Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 6,860
- 12,293
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ama baada ya salam ningependa niseme ukweli kwamba toka nchi yetu ilipopata uhuru mpaka leo hii CCM imeshafanya mambo mazuri na makubwa sana ndani ya nchi kuliko chama kingine chochote kile Tanzania.
Nitaweka baadhi ya mambo yalifanywa na CCM kupitia picha mbali mbali ili kuwafungua macho wale waliofungwa macho ili wasiweze kuona maendeleo na mazuri mbali mbali yaliofanywa na CCM, na kuwafungua akili wale waliofungwa akili ili wasiweze kugundua ukweli wa mazuri haya.
Bila kupoteza muda naomba nitaje sababu zinazonifanya niichukie CCM leo.
1) Kitendo cha serikali ya CCM chini ya Jakaya Kikwete kuleta maendeleo kwa vijana, kama vile kuwatengenezea mazingira ya ajira mbalimbali, kujenga shule za kata, kusambaza barabara za mitaani, wafanyakazi wa serikali kupandishwa vyeo, kuongezewa mishahara na unafuu wa maisha, vilipelekea wananchi kukipenda chama hicho na kukiona kuwa ni mkombozi wao katika kipindi chote cha maisha yao.
Hii ilijithibitisha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ambapo japo wapinzani walikuwa na wagombea wazuri na wazoefu katika siasa, lakini walishindwa kufutukuta mbele ya chama hicho na kupelekea wapinzani hao kushindwa uchaguzi kwenye uraisi na ubunge.
2) Kitendo cha CCM kuja na mission ya kuwaazima wapinzani mgombea mmoja mwaka 2015, pia kimechangia mimi kuichukia CCM maana kitendo hicho kilisababisha upinzani usambaratike na kuacha mapengo makubwa ndani ya vyama vyao.
Kwa mfano mpaka leo pengo la dr Slaa bado halijazibwa na mtu yoyote ndani ya chama chake cha zamani, japo wenye chama wanajitahidi kupachika pachika watu ili wavae viatu vyake lkn wapi bado viatu vyake vinawapwele pweta na hawajui wafanye nini ili apatikane mtu mwenye mguu kama wake ili viatu vimtoshe.
Hapa sijazungumzia kundi kubwa la wabunge na madiwani lililoondoka na mzee wa mission baada ya kumaliza kile kilichompeleka upinzani. Upande wa pili napo prof akajikuta anabaki mwenyew pale buguruni baada ya wapemba kuhamisha ofisi ya chama chao huko kwao chake chake.
3) Kitendo cha raisi wa awamu ya tano kupitia CCM hayati dr Magufuli kuwapa watoto wa masikini haki ya kusoma bure, kujenga miundo mbinu mbali mbali kama vile kupeleka maji na umeme sehem mbali mbali za nchi, kushusha gharama za umeme na maji, kuwapa wanyonge haki ya kujitafutia riziki zao bila bughuza yoyote, kuongeza ujenzi wa viwanda mbali mbali na kuleta maendeleo ya watu na vitu, kulisababisha watanzania waiamini sana CCM na viongozi wake hadi kupelekea wapinzani kuangukia pua vibaya sana katika uchaguzi wa mwaka 2020, licha ya wapinzani hao kumsimamisha m'beleji mweusi awe mgombea wao wa uraisi, na bila kusahau kusambaza chawa katika mitandao yote ya kijaa wakiwa na ID's tano tano lkn haikusaidia kuwaepusha wapinzani hao na kipigo cha CCM chini ya aliekuwa mwenyekiti wao hayati J.P. Magufuli.
Waswahili wana misemo yao miwili..
(a) dalili ya mvua ni mawingu
(b) nyota njema huonekana asubuhi.
Sababu ya kuweka misemo hiyo ni kutaka kuonesha dalili za CCM kushinda uraisi na ubunge zilianza kuonekana mapema sana kupitia mikutano mbali mbali ya kampeni za uchaguzi mkuu.
Nitaweka picha hapo chini ili wenye akili huru (sio wale wanaoshikiwa akili na mwenyekiti) waweze kuona kilichoendelea.
4) Baada ya hayati Magufuli ambae alikuwa kiboko yao kufariki, wengi tukajua sasa ni zam ya upinzani kunyanyuka tena na maana pengine alieingia angeweza kwenda kinyume na sera za chama, sasa cha kushangaza huyu alieingia nae kaja na mikakati kabambe ya kuwaletea watanzania maendeleo kwa kuendeleza miradi yote ya CCM iliyoachwa na hayati na kaenda mbali zaidi kwa kuhakikisha ifikapo mwaka 2024 na kuendelea kila mwanafunzi wa kitanzania atakuwa anasoma katika mazingira mazuri, na pia maendeleo yatakuwa zaidi ya vile wengi walifikiria. So sioni tena dalili za upinzani kupata hoja nzuri ya kushawishi watanzania au nguvu ya kushinda uchaguzi ujao.
Ushauri wangu kwa vile wananchi wengi wameamua kuendelea kuichagua CCM iendelee kuwaongoza, basi viongozi wa upinzani wasikate tamaa, wakaze buti waajiri lundo la chawa zaidi na ikiwezekana kila chawa amiliki IDs kumi mitandaoni ili waonekane kuwa wapo wengi na pia waje na hoja zenye mashiko ili kuwarubuni wapiga kura vizuri.
Najua sio rahisi kuwalipa chawa wote lkn ili mfike kule mnapotaka kufika inabidi muendelee kuwalipa ili vijana wawe na morali ya kutengeneza uongo kuhusu CCM na kuuleta hapa mtandaoni.
Nawatakieni siku njema. Angalia mikutano ya watu wanaodai kuibiwa kura hapo chini 🤣🤣🤣🤣.