Hivi walimu ni wajinga au wapumbavu?

Hivi walimu ni wajinga au wapumbavu?

Shida ninayoiona hapa ni nchi kuwa na maraisi waliowahi kuwa walimu hao ndio wanawamaliza walimu wenzao katika maslahi yao! Kuna msemo wa kiswahiki unaosema KIKULACHO KI NGUONI MWAKO,walimu tafakarini mchukue hatua October.
 
Suala la makato cwt liliwahi kujadiliwa bungeni na maelezo yaliyotolewa ni kwamba ili uwe mwanachama unapaswa ujaze form.kwa wasio wanachama watakatwa 2%ya mishahara yao kama ada ya uwakala.

Wanadai ndio wanaopigania haki za walimu kama mishahara ,malimbikizo,na madeni mengine.hata hivyo hakuna wanachofanya zaidi ya kuwaibia walimu. Nashangaa kama utetezi unafanyika kwa% !Kuna chama kipya kimeshaanzishwa kimesajiliwa kwa ajili ya walimu achaneni na cwt.

CWT ni mkono wa chama fulani cha siasa. Angalia aliyekuwa mkuu kabla ya akina Mkoba, yule mama aliteuliwa kuwa waziri tena wa elimu,naona ilikuwa shukrani kwa kukitumikia chama hicho vizuri ndani ya cwt.
 
Walimu sio wajinga wala wapumbavu bali wewe mleta mada ndiye. Kila utaalamu ukiwemo walimu ni lazima uwe na professional trade union yake na hilo halikwepeki. Tatizo lako hujui kuwa kuna mambo yako nje ya uwezo wa trade unions,mambo hayo yanahitaji political will of the goverment in power na economic ability of a given country najua wewe unahitaji maslahi kwa walimu.

CWT kama chama kinafanya kazi nzuri sana ya kuwasaidia wanachama wake,mfano kinasaidia mwalimu anapopata msiba kinatoa rambirambi,mwalimu anapostaafu kinatoa zawadi na mwalimu anapopata shida ya dharura kinampa cash money isiyorudishwa na zaidi kinarudisha asilimia ya makato kila mwaka kwa mwalimu mwenyewe in terms of cash huku kikipambana na serekali iongeze maslahi ya walimu sasa wewe ungetakaje? Walimu si wajinga ni werevu.
 
Mtoa mada kauliza ni wajinga au wapumbafu. Hajasema eti walimu ni wajinga na wapumbafu pia, by the way, kwa hali/tabia wanayoionesha walimu ktk kurespond ujinga wanaotendewa hata mi nashindwa kuwaelewa hawa walimu, yani utadhani wanavielement vya wabunge wa ccm wakibisha kidogo mwishowe wanakubali hawana msimamo hawa,waache waonewe tu maana hakuna namna ya kuwasaidia kama wao hawana msimamo ktk kutetea maslahi yao
 
Mkuu, umeongea jambo la msingi sana. Walimu wa nchi hii ni wajinga hata kuliko wakulima ambao hawakuwahi kwenda shule. Hili ndilo linalodhirisha kwamba mtu mwenye elimu nusu ni afadhali kuliko mtu asiyekwenda shule.
 
Wameonewa nn lete suluisho, mnafikiri hilo jitu jingine linalokuja halitakuwa na makato heeee? Baada ya kuona mnataka kuazisha bank sirikali imeona mtakuwa na nguvu sasa inataka kuwagawa ili mnyonywe vizuri, mkiua cwt mjue mmekwisha, sirikali haitaki trade union yenye nguvu kama yenu.
 
Dorogo

Umeongea vizuri mwerevu ila wapumbavu kama mie huoenda kuona japo vi data viwili vitatu ili kuona uhalisia kwa picha. . . .

1. Mtu akishaanza kutaja political will ni sawa na kisema majaaliwa ya Mungu. . . . Una hoja gani juu ya hili?!!
2. Economic ability sawa. . . . .Je hiyo ability kwa projection yako/yenu itakuwa tayati baada ya muda gani kuweza kuhudumia hao wahitaji??!!!
3. Rambirambi, zawadi na dharura havihitaji chama na michango ya kila mwezi huku mitaani wapumbavu sie tunazika, tunapeana zawadi, na.tunauguzana na hatuna chama wala jengo. . . . .Hebu nitoe upumbavu kwa asilimia ya michango inayoenda kwenye zawadi, rambirambi na dharura ewe mwerevu. . . . .
 
Last edited by a moderator:
SOLOMO

napingana nawe kuhusu suala la MSHIKAMANO. hv walimu wana mshikamano gani katika nchi hii? walimu ni kati ya watumishi wa ovyo kabisa katika nchi hii.
 
Last edited by a moderator:
Wakati nimemaliza kidato cha sita,nikiwa natafakari naangalia nikasomee nini cha kuisaidia jamii! Kuna Mwalimu mmoja aliniambia "kijana wangu ukiamua kua mwalimu maisha yako yote yatakua ni kuvaa suti moja tu na tai kila siku,kusubiria mshahara kwa ajili ya kulipa madeni,utazaa watoto wako wanne na kujenga kijumba kimoja cha vyumba vitatu basi na usubirie hela ya kustaafu" Mpaka leo sijafanikiwa kuipata vizuri kauli ya mwalimu huyo aliyekua amebakiwa na miaka 5 kustaafu alimaanisha nini.

ukitaka kujua alichomaanisha ingia kwenye fani ya ualimu ndipo utajua vzr.
 
Kama umefoji cheti unaweza kudai haki yako?

Uijue ofisi ambayo hata ukiwa na shida haiwezi kukupa msaada. Wapo walimu wapya wanaopangwa vituo vya kazi na wanacheleweshewa fedha ya kujikimu kabla ya kupokea mshahara lakini hata hao viongozi wa CWT hawawezi kuwasaidia.

Kumbuka pia walimu wengi ni wanawake hivyo woga na kutojiamini huchangia kufail kwa movement yeyote itakayoanzishwa.

Pia usiangalie CWT peke yake maana sio ya kwanza kwani kulikuwa na;
1.UTS mwaka 1962.
2.TSC mwaka 1989
3.TSD mwaka 2002
Hizo zote zilianguka kwakuwa zilikuwa zinajaribu kuegemea pande mbili (kwa walimu na serikali). Walimu wakitoa madai yao wanasikiliza bila kutekeleza na hapohapo wakitaka kugoma wanawatuliza.

mwishoni mwaka 1984 TPTA ikaundwa na kudumu mpaka 1994 Ambapo ilisambaratishwa na serikali kwakuwa ilikuwa na dhamira ya kweli ya kuwakomboa walimu.

Hivyo CWT inafanya yaleyale ya miaka ileee......

Kinachotakiwa ni kuiga mfano hapo jirani (Kenya).
 
Walimu wa nchi hii ni wapumbavu sana

umeona eeh? kuna dada yangu mmoja mwalimu wa s/msingi mwenye diploma (ya CHUPI) lakini kila siku nikijaribu kumthathimini naona hafanani na kiwango cha elimu yake (iliyopo kwenye cheti).

huwa najiuliza: hv hawa walimu wa nchi hii ni nani aliyewalaani? eti tangu dada huyu atimize miaka 18 hajawahi kujiandikisha wala kupiga kura kwa 7bu haoni umuhimu huo! hii ndiyo aina ya walimu tunaowategemea kufundisha watoto wetu. watoto wetu wataelimika kweli?
 
kson m, hicho chama kibaitwaje kina malengo gani?
 
Last edited by a moderator:
Tusiwatukane jamani wametutoa mbali walimu tujadili tu hoja. . . .,wengine wake zetu ati
 
Wameonewa nn lete suluisho, mnafikiri hilo jitu jingine linalokuja halitakuwa na makato heeee? Baada ya kuona mnataka kuazisha bank sirikali imeona mtakuwa na nguvu sasa inataka kuwagawa ili mnyonywe vizuri, mkiua cwt mjue mmekwisha, sirikali haitaki trade union yenye nguvu kama yenu.

Hakuna kunakoanzishwa bank ya walimu nchi hii labda useme wametumia jina la walimu kujinufaisha
 
inawezekana una lengo zuri sana la kueleza kile kinachokukera au kutaka kujua kile usichofahamu na pia inawezakana hata unachotaka kukieleza kimekupotea. labda naomb nikuulize swali moja;je,unafahamu matatizo ya walimu? au kwa mtazamo wako walimu wanamatatizo gan kadr ya hsia zako?

mtoa mada yuko sahihi 100%. moja ya matatizo ya walimu ni KUTOKUJITAMBUA (kama mtoa hoja anavyobainisha). malizia na matatizo mengine unayoyajua wewe ili tupate orodha kamili ya matatizo hayo.
 
Kwa kifupi: sio wajinga wala si wapumbavu.

Tatizo ni la kimfumo (systemic problem dues to issues inherent in the overall system...)

sasa mkuu hapa na wewe umeandika nini..? au na wewe ni mwalimu..?
maana naona hakuna "concordial relationship".
 
Back
Top Bottom