Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,320
Nimekutana na threads kadhaa ambazo wadau wanalalamika kuwa wamegundua kuwa walio nao wana wapenzi wengine hivyo wanaomba ushauri. Nimeona niianzishie thread kabisa, ili lijadiliwe upya.
Kwa wanaume,
Mwanamke mzuri unayemuona leo, ameshaonwa na wanaume wenzio kibao kabla yako. Unapomtongoza leo, keshatongozwa na wanaume kibao kabla yako. Na usishangae anapokukubalia leo, keshawakubalia wengine kabla yako. Hivyo sio kitu cha ajabu, kukuta kuwa demu wako alikuwa na mtu/watu wengine na pengine bado wanawasiliana.
Kwa taarifa yenu wanaume wenzangu ni kuwa asilimia kubwa ya wasichana wazuri siku hizi wana wapenzi mmoja au zaidi waukwel, na wengine kadhaa kwenye reserve list. Wanaume wengi waliowapata wanawake wazuri, hata kuwaoa, waliwazidi nguvu wanaume wengine waliokuwa wanataka hiyo nafasi. Hivyo itakuwa ni ujinga usio na maana eti unapolalamika kuwa nimegundua mpenzi wangu anawasiliana na x wake, au ana mpenzi mwingine.
Wasichana wengi wazuri hupunguza idadi ya wapenzi wa kwel au wa reserve list, pale mmoja wapo anapobahatika ku upgrade mahusiano kwenda level ya uchumba, na huwamaliza kabisa wanapoingia kwenye ndoa, japo kuna wengine wanakosa adabu na kuendelea na ma x hadi wakiwa kwenye ndoa.
Hivyo wewe uliye na demu mzuri kwa sasa, usivimbe kichwa na vijimamaneno unavyoambiwa 'upo peke yako' au 'bila wewe siwezi ishi'. Kwa taarifa yako mpo kadhaa, na wewe unapewa heshima unayopewa kwa sababu tu ya juhudi zako za kuonyesha upendo. Siku ukiharibu tu mwenzio anachukua nafasi fasta.
Na kwenu wanaume mnaojijua kuwa mnamendea demu mwenye mpenzi, msikate tamaa. Endeleeni kupiga jaramba hapo nje, kwani wakati wowote yakifurumuka humo ndani unawezajikuta unaambiwa vaa jezi, ingia, then unapata nafasi ya kuonyesha kiwango chako, na namba unaimiliki moja kwa moja.