Hivi wana JamiiForums mliandamana huko mitaani kweli?

Nimejiuliza sana hili kwa sababu mpaka muda huu naona kila mmoja wetu yupo active na cha kushangaza hatuna kifo hata kimoja.

Kiufupi hili jukwaa ndio jukwaa pekee ambalo halijakumbwa na msiba kama majukwaa mengine kuanzia tik tok mpaka facebook.

Hivi mlitoka au mlikuwa mmejificha majumbani au mlimbikilia vijijini! Mi binafsi nlitoka ila ni ile 29 na 30 hizo siku nyingine nlijificha baada ya kugundua kuna masnipers washenzi sana.

Niwapongeza members wote mlioandamana na hamkufikwa na maafa, mitandao mengine inapaswa kujifunza kwetu.

TUSISAHAU TAREHE 9/12/2025 TUNATOKA TENA AWAMU HII LAZIMA KIELEWEKE.
Hili swali lako halistahili kujibiwa,kwani ulitaka utuone hatuna ubongo ndio ujue au?
 
Vifo vingi havijawahusu waandamanaji bali waliokiuka amri ya kutotoka nje na waliofuatwa tu majumbani!
 
Halafu ile Jf imefungwa na mitandao imezimwa kuna maninja walikua wanaendelea kutema nyongo humu maana meseji zenu nimeziona sana.
 
Nimejiuliza sana hili kwa sababu mpaka muda huu naona kila mmoja wetu yupo active na cha kushangaza hatuna kifo hata kimoja.

Kiufupi hili jukwaa ndio jukwaa pekee ambalo halijakumbwa na msiba kama majukwaa mengine kuanzia tik tok mpaka facebook.

Hivi mlitoka au mlikuwa mmejificha majumbani au mlimbikilia vijijini! Mi binafsi nlitoka ila ni ile 29 na 30 hizo siku nyingine nlijificha baada ya kugundua kuna masnipers washenzi sana.

Niwapongeza members wote mlioandamana na hamkufikwa na maafa, mitandao mengine inapaswa kujifunza kwetu.

TUSISAHAU TAREHE 9/12/2025 TUNATOKA TENA AWAMU HII LAZIMA KIELEWEKE.
Humu kumejaa KEYBOARD WARRIORS tu, hakuna mtu wa kuandamana

Mimi nilitoka nikachukua matukio live, nili nusurika kukamatwa nikajificha mpaka tarehe 8 ndio nikawa huru nilikuwa natafutwa na mtu ninayemfahamu bila sababu za msingi kumbe snitch.
Nasikitika mrangi sijamuona jukwaani tangu apost picha ya maandamano, na hofia aliuwawa.
Chai.

Mrangi hajaonekana humu tangu jf ifungiwe 6 September
 
Back
Top Bottom