Hizi biashara za vyakula hazisambazi covid-19 kweli?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,823
35,829
Moja kwa moja kwenye mada.

Kuna hizi biashara za vyakula mfano: miwa iliyo menywa, mahindi ya kuchomwa, nk. Hivi hushikwa shikwa na watayarishaji hasa kwa miwa. Mahindi ya kuchomwa hushikwa shikwa hata na wateja kujiridhisha ugumu au ulaini wake.

Sahani za vyakula, nyuma (uma), vijiko, vikombe vya maji, chai, kahawa, nk, vitumikavyo mahotelini, migahawani, kwa mama ntilie, majiani nk. Usafi wa vifaa hivi katika maeneo haya ni wa viwango vya chini mno.

Hata hivyo hakuna tahadhari yoyote imekuwapo kuangazia kuhusiana na haya kama maeneo yenye hatari ya uwezekano wa kusababisha maambukizi.

Watu wanachapa kazi kwa raha zao.

Tuelimishane jamani hakuna uwezekano wa maambukizi katika maeneo haya? Biashara hizi katika maeneo mengi zinaendelea pasipokuwa na neno lolote la tahadhari.

Wizara ya afya na wadau wengine hili limekaa je?
 
wanasayansi wamesema ni ngumu

Sent using Jamii Forums mobile app

Ngumu kwa vipi? Virusi mgonjwa anakuwa navyo kiganjani na mdomoni. Vikombe, vijiko na umma uoshwaji wake unaujua.

Miwa na mahindi ya kuchomwa yanashikwa shikwa yakiwa baridi na watu tofauti tofauti.

Inafikirisha!

Wataalamu wapi wanaosema ni ngumu? Hawa hawa wa kupiga nyungu?
 
Mahindi vigumu Sana,maana unanunua mhindi wa Moto Sana,,
Kwa mama ntilie ndio inabidi tuongeze maombi,,
Bakery inahitaji uangalizi pia,hasa kipindi Cha kuiweka mikate kunako mfuko,,wanaishika kwa mikono,vizuri kyipitisha katika microwave kabla ya kuitumia au isitumike mpaka baada ya masaa 48,kwa maoni yangu
 
Mkuu si mahindi yote ni ya moto. Unakuta mahindi yashapoa mno na wateja wanashika shika kuangalia yapi lakini. Mtu anaweza shika shika hata 10 asikuchukue hata moja au aishie kuchukua moja.

Hujaziona hali hizo mkuu?

Mengine unakuta yanatembezwa madirishani kwenye mabasi yanayo safiri. Yameshapoa vilivyo. Wasafiri wanashika shika. Muda haupo hata wa kuchagua. Wanaishia kuchukua yoyote yanayo patikana na kula.

Hapo hapo vipi? Pako salama?
 
Mie haya mahindi ya kuchoma wanayouza kwenye magari hata kabla ya corona nilikuwa sinunui. Emagine mtu na mikono yake haujui ameshika nini na wapi anayashika shika wala hanunui wewe unakuja kuununua unakula tuu. Muhindi mmoja unashikwa za zaidi ya abiria kumi wa kumi na moja ndie ananunua.
Hii ni hatari sana
 
Ni jambo la kushangaza serikali inajua kuwa haya yanatokea watu wanaambukizwa nao wako kimya.

Hata hizi utensils uma, vijiko, vikombe nk havioshwi sawa sawa. Alipoweka mdomo mwingine kunywa maji au chai na mwingine anaweka hapo hapo.

Serikali wameamua kweli kuwatoa watu kafara.

Pana hata haja gani ya ma sanitizer mikononi kwa hali kama hizi ambazo nyanga inapelekwa moja kwa mdomoni bila hata kuguswa na viganja?
 
Moja kwa moja kwenye mada.

Kuna hizi biashara za vyakula mfano: miwa iliyo menywa, mahindi ya kuchomwa, nk. Hivi hushikwa shikwa na watayarishaji hasa kwa miwa. Mahindi ya kuchomwa hushikwa shikwa hata na wateja kujiridhisha ugumu au ulaini wake.

Sahani za vyakula, nyuma (uma), vijiko, vikombe vya maji, chai, kahawa, nk, vitumikavyo mahotelini, migahawani, kwa mama ntilie, majiani nk. Usafi wa vifaa hivi katika maeneo haya ni wa viwango vya chini mno.

Hata hivyo hakuna tahadhari yoyote imekuwapo kuangazia kuhusiana na haya kama maeneo yenye hatari ya uwezekano wa kusababisha maambukizi.

Watu wanachapa kazi kwa raha zao.

Tuelimishane jamani hakuna uwezekano wa maambukizi katika maeneo haya? Biashara hizi katika maeneo mengi zinaendelea pasipokuwa na neno lolote la tahadhari.

Wizara ya afya na wadau wengine hili limekaa je?
Inashangaza kama hizo biashara bado zinaendelea hapo bongo, aisee taifa linacheza na corona, watu watakwisha kama ni hivyo.
 
Ni jambo la kushangaza serikali inajua kuwa haya yanatokea watu wanaambukizwa nao wako kimya.

Hata hizi utensils uma, vijiko, vikombe nk havioshwi sawa sawa. Alipoweka mdomo mwingine kunywa maji au chai na mwingine anaweka hapo hapo.

Serikali wameamua kweli kuwatoa watu kafara.

Pana hata haja gani ya ma sanitizer mikononi kwa hali kama hizi ambazo nyanga inapelekwa moja kwa mdomoni bila hata kuguswa na viganja?
Uchaguzi mkuu huu wamekuja na njia ya kijanja kutoa kafara.Na hata huo uchaguzi unaweza usiwepo mwaka huu.
 
Back
Top Bottom