Habarini Wadau,
Ama kabla ya salamu, Binafsi naipenda JamiiForums, imenifundisha kupitia members wake
JamiiForums ina members wengi sana wenye haiba na tabia tofauti.
Humu kuna Waongo, Wapenda sifa, Wajivuni, Wakweli, Wastaarabu, Wakorofi wa maneno n.k
Lakini kuna members karibu kila mchango wao una manufaa kwetu members wengine, aidha michango yao inaburudisha, inatafakarisha au inatufunza jambo
Wengi wa members hawa ni Wakongwe ila pia wanaonekana kuwa na exposure na kufahamu maisha haswa
Kwa namna nyingine unaweza kugundua kuwa wao walienjoy sana maisha tofauti na sisi tuliozaliwa miaka ya karibuni
Nimejaribu kufuatilia michango yao, majibu yao au hata mada zao zimekomaa
Baadhi ya members hao wanaostahili kupewa maua yao ni pamoja na
Pascal Mayalla Kiranga Mohamed Said Nyani Ngabu tpaul CHIEF MKWAWA gwakisa n.k
Unaweza kutaja members wengine unaoweza kujifunza mambo flan kutoka kwao