Duniani kila mwenye Uhai ana maisha yake...tunaita Race, Mimi ni msukuma ila nimeishi umaisaini na nimewahi kudate Mmsai, nawafahamu nje ndani. Originally, wamasai sio watu wa kukaa sehemu moja; yaani kujenga, na kuwa na modern life wewe unayoikubali na kuiishi. Utamaduni wao ni kuhama hama kufuata marisho ya mifugo yao. Asili yao ni Juba huko South Sudan, manmo mwaka 1600 walianza kutembea na ng'ombe zao kuja East Africa nyanda za juu. Wamasai tunaowaona mjini ni wale optimisitic hivyo wameamua kujichanganya na modern life...so wamekuja mjini kuhustle, wanajaribu ku-blend in lakini wapi...ndio maana wanaishia kufanya kazi yao iliyoko iliyoko damuni, ULINZI. (walipaswa wawe maporini wakilinda mifugo yao).
Kitu nilichokipenda zaidi kwao, hawana wivu (wa maendeleo na usio wa maendeleo)...wewe ata ujenge, ununue gari, usomeshe wanao, yeye atakupongeza tu in case ukianza kuzungumzia hayo mambo yako na ataku appreciate, mkiachana hana time kabisaa, anaendelea na mambo yake na habari zako sio nzito, atakuwa kawaida tu.
Masai akikuchukia...utakuwa unamtesa sana, ni vyema ukajiongeza mzungumze yaishe otherwise atabaki na sononeko, uchungu na ghadhabu lakini hatothubutu kutafuta solution hata ya kukudhuru kwasababu ya aibu ya utu.
Kazi zao ni za kisanaa; kuchonga vinyago, kutengeneza urembo, n.k....pia kila kiazazi huja na design zake. Huenda trend ya draft na rangi nyekundu ikapotezewa kizazi kijacho.
Kwa updande wa Arusha, Manyara na mikoa ya kitalii, wamasai wenye akili wamepata fursa...kwanza ni kivutio cha kitalii..pia wawekezaji wanaanzisha nao Projects za kijamii...halafu kuna hii aina ya Lodge inaanza kutrend inakwenda kutikisa bunglow hotels na lodge za kifahari za nyota 5 zilizoko huko maporini...trend hii Maasai Lodges, yaani sasa; nyumba zao (za udongo na manyasi) zinageuzwa Lodge/Hotel
SO unaweza kuja huku ukaongea na Raigwanan mwenye boma, kisha home yake ukaifanya Hotel na kupiga pesa na kutoa ajira...hamna gharama, ujenzi ni wao wenyenye, wanajenga kwa tamaduni zao...mbao wanaingia tu porini wanakata...furniture ni local,,,,wewe utaingia gharama ya kununua Solar, vyoo na masiki.
Nje ni kma banda la mganga, ndani pakoo furnished lakini kimasai...mfano kitanda, miti au meza ni mtiti wnaakata na kupigilia misumari tayari meza!! hamna mbwembwe...kitanda kinawekewa godoro la 6x6 lakini cha miti, vitambaa vyote ni vya kimasai.....bei yake sasa!!!! DOla 290 peer night.
Nipo huku ndo naondoka kesho kuja Dar. Nimeambaanisha picha za huku na za chumbani...najihisi nipo kwa mganga, akili imekataa kukubali kwamba nipo utalii likizo kwenye mjengo wa bei. Ila msosi ni wa nyota 5 si kitoto. NOTE: nimekuja kuwafanyia kazi ya kiteknolojia kwa wiki 1 so Lodge ndo imenileta, sina hela ya kulala maporini.