Hivi wakati mwingine huwa tunalaumu wanaume pasipo kujua? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi wakati mwingine huwa tunalaumu wanaume pasipo kujua?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by FirstLady1, May 15, 2011.

 1. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Jamani nimeanza kuuliza hilo swali baada yakuona kisa na mkasa sehemu today nikiwa nimefika tu home nikitokea church...Binti wa kazi kumbe katoka kwao kwa shughuli maalum ,,
  Katika kupanga panga nguo zake mara madubwasha yakadondoka...kalikuwepo katoto ka 5 yrs chumbani na dada wa kazi kakamuuliza dada nini hii..Binti kamwambia ni dawa za tumbo mara mtoto akamwita mama yake aje kuona ...mama kuingia chumbani aliyoyakuta kapigwa butwaa kitanda kimejaa mavitu ya ajabu si vibuyu ,,...si miti ya aina mbali mbali..madude meusi ya kutisha mama kachanganyikiwa ...
  kaita majirani msichana wa kazi kaanza kulia anaulizwa kwa nini katembea na miti shamba kagoma kusema alipotishiwa sana kama anapelekwa police ndipo aliposema mama yake kamwambia aangalie kama mme wa huyo mama ana uwezo aanze kuogea dawa na zingine aangalie mama akiwa hayupo ajitahidi kumuwekea baba kwenye chakula anachokula ili baba amwache mkewe binti aolewe..
  Na kama baba atakuwa hana uwezo atafute sehemu nyingine .....mama wa watu kumuuliza binti kama alishaanza kumuwekea mmewe kakataa kata kata eti ndo alikuwa anataka kuanza ..

  Hii kesi bado inaendelea kwa mama wa binti kutafutwa... swali ....

  1. Hivi kumbe kuna mambo yanayoendelea pasipo nyie kujitambua ?
  2.Kina mama inabidi tuwaombee waume zetu sana
  3.Ni lazima kukagua mabegi ya mabinti zetu wakifika??
  4..Hivi haya mambo ya ukalumanzira yapo ??

  Ooooops!!
   
 2. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,547
  Likes Received: 2,260
  Trophy Points: 280
  Sisi wanaume tunawindwa sana kila kona!nani mwili huu!limbwata sisi,mahouse gal sisi,nyumba ndogo ni sisi,walioko mtaani wanatutamani sisi jamani tutakuwa wageni wanani?
   
 3. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Dah! FL1 narudii.....
   
 4. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #4
  May 15, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  [FONT=&quot]First Lady 1, please forgive me kwa urefu wa post….[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Inasikitisha sana mambo ambayo yanatokea katika jamii na hasa katika ndoa… Imekua ni mtihani kwa kweli… Sijui kama nitakua natoka off topic (sorry – kueleweka nataka nidadafue the way naelewa).
  [/FONT]

  [FONT=&quot]Kutokana na ukweli kua maisha yamebadilika sana in every level hivyo kupanda kwa gharama kila sehemu ugusayo hasa ukitaka kitu quality ili kupata huduma ya uhakika iwe education, malazi/makazi, matibabu, chakula, - facts zinazofanya wenza wote wawili mujishulishe hivyo kama mna watoto mnamtafuta binti wa kuwasaidia… Tatizo ndo linakuja hapo.. NDIO akina dada tuko busy saaana lakini jamani are we so busy to the extent huwezi nyanyua kidole hata kidogo??? – Nauliza/nasema hivi in the sense kua NDIO Msichana wako anakupa support katika kuendesha/kuangalia nyumba lakini je kuna haja ya kumpa full access kwa mumeo… kwa mtazamo wangu wadada/mama wengine huyataka mambo kama haya ya kwenye thread hii kuwatokea tokana na the way anendesha mambo yao katika ndoa yake….
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Kwanini umpe msichana wako FULL ACCESS kwa mumeo???? Ladies if you love your man and proud of him at all cost minimize vitu/mambo yawezao kumshawishi (akina mama tuna njia tofauti hii ni kwa wale wataoona I am right) … Kama Speaker alivyosema katika moja ya post.. "Never let your man's mind wander .... " Hivyo akina dada/mama tujiulize je wewe personaly umempa msichana wako (maarufu kwa house girl) Full Acces OR No Access kwa mumeo???[/FONT]
  [FONT=&quot]FULL ACCESS[/FONT]

  [FONT=&quot]Anaingia chumbani kwenu (eti kufanya usafi…lol!) na worse enough yeye ndo anatandika kitanda ambacho wewe na hubby mnajimwaya; Anapika mwenyewe (si mbaya sana) but worse enough yeye ndo anaandaa chakula na kumkaribisha hubby mezani..; Anampokea mizigo akifika – in other words mumeo anatangulia kufika kabla yako kila siku (bad news - kwa wale ambao iko nje ya uwezo …); Ndio afue nguo (for maybe you have no time) but ziwahi hakuna haja ya hubby kuulizia soksi ikowapi which at the end of the day atamfuata binti kumuuliza mana anajua wazi hufui wewe…. Etc.[/FONT]

  [FONT=&quot]NO ACCESS[/FONT]
  [FONT=&quot]Huna nafasi ya kupika, but unahakikisha umekagua chakula, umeandaa mwenyewe na umemkaribisha mwenyewe mezani, Ndio nguo hafui but at least anahakiki zimetakata zimenyoshwa vizuri na zinarudishwa room kabla hubby hajazimiss..; Ana hakikisha kila mumewe anpokuwepo nyumbani yupo tayari home' labda in rare cases plus kujitahidi kurudi kabla ya the hubby… etc. Kwa ufupi kutojenga mazingira ya wao kuwa karibu…. House girl awe karibu na watoto…. BUT not the husband[/FONT]

  [FONT=&quot]Note; Wanaume hawalindiki hasa akiwa na nia but at least ikitokea utasema "I tried my best but he is just a Ba****"[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  swirry thanx so much kwa maelezo mazuri sana ..na tulio kwenye ndoa tunajitahidi kufanya wajibu wetu juu ya wenza wetu ...swali langu hapa ni hili la kumkamata mwenza wako kwa nguvu za giza...hapa ndpo pamenishangaza mwenzio....:smow:
   
 6. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  bahari hailindwi,unaweza kupekua begi la house girl uko nyumba ndogo je??utapata wapi access ya kujua mumeo anawekewa nini huko??sali tu:dance:
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  :biggrin1::biggrin1:
   
 8. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #8
  May 15, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Naelewa dear ndo mana nikaomba msamaha kidogo kutoka off point....
  Ila samahani sijaelewa kumkamata mwenza na nguvu la giza... Si ni the house gal ndo alikutwa???
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  May 15, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hause gal kumkamata mwenza wako na nguvu za giza sorry hizi lugha Asha D
   
 10. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #10
  May 15, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160


  Thats the point.....+ kuomba sana!
   
 11. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #11
  May 15, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kweli inasikitisha sana na haya mambo yapo sana tu siku izi na wengi wanaangalia hapa kuna nini cha kujinufaisha ndo anaanza kuhangaika nacho.
  Lakini ukweli utabaki palepale hakuna nguvu kubwa kama kusali na kumtegemea Mungu.Tuchukulie ni mama anayejali sana familia yake na majukumu yake ya kikazi yanamuhitaji kusafiri na wakati mwingine kuchelewa kuwepo nyumbani utasema unalinda ,utalinda kwa nguvu zipi.Unaweza usimpe nafasi ya kuwa karibu na mumeo lakini akawa na dawa hata za kumuita mtu kwa jina akiwa usingizini.

  Kikubwa ni kusali na yeye mwenyewe kukubali na kuamua kufanya mema kwa ajili ya familia yake
   
 12. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #12
  May 15, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180


  Mpenzi hio imagination tu inanifanya niwe na hasiraaa ile mbayaaaaa........ Niseme tu ukweli hapa FL1 - sielewi nitakafanya nini hako kabinti.... kweli sijui dear.... Mana nikiangalia upande wake ni kua she is young (mara nyingi hua hivyo) na anaoneka kalelewa katika malezi ya kuonesha she has to do anything to steal a man... tatizo liko sana kwa mamake... sijui niseme kwa bibi yake... mana tabia hizi za ushirikina zipo kurithishana for inakua controlled na imani...

  But all in all .... Sijui nitamfanya nini huyo binti,,,, kweli sijui..... Ndo maana FL1 my man will be taken care by me! me! me! in my home... Bcoz I try my best by doing what i think is best... Mi mvumilivu na napenda ku-reason-Hivyo hunipa nafasi kua mwanaume anaponitubua hakuna la ziada ninaloweza fanya ili nimfurahishe.... akileta upuuzi usiokua na msingi wala hauteteki....SIMTAKI TENA.... (naona natoka tena off topic)
   
 13. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #13
  May 15, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Tena hapo ushukuru umkamate kabla hizo konokono alizobeba hajamlisha mumeo.

   
 14. Egyps-women

  Egyps-women JF-Expert Member

  #14
  May 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  FL1 unashangaa nguvu za giza ? hata kwenye bible mbona imeandikwa wachawi walikuwepo kesheni mkiomba ...
  haya mambo yapo wewe endelea kumuombe tu wa kwako
   
 15. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #15
  May 15, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Ndo hapo Chauro.... Mana ikitokea kakupiku tushazoea kuwa laumu wanaume, ningechulia kua mume wangu ana tamaa... Sasa ndo nimemkamata hivyo kabla.... ha ha ha..... kama nilivyosema sielewi nini nitafanya..... Ninachoelewa ni kua atajuta!!!!!!!!!
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  May 15, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mosi, penzi halina mitishamba.

  Pili, mimi kama mimi hakuna mwanamke atakayenifanya nimpende pasipo mimi mwenyewe kumtamani na kutaka kulala naye. Hivyo kama ningekuwa na mke halafu nitoke nje ya ndoa basi huyo mke wangu ana haki ya kuzielekeza lawama zote, shutuma zote, na adhabu yoyote au zozote zile atakazoona zinafaa kwangu mimi. Kuelekeza nguvu na hasira kwa mtu niliyecheat naye ni sawa na kupaka rangi upepo! Tatizo siyo yule nilicheat naye. Tatizo ni mimi niliyecheat.

  Tatu, huyo mama kwenye hiki kisanga ni aongee tu na mumewe ajue kinachoendelea. Kwani hata akimfukuza huyo msichana wa kazi hiyo haimaanishi huyo mumewe hawezi kutoka nje ya ndoa. Kudili na msichana wa kazi, narudia tena, ni sawa na kupaka rangi upepo!!!!
   
 17. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #17
  May 15, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwa hali hii kuna haja ya kua mnawapeleka wasichana wa kwenye maombezi na kuchunguza familia zao kidogo kabla hamjawakabizi mamlaka ya kuangalia familia zenu!!

  Ila kama alivyoelezea partner wangu hapo juu jaribuni na jitahidini sana contact kati ya baba mwenye nyumba na dada wa kazi yawe minimum!!!Maana ikiwa hivyo hata kwa hizo tinguli na madawa msichana hatapata mwanya wa kumchanganyia mumeo.Hata mlango wa chumba chenu ikibidi unafunga mpaka mtakaporudi kwahiyo kama aliambiwa awaekee chini ya godoro anakosa mwanya....usafi unafanya mwenyewe
  weekend....chakula unajitahidi kupika kila unapoweza msije mkalishwa vitu vya ajabu ajabu!!!

  Mama wa kwanza kweli wakati mwingine inaweza kutokea isiwe mwanaume wala mwanamke mwenye kosa....ongezeni maombi wamama!!!!
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  May 15, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Watu kibao wapo na watu ambao hata hawajawahi uwatamani....ngoja uendewe bwagamoyo ndo utajua!
   
 19. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #19
  May 15, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180


  Thanks partner...
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  May 15, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Aaah wapi! Penzi halina mitishamba bana. Kwanza uchawi haupo. Kama upo basi nawapa rukhsa hao wachawi waniloge tuone kitakachotokea.
   
Loading...