Hivi vibwengo kweli vipo?

Hivi vibwengo kweli vipo?

Kuna jamaa yangu alikuaga mtu wa club sana,aliwahi kunipa stori kuna siku mida ya tisa tisa night kali anatoka zake kuruka debe ile anakatiza mitaa fulani akakutana na katoto kama ka miaka minne hivi dogo aka muomba fegi jamaa hilo nduki lake si mchezo na pombe yote iliish.mpaka leo akienda club kurudi hadi kupambazuke kabisa.
 
Imani mbovu tu..kila mtu anadai fulani alukutana navyo mara nilisikia...hakuna hata mmoja mpaka sasa aliyeviona!!
 
Kuna jamaa yangu alikuaga mtu wa club sana,aliwahi kunipa stori kuna siku mida ya tisa tisa night kali anatoka zake kuruka debe ile anakatiza mitaa fulani akakutana na katoto kama ka miaka minne hivi dogo aka muomba fegi jamaa hilo nduki lake si mchezo na pombe yote iliish.mpaka leo akienda club kurudi hadi kupambazuke kabisa.

Imani mbovu tu..kila mtu anadai fulani alikutana navyo mara nilisikia...hakuna hata mmoja mpaka sasa aliyeviona!!
 
Kigonsera sec school walikuwepo...

Ni hatari tupu, kuna jamaa alikuwa anaishi bweni la TWIGA anaitwa Myoba alikuwa anakumbana navyo sana usiku. Vinapenda sana bweni la Twiga pale Caigo!
 
Vibwengo vipo vinyamkera pia vipo mashetani yapo majini na maruhani pia yapo ila ni vitu visivyoonekana moja kwa moja kama wana JF ambao tunasomana post zetu na kufanya imagination tuu kuwa pen fine huyu katika uhalisia wake anafanana hivi au vile
mizimu pia inaingia kwenye kundi hilo na sura zao haziko kamili nyingine ziko nusu nyingine robo nyingine kama moshi nyingine kama zinatiririka na nyingine kama zinapenyeka! Lakini vile vile kuna zile ambazo ukiziona zinakuja na kupotea na huwezi kuziona na kuzitambua kama ni mnyama mdudu binadamu kizuka nk
Hivi ni viumbe vinavyoishi kwenye ulimwengu usiionekana na mara nyingine ulimwengu wa kufikirika kuna nguvu ambazo ukiweza kuwa Nazi ndo unaweza kuviona na hata kuvilimiki
 
Old Moshi kulikuwa na ngolomiko, Umbwe sek kulikuwa na ndrua Hasa kule mtoni
 
Vibwengo ni aina Ya Majini wanaopenda kutembea usiku na Vijinga vya moto

haswa pembezoni mwa bahari ni kweli Mashetani hawa wapo hswa katika miji yenye Bahari kwamfano Mji ya

Dar,Tanga na Mtwara

wanapatikana kwa wingi Mashetani wa aina hiyo ya Vibwengo. Na haswa wakati wa usiku kandoni kandoni

mwa ufukweni mwa bahari

unaweza kuwaona wakati wa usiku mwingi ukiwa wewe ni mtembezi mwa ufukweni mwa bahari kwa wakati

huo ni Mashetani

wanaopenda sana kuwachezea Wavuvi wakati wa usiku baharini. Wavuvi wengi wanawajuwa hao Mashetani

wa Vibwengo ni wafanyaji wa

vituko vingi nyakati za usiku haswa ukiwa baharini au ufukweni mwa bahari wanakujia na kijinga cha moto

kukuchezea akili yako na wanapenda sana kuwachezea binadamu Nyamuleha jr

Nipe mbinu za kuviona vibwengo face to face MziziMkavu.
 
Last edited by a moderator:
Miaka ya 90 kinondoni msufini ilikuwa kawaida ya kijitu kifupi kilichovaa kanzu nyeupee na mzuzu mrefu na barakashia kuwatokea watu chooni kama kuna mtu anabisha akawaulize watu wa kinondoni msufini wa enzi hizo.

Huyu kibwengo alikuwa anawatokea watu wakati wapo bafuni wanaoga hapo mtu akishajipaka sabuni usoni ndio atasikia salamu alisalimiwa asalam alyekum kwa kuwa una mapovu utataka unawe umuangalie si unajua uswazi maji kwenye ndoo ile uimame uchote maji utapigwa makofi na utatoka chooni uchi.
Ukihadithiwa na ukabisha ukienda kuoga unaye.
sio hadithi ni ukweli.
 
kahtaan anayafahamu vizuri, was born and bred with them
 
Last edited by a moderator:
Ukienda usiku kanisani hali ya kuwa una janaba (yaani umefanya ngono bila kuoga) utaviona tu!

Vinafanana sana na ile picha ya kadhungu iliokaa kama alama ya jumlisha.
Na mama Nyakageni ndio mfugaji pale Ujiji, kwa wapiga Gongo!

umesha anza utoto wako kwanza nani ame kuita humu?
 
Last edited by a moderator:
Teh teh teh!
A love you too.

Muulize dada Nyakageni hapo juu kwanini kaniita huku kwenye miungu ya wagalatia!

Ukienda pale kwenye kanisa la pengo karibu na baharini nyakati za usiku utavikuta vibwengo kwa uchache kama sita hivi.

Vina tabia ya kuvaa zile chupi za Kizamani za VIP! na misalaba kiunoni!

Hatari sana vile.

Kwa taarifa yko vibwengo ni vifupi sna,vinavaa kanzu/msuli na kibarakashee!
 
Last edited by a moderator:
Mwingine alistuka usingizini akaona kibwengo kimelala pembeni yke;akarusha ngumi ikatua ukutani.Hakuweza kufanya shughuli yoyote kwa mwezi mzima kwa maumivu aliyoyapata.

Hahaha nmecheka sana hyo sentensi..

Kimsingi waTZ huwa hatuaminig mambo mpaka yatutokee,m nmewahi kusumbuliwa na vibwengo nilipokuwa nasoma HAPPY SKILFUL INTERNATIONAL SCHOOL,iliyopo tabata segerea..
Nilisumbuliwa sana kias kwamba usiku ukiingia tu napata hofu,had pale nilipo omba ruhusa shuleni na kurud nyumbn nikapelekwa kwa mganga tatzo likaisha kabsa..


Hili ni tangazo la biashara
 
Kuna jamaa mmoja alikuwa na masihara/kutania/kukosoa/wenzie sna.Ilikuwa siku ya ijumaa baada ya kurudi bwenini toka "prepo"akaanza kutania kila mtu bwenini kuanzia kitanda kimoja hadi kingine(baunsa hakuwepo siku hiyo).
Baada ya mda kila mtu akapitiwa na usingizi kivyakevyake tukalala.
Mida ya saa kumi na moja kasoro kila mtu alistuka baada ya kusikia kelele kubwa (kama yowe vile).Kuwasha taa tukamwona yule jamaa anaependa kutania wenzie kasimama dirishani anaangalia tu nje.Tukamuuliza vp, kuna nn?hakujibu,kila tukimuuliza aeleze kilichotokea anapiga kimya na kukasirika.
Basi watu wakaamua ku-conclude kuwa jamaa keshatafunwa na Kibwengo.Kila mtu akawa anacheka kivyakevyake hadi kukakucha.Anzia hapo jamaa akitaka kuleta utani,ni kumkumbushia tu hiyo movie na utani anaacha.
 
Pamoja kamanda!

Lkn mara zote mi nachokozwa! We soma huko mwanzo utaona mwenyewe.

Mimi wagalatia mbona naishi nao miaka yote tu? Tatizo ni wale wavuta bange.
Hata Pengo nimeshakwenda nae Lunch siku moja. Muulize tu atakupa majibu.

Basi usikimbizane na chizi waweza onekana chizi zaidi yake
 
Nipe mbinu za kuviona vibwengo face to face MziziMkavu.
ukitaka kuviona hivyo Vibwengo nenda usiku wa manane Kandoni kandoni mwa baharini kila ikifika usiku wa saa 8 au saa 9 usiku huwezi kufikisha siku 14 bila ya kuwaona na je ukiwaona utaweza kupambana nao? Swali gumu kujibika kazi kwako Utajibeba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom