maandamano? Uhalisia wa maisha ya mtanzania ni mitaani na sio kwenye mitandao. Mtu anaishi US eti ana hasira na utawala 🤪! Umemkosea nini

Ule wa juzi haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box.
 
Kuapishwa kwake sio kwamba ataongoza taifa kama Mfalme wa miaka 5 iliopita, kashikashi ya vikwazo na vitimbi vipo "LOADING".

Msione wapinzani na mabeberu wapo kimya, wanatunga sheria za kuujeruhi vibaya huu utawala wa kifalme.

Kwa mwenye akili timamu lazima atambue, mabeberu kamwe hawapotezei "DHARAU na DHIHAKA" wanapofanyiwa, hasa kwa nchi hohehae. So kitakacho fuata ni "VIKWAZO" mpaka bei ya chumvi ifike hata elfu sabini au tisini. Ili sisi wananchi akili itusogee tutambue makosa yetu.

1) Upumbavu wetu wa kutokudai "TUME HURU NA KATIBA".

2) Nyinyi wana lumumba mtambue makosa yenu ya "KUUNGA MKONO KILA KITU". Maana hata mgeambiwa mtoe wake zenu sadaka au mvue suruali, mgeunga mkono.
Rais Magufuli anafanya mambo yanayowagusa wananchi wa chini kabisa.
Tulio kwenye hayo maisha ndio tunamuelewa... Na vile tunauombea ndio Mungu anavyomnariki
 
Back
Top Bottom