Hizi hapa sababu wanawake kukimbilia mikopo ‘kausha damu’

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,227
5,950
Serikali imetaja sababu za wanawake kukimbilia mikopo yenye masharti magumu, ikiwamo wengi kuwa na elimu ndogo ya fedha.

Tatizo hilo lilielezwa ni chanzo cha wanawake kujiingiza katika mikopo hiyo maarufu kwa majina kama vile ‘ kausha damu’ na ‘mikopo umiza’.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa alisema jana kuwa wanawake wanaumizwa na mikopo umiza kwa sababu hawana elimu ya fedha.

Alitoa kauli hiyo wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo ambayo hadi sasa imewezesha mikopo ya Sh9.1 trilioni kwa watu 8.6 milioni.

Being’i alisema mbali na wanawake wanaotajwa kujiunga na mikopo umiza, kwa ujumla wake elimu ya fedha kwa Watanzania wengi imekuwa ni tatizo.

“Wanawake wengi wamejiunga na mikopo umiza ambayo haina tija kwao hata kidogo, hili siyo jambo zuri kwani inahatarisha maisha yao na familia kusambaratika. Tunawataka wasikurupuke kutaka vitu kwa haraka na watambue hakuna anayeweza kupewa fedha kama hana shughuli ya kufanya,” alisema Beingi.

Akizungumzia suala la uwekezaji, alisema sera ya ubinafsishaji haikufanya vizuri kwa wakati ule na mpaka sasa haipo kama ilivyokusudiwa, ndiyo maana wamekuja kwa namna nyingine.

Mtendaji huyo alisema kazi kubwa waliyonao ni kuona namna gwanavyoweza kuwasaidia wajasiriliamali 3.5 milioni ili waweze kufanya vizuri na kukuza mitaji yao.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, kuna mifuko 72 ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ambapo 10 ni ya binafsi, huku i 72 ikiwa ni ya Serikali ambayo imesaidia pia kutoa ajira 17.6 milioni.

Kasi ya matapeli
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Gerson Msigwa aliwataka Watanzania kuongeza umakini katika matumizi ya fedha hasa kwenye suala la mikopo kwani matapeli wameongezeka.

Msigwa alisema wengi wamekuwa wakidanganywa, kwa sababu ya kutaka mikopo ya haraka isiyokuwa na masharti, lakini wanasahau kwenye malipo wanakutana na kilio.

Alitaka kuwapo kwa tahadhari kubwa kwa wakopaji, kwani utapeli umekuwa ni mkubwa hasa kupitia mitandao ya kijamii.

Mwandishi wa habari Carlos Ngonyani alisema mikopo umiza imeshawaliza watu na kusababisha ndoa kuvunjika, kwa sababu wengi huenda kuchukuliwa vitu vyao kwa kushindwa kurejesha.
 
Back
Top Bottom