Hivi wana JamiiForums mliandamana huko mitaani kweli?

Hivi wana JamiiForums mliandamana huko mitaani kweli?

Mimi nilikuwa magetoni nafuatilia live kama nilivyoahidi mpaka walipozima intaneti
1000072980.jpg
 
Kama kwetu
Hapakuwa na heka heka ile j5 mchana…
Ilaa usiku wake zilipigwa za kujeruhi na kuua.. zilisababisha nikae ndani kuanzia huo usiku mpaka j4 waliposema sasa kazi ziendelee 🥲

Bora lockdown ya korona, hii inatisha sana
tujiandae tu kisaikolojia....

kuna watu hawakuwa na mpango ila walipoona polisi wanataka kuingia ndani ikabidi watoke mlango wa nyuma wakajichanganye
 
Mimi nilitoka nikachukua matukio live, nili nusurika kukamatwa nikajificha mpaka tarehe 8 ndio nikawa huru nilikuwa natafutwa na mtu ninayemfahamu bila sababu za msingi kumbe snitch.
Nasikitika mrangi sijamuona jukwaani tangu apost picha ya maandamano, na hofia aliuwawa.

dah umenishtua sana, mwamba ni very senior humu jukwaani. ila mbona inaomekanwa hakapost kitu tuko September mwanzoni?
 
Tarehe 29, huku nnapokaa palikua na utulivu mpaka mchana, kuna demu nlimuita akaja home, lengo ilikua saa 12 jioni arudi kwao, sasa cha ajabu ilivofika saa kumi jioni tukaanza kuskia milio ya risasi, kumbe ndo kulikua kushachangamka mbaya, ikabidi mtoto wa watu alale tuu home, kesho yake yani tarehe 30, nlimtoa kwa tahadhari sana, nashukuru Mungu alifika kwao salama, uzuri mimi na yeye hatukai mbali sana ni umbali wa sh 1000 kwa boda
 
dah umenishtua sana, mwamba ni very senior humu jukwaani. ila mbona inaomekanwa hakapost kitu tuko September mwanzoni?
Nilianza kutafutwa na mtu ninayemfahamu bila sababu za msingi nikahisi ni mtego, maana alianza kuniambia nimekuona sehemu fulani ghafla umepotea uko wapi? Nikamuuliza yeye yuko wapi na kwanini ananitafuta hakunijibu, baadaye ananiuliza niko wapi aje nilipo?
Nikamuuliza kuna issue gani? Hakunijibu nikakata simu nikatoa sim card nikaanza kupotea.
Nikapigiwa simu nyumbani kwamba kuna mgeni ananitafuta nikapotea jumla.
 
Nimejiuliza sana hili kwa sababu mpaka muda huu naona kila mmoja wetu yupo active na cha kushangaza hatuna kifo hata kimoja.

Kiufupi hili jukwaa ndio jukwaa pekee ambalo halijakumbwa na msiba kama majukwaa mengine kuanzia tik tok mpaka facebook.

Hivi mlitoka au mlikuwa mmejificha majumbani au mlimbikilia vijijini! Mi binafsi nlitoka ila ni ile 29 na 30 hizo siku nyingine nlijificha baada ya kugundua kuna masnipers washenzi sana.

Niwapongeza members wote mlioandamana na hamkufikwa na maafa, mitandao mengine inapaswa kujifunza kwetu.

TUSISAHAU TAREHE 9/12/2025 TUNATOKA TENA AWAMU HII LAZIMA KIELEWEKE.

Wapo walioandamana na hawakufariki na pia wapo ambao hawakuandamana na wamefariki wakiwa ndani au wakiwa wanarudi/enda kwenye shughuli zao na wakapigwa risasi na MAGAIDI WA ABDUL.
 
Back
Top Bottom