Hivi wakati mwingine huwa tunalaumu wanaume pasipo kujua?

Mamushka ; dharula zipo na kama weye ni mke wa aina dada Asha alyemsema hili la dharula halitakuwa hatarishi upande wako

MJ, Mimi ninajiamini ntafanya vyote, na huyo dada ntamdhibiti, vilevile hatapata hata nafasi ya uchawi, akija naushirikina wake ataondoka mwenyewe kwa jina la mungu ninaemuamini.
 
Mosi, penzi halina mitishamba.

Pili, mimi kama mimi hakuna mwanamke atakayenifanya nimpende pasipo mimi mwenyewe kumtamani na kutaka kulala naye. Hivyo kama ningekuwa na mke halafu nitoke nje ya ndoa basi huyo mke wangu ana haki ya kuzielekeza lawama zote, shutuma zote, na adhabu yoyote au zozote zile atakazoona zinafaa kwangu mimi. Kuelekeza nguvu na hasira kwa mtu niliyecheat naye ni sawa na kupaka rangi upepo! Tatizo siyo yule nilicheat naye. Tatizo ni mimi niliyecheat.

Tatu, huyo mama kwenye hiki kisanga ni aongee tu na mumewe ajue kinachoendelea. Kwani hata akimfukuza huyo msichana wa kazi hiyo haimaanishi huyo mumewe hawezi kutoka nje ya ndoa. Kudili na msichana wa kazi, narudia tena, ni sawa na kupaka rangi upepo!!!!
unazijua nguvu za giza wewe?
 
dah katika hali kama hii...nitafurahi sana kama nitampata mke bora anayemjua mungu,coz me naamini ukiwa na mke anaye mtanguliza mungu ktk kila jambo familia yako itakua mfano wa kuigwa even ur kids watakua tofauti na wenzao
 
Nadhani respects on both sides in Muhimu. Baba ajue huyu ni dada wa kazi na abaki hivyo. na sisi wakina mama, let us put the limits,,, dada anaweza kufanya nini na wapi haingii! Wanawake wengine ni wavivu na wazembe, utakuta kaacha chumba chote wazi, dada wa kazi ruksa! Shauri yako!
 
Sisi wanaume tunawindwa sana kila kona!nani mwili huu!limbwata sisi,mahouse gal sisi,nyumba ndogo ni sisi,walioko mtaani wanatutamani sisi jamani tutakuwa wageni wanani?

Nyumba ndogo huwa mnaanza kuzitamani wenyewe kakakiiza ,mkishaingia mkenge ndio wanataka wawamiliki kabisa .
 
Kweli inasikitisha sana na haya mambo yapo sana tu siku izi na wengi wanaangalia hapa kuna nini cha kujinufaisha ndo anaanza kuhangaika nacho.
Lakini ukweli utabaki palepale hakuna nguvu kubwa kama kusali na kumtegemea Mungu.Tuchukulie ni mama anayejali sana familia yake na majukumu yake ya kikazi yanamuhitaji kusafiri na wakati mwingine kuchelewa kuwepo nyumbani utasema unalinda ,utalinda kwa nguvu zipi.Unaweza usimpe nafasi ya kuwa karibu na mumeo lakini akawa na dawa hata za kumuita mtu kwa jina akiwa usingizini.

Kikubwa ni kusali na yeye mwenyewe kukubali na kuamua kufanya mema kwa ajili ya familia yake

Naona siku hizi watu wanaangalia maslahi kuliko upendo wa dhati ...iko kazi sijui tutafika...
 
Mosi, penzi halina mitishamba.

Pili, mimi kama mimi hakuna mwanamke atakayenifanya nimpende pasipo mimi mwenyewe kumtamani na kutaka kulala naye. Hivyo kama ningekuwa na mke halafu nitoke nje ya ndoa basi huyo mke wangu ana haki ya kuzielekeza lawama zote, shutuma zote, na adhabu yoyote au zozote zile atakazoona zinafaa kwangu mimi. Kuelekeza nguvu na hasira kwa mtu niliyecheat naye ni sawa na kupaka rangi upepo! Tatizo siyo yule nilicheat naye. Tatizo ni mimi niliyecheat.

Tatu, huyo mama kwenye hiki kisanga ni aongee tu na mumewe ajue kinachoendelea. Kwani hata akimfukuza huyo msichana wa kazi hiyo haimaanishi huyo mumewe hawezi kutoka nje ya ndoa. Kudili na msichana wa kazi, narudia tena, ni sawa na kupaka rangi upepo!!!!

NN sidhani kama mama ataweza kuvumilia kukaa na binti ambaye tayari hamwamini ..akishindwa mitishamba yake anaweza weka hata sumu
Chukua tahadhari mapema
 
Ahimidiwe Mungu aishie na kumiliki. Watoto wa kazi ni hatari. Wengine unapowaacha nyumbani wanajifanya ndo wamiliki wa nyumba. Ukiwaachia watoto wadogo hasa wa kiume wanaanza kumshikashika na kumchezea mtoto DUDU yake hadi mtoto anashikwa na ule ugonjwa wa kutahiriwa angali akiwa mdogo sana. Fanya uchunguzi utapata majibu.

Jamani ..unaniogopesha ....ooops unaweza kutamani kuwa mama wa nyumbani ..
 
...Amen, amen 1stLady, pheeewwww!

unajua haya mambo sio hawa housemaids peke yao,
hata huko 'nyumba ndogo' unadhani inakuwaje?
Wanatuloga kweli hawa watu... heri tu mtuombee enyi wake zetu wapendwa.

Angalia IMF chief Dominique Strauss-Kahn nae alivyoponzeka maskini,
arrrghhhh[/I],....huu uchawi umeenea sana duniani!

Bwana Mbu na wewe unajuaje kama jamaa alitupiwa alitupiwa Nduba :biggrin1:
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Tunatakiwa kusali na kumwomba Mungu
wasichana wandani wamekuwa wakitumiwa kwa uchawi, madawa na mambo mengi kwa ajili ya kuvuruga familia wanamoishi. Hii inatokana na wivu kutoka jamii inayotuzunguka au tamaa kwa madada wa kazi ya kutaka kuolewa na boss wake
ikishatokia kama hivyo bora aondoke sababu huwezi jua atafanya nini next time
 
Hivi haya madudu huwa kweli yanakamata hawa wenzetu vichwa ngumu?
sasa tufanyeje na hawa ma HG? maana na sie tunachoka sana, kazini home na bado usiku mtu anataka umpigie kazi lol mie acha nije kuibiwa tu lazima HG niweke
 
bahari hailindwi,unaweza kupekua begi la house girl uko nyumba ndogo je??utapata wapi access ya kujua mumeo anawekewa nini huko??sali tu:dance:

Umeona eeh! Just do your best and leave the rest to God. Ukifikiria sana unaweza kuchanganyikiwa.
 
Hivi haya madudu huwa kweli yanakamata hawa wenzetu vichwa ngumu?
sasa tufanyeje na hawa ma HG? maana na sie tunachoka sana, kazini home na bado usiku mtu anataka umpigie kazi lol mie acha nije kuibiwa tu lazima HG niweke

Kwanza faham kuwa matatizo tumeyasababisha sisi binadam wenyewe,from the bigining Mungu aligawanya majukumu,mwanamke alipangiwa kulea familia,haya mambo ya hausegirl ni matatizo ya kujitakia,pili;inaonekana mnaupa uchawi uwezo mkubwa sana,ili mtu alogwe ni lazima yeye mwenyewe aruhusu kulogwa!!
 
Enzi hizo Mungu anatupangia majukumu ya kulea familia kulikuwa wanaume wanaenda vitani na mashambani labda na hakuna mwanamke aliyekuwa anafanya kazi maofisini i guess, sasa dunia imebadilika mwenzangu tufanyeje?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom