Uzembe wako ndio Umasikini wako: Kazi hizi za 'Kichovu' zinalipa mno Ulaya/Marekani- Ila uwe 'Kidume' kweli

dalalitz

JF-Expert Member
Sep 6, 2013
3,332
1,862

Salaam,

Kuna watu huwa wanawaponda sana wenzao waliopo Ng’ambo hasa Ulaya na Marekani wakidai kuwa ni ‘Wabeba Maboksi’ tu na hawana lolote. Kituko ni kuwa ukichunguza haohao wanaoitwa Wabeba Maboksi wengi tu ‘wametoboa’ na sasa wana maisha yao mazuri huko waliko.

Mwingine anaweza kunidadisi; Maisha mazuri ninayomaanisha ni yapi?
- Mtu akiwa na Kazi inayomlipa
Familia inaishi vizuri, anayo makazi yake mwenyewe (Nyumba sio kupanga)
Ndoa imetulia, Watoto wanasoma na maramojamoja huyooo vacation huku na kule, atake nini tena?
Ukinibishia kuwa huyu ana maisha mazuri hapo unalo lako linguine, Ila kifupi Mtu huyo katoboa.

Nimetafiti na kuona kuwa zaidi ya hayo yanayoitwa maboksi zipo kazi lukuki baadhi ya sehemu za Ulaya na Marekani ambazo zinalipa vizuri. Uchunguzi wangu mdogo nimeufanya kwa Marekani na hapa nawadondoshea aina, majukumu, changamoto na athari za aina kumi (10) tu za Kazi ambazo Mswahili ukifanikiwa kuipata, ukijizatiti kuifanya kwa weledi basi ndani ya muda mfupi tu sio wewe tena,
Yaani Kibongobongo umeyatoa.

Orodha hii haifuati utaratibu, na pia Kazi hizi ni kwa mujibu wa Idara ya Kazi huko kwa mzee Biden.

Twende sasa;

1. CRIMES SCENES CLEANERS (Watu wa Usafi sehemu za matukio ya Kijinai kama Mauaji/Vifo, Ajali n.k.)
Changamoto ya kazi hii ni kuwa mazingira yake yanazaweza kuchefua. Kazi yenyewe hufanyika mara tu baada ya zoezi la uchunguzi wa eneo husika kwa minajili ya kukusanya ushahidi /taarifa tukio, shughuli inayofanywa na wapelelezi.

Huwa inahusisha kupanga na kuweka sawa mandhari kadiri itakavyoelekezwa. Iwapo unayo shida ukiona Damu inakuchanganya basi Kazi hii haikufai maana itakuwa ni swala la kwaona sana kuona Damu.

Athari/madhara ya Kazi hii ni kuwa inaweza kukusababishia msongo wa mawazo mbeleni.

Mshahara: Kazi hii malipo yake ni $75,000/Mwaka.


2. GARBAGES COLLECTORS (WAZOA TAKA)

Mojawapo ya changamoto za Kazi hii ni Harufu ya taka zilizooza. Pia ni Kazi inayofanyika muda wote bila kujali hali ya Hewa, yaani wakati wa Baridi,Mvua nk. Kwa kuwa mrundikano wa Taka unaweza kusababisha milipuko wa maradhi iwapo utaachwa.

Mshahara: $60,000/Mwaka.

3. OIL RIGS WORKERS (KAZI KATIKA MACHIMBO/VISIMA VYA MAFUTA)
Hii ni Kazi ya ‘Kidume’, inahitajiwa Afya na ari pia kujituma kutokana na mazingira ya Kazi yenyewe. Maisha kwanza ni maeneo ya Maji mbali na Mji Baharini huko na Kazi wastani ni masaa 12 kwa siku. Utakuwa mazingira yenye Joto kali muda mwingi na mazingira hatarishi yenye uwezekano wa kutokea milipuko pia.

Changamoto: Ukiwa mzembe hasa wa kuvaa zana mf. Za kuzui makelele unaweza kupata changamoto ya kusikia mbeleni.

Mshahara: Kima cha chini $40,000/Mwaka.

4. PORTABLE TOILETS CLEANERS (WAOSHA VYOO VYA KUHAMISHWA)
Jombaa hapa una-deal na ‘Nya’ ya Mwanadamu –live kila uchao, Tehee!
Kumbuka Kazi hii inatakiwa kweli ifanyike ndani na pande zote cha Choo husika kisha kupulizia madawa ili kuua vijidudu.

Kuna Mwehu atasema, Ohoo mie siwezi. Nyau Wewe! Amerika na Ulaya hawafanyi kwa kukishika hicho Kinyeshi, ishukuliwe Teknolojia basi, Zipo ‘Pressurized Water Jets’ yaani Dakika tu umemalizana na kimoja unachukua kingine fasta tu huku gear kama zote.

Inakadiriwa unaweza kusafisha Vyoo 50 hadi 60 kwa siku na inakuwa umemaliza siku yako ya Kazi.

Athari:Kwakuwa Kazi yako inakuweka karibu na Kinyesi, unakuwa na hatari ya kuambukizwa maradhi kama Kipindupindu, Kuhara, Kutapika, Typhoid au Homa ya Ini n.k;

Mshahara: Si chini ya $60/Mwaka.

5. CRABS FISHERMEN (WAVUVI WA NGADU/KAA)
Hii ni Kazi ya hatari ijapokuwa malipo ni cheko mpaka basi. Wavuvi wa Kaa wanapambana na nguvu za Asili huko Baharin kama
Hali ya hewa mbaya, mawimbi na madhuruba yote ya Bahari ni za kwao katika kazi hii.

Athari : Uwezekano wa kupata maradhi ya mapafu/upumuaji kutokana na kujiweka muda mrefu katika
mazingira yenye hali ya hewa ya ubaridi na Upepo mkali.

Vilevile Nyenzo za uvuvi usipokuwa makini zinaweza kukusababishia ajali na kupelekea hata hata Kifo.

Mshahara; Unaanzia $60,000/Mwaka.

6. SEWERAGE INSPECTORS ( WAKAGUZI MIFUMO YA MAJI-TAKA)
Hawa nao hufanya Kazi ngumu ya muda mrefu na yenye hatari kubwa. Kufuatilia/kutafuta vikwazo vinavyozuia mfumo kutenda Kazi vyema. Hudumbukia ndani kabisa ya mifereji na wakati mwingine kuogelea kabisa katika maji-taka ikiwemo yenye Kinyesi cha Binadamu au Kemikali za haatari ili tu kuweka mambo sawa ni kitu cha kawaida kwao.

Inahusisha wakati mwingine kufanya kazi chini ya ardhi ambako mwanga au hewa inakuwa ni hafifu na mengine mengi yanayohitaji moyo kweli kuhimili, yote shida Pesa, hizi Pesa jamini.;)

Mshahara: $60,000/Mwaka.

7. COAL MINERS (WACHIMBA MAKAA YA MAWE)

Hii pengine ndio Kazi ya hatari zaidi kati ya hizo nilizotangulia kuziweka. Hasa ukizingatiwa kuwa Makaa ya mawe yana kiasi cha Gesi ya ‘methane’ ambayo inaweza kulipuka muda wowote kwa chanzo kidogo sana hata cha mkwaruzano/mgongano unaoweza kusababishwa na kuporomoka au kugongana kidogo tu kwa Mawe yenyewe kwa yenyewe ambayo huwepo kwenye machimbo hayo ni kawaida.

Athari: Kuvuta na kuingiza ndani ya mwili kwa Vumbi la Makaa husababisha tatizo linaitwa ‘Mapafu meusi’ ambapo Vumbi hilo hujikusanya juu ya mgongo wa mapafu na hivyo kupelekea shida kwenye upumuaji ikiwa ni pamoja na kufutuka kwa vifuko vya hewa katika Mapafu.

Mshahara: $65,000/Mwaka.

8. LANDFILL OPERATORS;
‘Wasaka-Tonge’ hawa sijapata jina/neno lao rahisi kueleweka la Kiswahili, lakini itoshe kusema tu kuwa Kazi yao kuu ni Kuzika na Kufukua maziko ya taka kwa minaajili ya kuzika tena au kuyatumia tena maziko hayo kwa Kazi nyingine.

Taka zinapozikwa na kukaa kwa kuda fulani huoza. Upo utaratibu wa kila bada ya muda fulani wenzetu hufukua maeneo ambayo walizika taka muda mrefu uliopita na kuhitaji kurudia kuweka taka mpya katika kufanya hilo huchimba ama kutanua maeneo/makaburi hayo ya taka ya zamani. Hiyo ndio kazi za hawa wanaoitwa ‘Landfil operators.

Athari: Maeneo haya ya taka ni nyumbani kwa visababishi vingi vya maradhi.
Pia kwenye mrundikano wa maradhi kuna uwezekano wa kuzalishwa Gesi ambayo inaathari kubwa kwa mwanadamu lakini pia milipuko ni kawaida kutokea.

Mshahara: 100,000/Mwaka.

9. ADULTS' ENTERTAINERS ( WAIGIZAJI/WABURUDISHAJI/WAUZA ‘UTRAM’)

Kazi hii haihitaji ufafanuzi mwiingiiii kwakuwa mtu mzima yeyote anajua inahusiana na nini.

Changamoto yake ni kuwa; Mfanyakazi akiajiriwa kwa kawaida hupangiwa nini cha kufanya na nani wa kufanya nae,
Yeye mfanyakazi/muigizaji hachagui nani wa kwenda nae.

Pia maradhi, ingawaje huwa wanapimwa na kufuatiliwa na matabibu lakini bado upo uwezekano wakuambukizana baadhi ya maradhi na kusababishiana madhara ya kimwili. Kwa jinsia zote ( Wazee wa X Mpoooo?)

‘Wafanyakazi wa Utamu’ wamegawanyika; Wapo wanaolipwa kwa kushriki Filamu na wapo wanaolipwa kwa kushiriki na wateja yaani huduma na malipo hapoahapo au wale wa njia ya mtandao/simu/video.

Ingawa inaweza kuonekana kama ni Kazi laini unaambiwa hii si kazi ya lelemama. Kipande tu cha dakika moja (Scene) kinaweza kuchukua masaa kufanikiwa kukikamilisha kwa kupata ‘shoot kali’.

Mshahara: Wale wa Filamu hulipwa Mapesa mengi sana na wale wa kuuza Uroda papo kwa papo vilevile wanatengeneza za kutosha.

Kuna Mpuuzi atataka atajiwe kiasi wanachoingiza, - 'Gerarehia.':D

10. MORTICIANS (WAHUDUMU WA WAFU/MAITI)
Hawa Kazi yao kubwa ni kuhakikisha maiti wapo katika hali nzuri kwaajili ya mazishi/kuagwa. Ni kazi ya hatari kwakuwa muda mwingi inahusisha mazingira yanayoweza kusababisha maambukizo kutoka kwa miili iliyokufa.

Kuwapaka urembo na vipoozi anuai ili Marehemu wavutie ni jukumu lao ihawa waheshimiwa ikizingatiwa kuwa wakati mwingine bidhaa zenyewe zinakuwa na changamoto tofautitofauti na nyingine za kutisha lakini wao watafanyaje? Aliegundua Pesa mwehu sana.

Mshahara: $60,000/Mwezi.

Kuna Mtu atakuja na kusema mbona kulea Vikongwe haipo?,
-Natambua uwepo wake
.;)

KUMBUKA:

Kazi hizi hazihitaji Elimu kubwa sana ingawa shurti upewe muongozo na wajuzi kisha uingie mzigoni.
Pia, kwa Marekani ingawa zinaweza kuonekana kama ni Kazi fulani za chini jua kuwa si yeyote anaweza kupewa Kazi hizi.

Kwahiyo badala ya kuangalia Pesa tu iwapo kweli ungependa kuzifanya ikitokea umekwenda au kama upo huko tayari,
utalazimika kuwa ni mkazi halali na huna historia ya Uhalifu.

HITIMISHO:
Si kuwa ni hizi pekee ndizo Kazi zisizohitaji Elimu ya juu sana kuzifanya na kulipwa vizuri huko Marekani. ama Ulaya zipo nyingine pia na
Tofauti na hizi ili utengeneze Pesa nyingi itakubidi ufanye Kazi masaa mengi zaidi na vilevile kutangatanga maofisi ili kuingiza Pesa zaidi.

Swali:
Kuna Tija gani unapulizwa na Kiyoyozi Ofisini lakini kwa mwaka unaingiza $25k, Ilhali, mwingine yupo Nje ya Kiyoyozi lakini anakunja zaidi pengine marambili ya mshahara wako?

Jibu, KUPANGA NI KUCHAGUA.
Ni Ujinga Mtu akikulaumu wewe kama ilivyo Ujinga kwako pia ikiwa utamlaumu au kumponda anaezifauya hizi kazi.

NAWASILISHA.​
 
Matumizi ya kila siku?
Bei za vyakula?
Huduma kama internet, umeme, maji, gesi n. k
Gharama za maisha bado zipo juu huko kuliko huku kwetu.
Wewe wasema.

Lakini unajua Mshahara wa kima cha chini huko ni kiasi gani au unapuyanga tu ili uonekane kuwa nawe umesema?
 
Sasa si jibu? Ok it's 7.25 $ per hour. Haya turudi kwenye hoja yangu. Tupe minimum gharama za mortgage, gas, umeme, matibabu, insurance, tax, usafiri, msosi, etc.
Bro anajulia wapi haya yote ingali yupo kwa mpalange(kidding) 😅.
Katafuta article online katuletea tafsiri isiyo rasmi.

Kibaya zaidi huwezi kukwepa kodi hizo nnchi za wenzetu.
 
Vipi kuhusu kodi mkuu wanakataje?

Ila najiuliza hawa ndugu zetu wanaorudigi mikono mitupu wao huwa wanakuja kulala au?

Wapi Le Mutuz mzee wa mabebezz
 
Back
Top Bottom