Duniani kila mwenye Uhai ana maisha yake...tunaita Race, Mimi ni msukuma ila nimeishi umaisaini na nimewahi kudate Mmsai, nawafahamu nje ndani. Originally, wamasai sio watu wa kukaa sehemu moja; yaani kujenga, na kuwa na modern life wewe unayoikubali na kuiishi. Utamaduni wao ni kuhama hama kufuata marisho ya mifugo yao. Asili yao ni Juba huko South Sudan, manmo mwaka 1600 walianza kutembea na ng'ombe zao kuja East Africa nyanda za juu. Wamasai tunaowaona mjini ni wale optimisitic hivyo wameamua kujichanganya na modern life...so wamekuja mjini kuhustle, wanajaribu ku-blend in lakini wapi...ndio maana wanaishia kufanya kazi yao iliyoko iliyoko damuni, ULINZI. (walipaswa wawe maporini wakilinda mifugo yao).
Kitu nilichokipenda zaidi kwao, hawana wivu (wa maendeleo na usio wa maendeleo)...wewe ata ujenge, ununue gari, usomeshe wanao, yeye atakupongeza tu in case ukianza kuzungumzia hayo mambo yako na ataku appreciate, mkiachana hana time kabisaa, anaendelea na mambo yake na habari zako sio nzito, atakuwa kawaida tu.
Masai akikuchukia...utakuwa unamtesa sana, ni vyema ukajiongeza mzungumze yaishe otherwise atabaki na sononeko, uchungu na ghadhabu lakini hatothubutu kutafuta solution hata ya kukudhuru kwasababu ya aibu ya utu.
Kazi zao ni za kisanaa; kuchonga vinyago, kutengeneza urembo, n.k....pia kila kiazazi huja na design zake. Huenda trend ya draft na rangi nyekundu ikapotezewa kizazi kijacho.