Kumekuwa na hatari kubwa kwa wanasiasa kulinda maslai yao kuliko ya wananchi

Vallekh

New Member
Jul 14, 2021
2
4
Biashara ya nyumba ni moja kati ya biashara kubwa Duniani, biashara namba tatu duniani kwa faida na wepesi wa kuiendesha ukilinganisha na biashara nyingine hii inahitaji uangalizi mdogo lakini inakupa faida kubwa.

Ongezeko la watu, kupanda kwa thamani ya viwanja, kupanda kwa mali gafi za ujenzi, kukua kwa uchumi na maendeleo ya miji ni miongoni mwa sababu zinazopelekea kukua kwa biashara hii kwa kasi.

Hata hivyo biashara hii imekuwa na changamoto nyingi katika kuendesha kama ifuatayo:-
Kukosekana kwa sera ya biashara ya nyumba Tanzania.

Ukosefu elimu ya biashara kwa wamiliki.

Majanga ya moto.

Mfumo mbovu wa bei.

Kutotambuliwa na mamlaka za biashara.

Mchango mdogo katika pato la taifa.

Pamoja na faida nyingi zinazopatikana kwenye biashara hii lakini bado Serikali imekuwa ikivuta kuifanya biashara hii kuwa rasmi na hii itahusisha mambo yafuatayo:

Kuirasimisha biashara hii katika mifumo ya kodi. Kwamba, ubunifu katika nchi masikini haupo lakini utakuwa na tija kama ubunifu huo utakuwa haugusi maslai ya watunga sera;

Katika mtaa mmoja niliona kituko cha mwaka pale mamlaka za kodi zilimfungia mmiliki wa duka lenye thamani ya milioni moja kwa kosa la kuchelewa kulipa kodi wakati huohuo mmiliki wa vyumba vya biashara anayemiliki vyumba hivyo na ayechukua hela ya pango kwa Mwezi laki tatu kwa Mwezi kumfanya kukusanya kwa Mwezi milioni tatu na laki sita kwa vyumba vyake 12, akiachwa bila kusumbuliwa kuhusu kulipa kodi kana kwamba yeye hafanyi biashara.

Biashara ya nyumba ni biashara kama biashara nyingine na inapaswa kulipiwa kodi lakini mpaka sasa hakuna anayeliona hili.

Mamlaka za kodi zinafukuzana Na wafanyabishara wadogo wenye mitaji ya laki tano huku wafanya biashara wa nyumba ambao wanaingiza mamilioni kwa Mwezi wakiachwa kuwa huru kana kamba wanafanya ya kanisa.

Rashid alifungiwa Duka lake la chakula mpaka alipe kodi wakati huo huo mmiliki wa vyumba kumi vya biashara ambavyo Rashid alikuwa anamlipa kodi akufuata hata kuulizwa kama amewai kulipa kodi.

Katika moja ya mazungumzo ya kijiweni huko Mbagala, mmoja wa walimu wastaafu alitetea hoja ya nyumba kutolipiwa kodi. Alisema:

Nyumba za biashara zinamilikiwa na wastaafu kama sehemu ya viunua mgongo ndio maana serikali hazitozi kodi biashara hii, nilimhoji kama ndio Je mstaafu akifungua biashara ya Duka la dawa hapaswi kulipa kodi?

Utoawaji wa leseni za biashara nyumba kama ilivyo biashara nyingine. Ingawa biashara yoyote lazima iwe na utambulisho wa serikali na hivyo zinapaswa kukatiwa leseni kulingana na biashara husika, hata biashara ya nyumba haina leseni wala haitaji kuifanya kuwa na leseni.

Serikali haikuwai kutoa sababu kwanini wamiliki wa biashara ya nyumba hawapaswi kuwa na leseni.

Kuweka utaratibu wa uendeshaji. Changamoto nyingine biashara kukosa utaratibu kabisa kila mmiliki ana utaratibu wake ni kama tupo baharini kila mmiliki anaongelea na mtindo wake na serikali imebaki inaangalia tu.

Kuna mambo ya ajabu Tanzania hata hatujui lini yataisha kwamba wamiliki wengi wanapenda kulipwa kodi kwa mwaka mzima na wengine kwa miezi mitatu na hili imekuwa ikiwaumiza sana wateja na wananchi wa Tanzania.

Kwamba, kama hakuna mtu anayelipwa mshahara kwa mwaka mzima au miezi mitatu au miezi sita itawezekana vipi mtu huyo kulipa kodi ya nyumba kwa mwaka mzima? Au miezi sita? Au miezi mitatu?

Watu kulazimishwa kulipa kodi kwa miezi sita au mwaka ni ukatili mkubwa sana kwa wateja na moja ya kusababisha watanzania wengi kuwa:

Kuwa Masikini
Kushindwa kujaribu
Kunyanyasika
Kujiingiza kwenye matendo ya kuomba rushwa, ufisadi na ualifu kwa lengo la kutafuta kodi ya mwaka au miezi sita au mitatu.

Mpaka sasa haijulikani utaratibu wa watu kulipia kodi kwa mwaka mzima umetoka wapi maana hata katika nchi zilioendelea haupo, nimeona utaratibu wa kulipia kwa mwaka haupo.

Katika biashara hali imekuwa mbaya zaidi, watu wengi wamekuwa wakishindwa kufanya biashara si kuwa wamekosa mtaji bali kwasababu ya kukosa kodi ya mwaka au miezi sita.

Kwa mfano Kariakoo ambako ndio kitovu cha biashara Tanzania, wafanya biashara wanalazimishwa kulipia kodi kwa mwaka mzima.

Hela ya pango inaanzia 600,000-1,000,000 kulingana na eneo au mtaa lakini mbaya zaidi wamiliki wanataka kodi ya mwaka mzima hivyo mtu analazimika kuwa na kodi ya mwaka mzima kuanzia 7,200,000-12,000,000 na hili hii imefanya wengi kuingia kwenye umasikini mkubwa pale biashara inapokuwa ngumu na mbaya zaidi wengi kujiingiza kwenye mikopo.

Kama serikali inataka kuwasaidia wananchi wake ina budi kuingilia utaratibu huu wa kulipa kodi sababu unawafanya wamiliki kuishi maisha kama Miungu na watu ambao hawajui hasara.

Kama utaratibu wa watu kulipia kodi kwa Mwezi utafanikiwa utasaidia sana kama ifuatavyo:-
Uchumi wa mtu mmoja moja kuongezeka na kukua.

Utawafanya watu wengi kuingia kwenye biashara na hivyo kodi ya serikali itaongezeka. Utaokoa hasara zisizo za lazima kwa wafanya biashara Utaongeza ushindani wa soko la nyumba na kukua kwa biashara ya nyumba.

Mwisho tumefika hapa kwasababu wanasiasa wengi wamekuwa wakifanya biashara za umiliki wa nyumba au kuwekeza kwenye biashara hii ndio maana kunakosekana kwa mwamko wa ndani kutetea jambo hili katika vikao vya kila siku vya bunge.

Kumekuwa na hatari kubwa kwa wanasiasa kulinda maslai yao kuliko ya wananchi na hivyo kupeleka changamoto nyingi za wananchi masikini kushindwa kutatuliwa au hata zinapotatuliwa basi kwa namna ya kulinda maslai ya hao wanaozitatua.
 
Biashara ya nyumba ya kupanga kwa nchi yetu Haina faida kiivyo Kama unavyofikiria,

Kiuhalisia,
Soko la nyumba limeshuka Sana miaka hii.

Kinachoingia ni kidg mno kulinganisha na uwekezaji mkubwa uliofanyika.
 
By the way,
Mtoa mada acha upotoshaji.

Kwa Sasa wamiliki wote wa nyumba wanalipa Kodi kwa mujibu wa sheria kupitia makato ya luku.

Vinginevyo utwambie unaishi Kwenye nyumba ya giza
 
Unachopaswa utambue mtoa mada,
Endapo serikali itanzisha utaratibu wa Kodi Kama unavotaka.

Atakaeumia Ni mpangaji na sio mwenye nyumba,

Atakachokifanya yeye mwenye nyumba Ni kuongeza TU Bei ya pango kufidia Kodi ya serikali, KAMA UTAKI HAMA.

Kwasababu,
Kwenye nyumba za kupangisha Hakuna mambo ya Bei elekezi, ni maelewano yenu.

Na ukishindwana na mwenye nyumba, serikali haiwezi kuingilia.
 
Back
Top Bottom