Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 550
- 786
TRA kuweni serious !
Kwenye Mshahara wangu wa mwezi nakatwa kodi na madudu mengine karibu nusu ya Mshahara kabla sijaupokea, nafungua Biashara mnataka Kodi kabla sijaanza,Mwenye Nyumba ya Biashara anataka Kodi kabla sijaingia.
Mwenye Nyumba ya kuishi anataka kodi kabla sijaingia,Manispaa wanataka kodi ya Leseni na Kodi ya Ushuru wa huduma kabla sijaanza Biashara.
Osha wanataka Kodi,Zimamoto Kodi,Wakusanya taka Kodi,Sungusungu Kodi,nk
Manunuzi yoyo te ninayoyafanya hata kama nakunywa soda nalipa Kodi.
Ukigeuka huku kuna Kodi ya Ardhi,jengo,sijui na vitu gani!
Bado Mamlaka zina yake sijui kupima Afya wafanyakazi Kodi,kulipia Leseni za Taaluma Kodi.
Bado Maafisa wa Serikali wanataka Kodi za Familia zao kila wakija kukukagua.
Hizi Kodi zinalipwa vipi jamani!Hata mtu akishindwa au akikwepa analaumiwaje?Ni biashara gani utafanya uweze kulipa utitiri wa kodi zote hizi bila kufilisika?
Serikali haioni tatizo ikaja na Mamlaka na Sheria moja tu ya kukusanya Kodi ukilipa umemaliza vyote?