Hivi walokole hamuwezi kuabudu kimya kimya!??

Hivi walokole hamuwezi kuabudu kimya kimya!??

Hapo ni sawa na kuwaambia waislamu wasitumie zile horn speaker kwenye misikiti. Ngumu sana hao watu kukuelewa kwa hilo.
Kuna mtaa nilihamia kipindi nipo chuo, asee ilikua ni kero sana. Yaani asbh sana, unaskia kipaza sauti....
 
Duuuh....Mimi imenibidi nizoeee tu...ikifika sakumi wanaaza kuimba KILA siku...masoezi ya kwaya...
Ikifika ijumaa satatu mkesha.wanaimba mpaka sasita usiku..
Jumapili.kwanzia sanne Ni ibada wataimba na kuomba Hadi sa sa Saba mchanaa....alafu wataanza tena sakumi jioni...

Nyimbo zao nimezikariri ....nazijua vizuri tu....tumelalamika tumeona tukubali Hali.
Nunua mziki Mkubwa kuwazidi halafu ikifika muda Wa kero weka diamond kwa sauti Kubwa. Mbona hawataelewana wataomba poo. Omba kistaarabu usikere wengine ni dhambi. Dawa ya moto ni moto. La sivyo utaharibiwa masikio bure.
 
Hii ni shida Sana inaendelea hapa mtaani

Watu hatulali Hawa walokole wa kanisa la hapa mtaani mida hii wanaungurumisha music na kuimba kwa kelele Sana

Nashindwa kuelewa kwa nini serikali isipige Marufuku mtindo huu wa kuabudu kwa kupiga muziki tena wa juu Sana Hali inayopelekea noise pollution kwa wakazi husika.

Mida ya usiku ni muda wa kupumzisha akili na kunakuwa na utulivu wa Hali ya juu,sasa Hawa walokole wanapoanza kupiga miziki yao inakua kero kwa watu wa maeneo ya jirani.

Niambie wapi naweza kwenda kutoa mashtaka dhidi ya hili kanisa manake ni kero sasa kwa hii style yao ya kuabudu ni kelele mtaa mzima.
Serikali haina dini, Watu wake ndio wana dini. Hiyo kesi ngumu,je waislamu na RC na AIC.....
 
Nunua mziki Mkubwa kuwazidi halafu ikifika muda Wa kero weka diamond kwa sauti Kubwa. Mbona hawataelewana wataomba poo. Omba kistaarabu usikere wengine ni dhambi. Dawa ya moto ni moto. La sivyo utaharibiwa masikio bure.
Siwezi wakera watu namna hiyo
 
Hapo ni sawa na kuwaambia waislamu wasitumie zile horn speaker kwenye misikiti. Ngumu sana hao watu kukuelewa kwa hilo.
Bora muslims yao ni short...walokolee siku nzima na usiku pia inakera
 
Pambana na hali yako.
Watu hawawezi acha kumuabudu Mungu kwa sababu za kijinga namna hiyo


Hata Mimi asubuhi Sina ratiba ya kuwahi saa 11 Ila huwa naamshwa na kelele za Allah Akbar zinapenya kwenye ngoma za masikio yangu hadi nahisi yanatoboka..lakini sijawahi kasirika kwa sababu naheshimu ratiba na imani za watu .
Hizo kelele nazisikia kutwa Mara 5.

Kelele za Bar usiku kucha ni vurugu hamisikii,ila mmekazana na watu wanaosali.
Nyie mna mapepo.
 
Kunya anye kuku akinya Bata kaharisha,

Ile azana ya saa 11 mnasema inawaamsha kama alarm vile ila hii ya walokole inawasumbua.
Azana inapigwa si zaidi ya dakika 5 tena kwa sauti ya kawaida,
Azana inapigwa saa 11 alfajiri ambapo takribani asilimia kubwa ya watu washaamka wanajiaanda kwenda kwenye shughuli,
Haya makanisa ya walokole wanafungulia miziki tena ile ya kupiga bend usiku kucha,
Tukatae tukubali kunae muda inabidi ukweli usemwe...
 
Siwezi wakera watu namna hiyo
Huwakeri unawafundisha hekima. Hekima inasema muubudu na umtumikie kwa namna ambayo utawapa Na wengine wivu. Ukumbuke wivu Wa Bwana Wa Majeshi. Huwezi kuvutia wengine wamjue Mungu wako kwa kugeuka kero mtaani. Watu watamdharau Mungu wako.
 
Hivi ukisali kwa kupiga kelele na mayowe ndiyo Mungu anasikia sala zako? Yesu mwenyewe alipotaka kuzungumza na Mungu alijitenga kwenye sehemu ya ukimya.Huu upuuzi huwezi ukuta ndani ya kanisa katoliki.
 
Nakumbuka Siku moja usiku tukiwa tunafanya mazoezi ya muziki,
Alikuja mchungaji atuambia mazoezi mwisho saa tatu na tutumie spika za monita ili tusiwasumbue majirani,
Sio lazima sauti iwe kubwa ndio Mungu asikie sifa na maombi, mana hiyo sauti kubwa inawaumiza hata waumini wenu.
 
Back
Top Bottom