Hivi vibwengo kweli vipo?

Hivi vibwengo kweli vipo?

Waliosoma Jitegemee(Jiteute) enzi za Massawe watakumbuka jinsi vibwengo vilivyokuwa vinasumbua baadhi ya watu.
Kuna jamaa mmoja alikuwa hawezi lala mwenyewe lazima aombe mtu alale nae coz alikuwa anasumbuliwa sna na hv vibwana.
Kwenda chooni mwenyewe usiku mbinde lazima uombe kusindizwa.
Tisa kumi kuna njemba moja ilikuwa baunsa imepanda hewani halafu ni mbavu nene kishenzi.Alikuwa akisema/kukutuma kitu lazima uache mambo yko utekeleze anachokuagiza.Siku moja aliamka kama saa tisa usiku kwenda class kupiga msuli.Akapitia kwanza bombani anawe uso kuondoa wenge la usingizi.Alipoanza kuinama ili afungue maji alipigwa bonge la kelbu ya mgongoni,akasimama wima ila hakuona kitu;wkt anatafakari alistukia bonge la kelbu kisogoni;hapo ndo mbio kama za Usain bolt zilipoanza tukastukia mlango wa bweni upo chini huku njemba ikipiga mayowe kama kafukuzwa na simba.
Mwingine alistuka usingizini akaona kibwengo kimelala pembeni yke;akarusha ngumi ikatua ukutani.Hakuweza kufanya shughuli yoyote kwa mwezi mzima kwa maumivu aliyoyapata.

Dj Mat u made my day, hahaaaaaaaaa
 
Hahahahahh' dah mwana hyo stori ya njemba imenifanya nicheke hadi michoz imentoka' boading kulikua na vituko sana' jamaa alichezea kelbu za kutosha tuu
Hahah

Yaani njemba ilichezea kelbu za kumwaga.Badala ya kukimbia mapema yy akataka kuzichapa na kitu ambacho hakioni.Kila akigeuka anachukua kelbu,akaona isiwe tabu akatimua mbio iliyoandamana na mayowe ya kufa mtu!
 
Niliwahi kusikia wanafunzi huko masekondari zamani walikuwa wanaonaga wanyama flani kama binaadamu kama mashetani sasa naomba mwnye kuwafahamu au mwenye picha ya hao vibwengu aitupie eti hata wengine walipo lala walikabwa usingizi na hao vibwengu je hii ni myth au ni jambo la kweli

Hakuna kitu kama iko..ila watu watakulazimisha wapo..ni kama hadithi za abunuwasi..hakuna vibwengo uchawi au mizimu..ila umaskini wetu na ulimbukeni tumeshupalia hayo mambo..
 
Hakuna kitu kama iko..ila watu watakulazimisha wapo..ni kama hadithi za abunuwasi..hakuna vibwengo uchawi au mizimu..ila umaskini wetu na ulimbukeni tumeshupalia hayo mambo..

Ni kweli,bila kuona huwezi amini ila vibwengo vipo mkuu!
 
Waliosoma Jitegemee(Jiteute) enzi za Massawe watakumbuka jinsi vibwengo vilivyokuwa vinasumbua baadhi ya watu.
Kuna jamaa mmoja alikuwa hawezi lala mwenyewe lazima aombe mtu alale nae coz alikuwa anasumbuliwa sna na hv vibwana.
Kwenda chooni mwenyewe usiku mbinde lazima uombe kusindizwa.
Tisa kumi kuna njemba moja ilikuwa baunsa imepanda hewani halafu ni mbavu nene kishenzi.Alikuwa akisema/kukutuma kitu lazima uache mambo yko utekeleze anachokuagiza.Siku moja aliamka kama saa tisa usiku kwenda class kupiga msuli.Akapitia kwanza bombani anawe uso kuondoa wenge la usingizi.Alipoanza kuinama ili afungue maji alipigwa bonge la kelbu ya mgongoni,akasimama wima ila hakuona kitu;wkt anatafakari alistukia bonge la kelbu kisogoni;hapo ndo mbio kama za Usain bolt zilipoanza tukastukia mlango wa bweni upo chini huku njemba ikipiga mayowe kama kafukuzwa na simba.
Mwingine alistuka usingizini akaona kibwengo kimelala pembeni yke;akarusha ngumi ikatua ukutani.

dah nimecheka hd basi.
 
ukitaka kuviona hivyo Vibwengo nenda usiku wa manane Kandoni kandoni mwa baharini kila ikifika usiku wa saa 8 au saa 9 usiku huwezi kufikisha siku 14 bila ya kuwaona na je ukiwaona utaweza kupambana nao? Swali gumu kujibika kazi kwako Utajibeba.
Kwani vina nini mpaka nishindwe kupambana navyo?
 
Niliwahi kusikia wanafunzi huko masekondari zamani walikuwa wanaonaga wanyama flani kama binaadamu kama mashetani sasa naomba mwnye kuwafahamu au mwenye picha ya hao vibwengu aitupie eti hata wengine walipo lala walikabwa usingizi na hao vibwengu je hii ni myth au ni jambo la kweli

Sisi Kwetu Tunaita VISUKA VIPATIKANA MAKABURINI
 
vibwengo vipo mpaka kesho hayo ni majini tu yanajibadili style
waulize madereva wanaosafiri safari ndefu watakuambia sometimes vinasababisha ajali unaweza kukikuta katikati ya road ukikwepa tu chali.
 
Kibwengo na Popobawa ni mtu na kaka/ake wote watoto wa mashetani
 
Mimi nimewahi kukutana na jini baadae nikakutana pia na vibwengo. Inatisha sana wakuu usiombe ukutane na hawa viumbe. Imagine saa9 usiku unakutana na kibibi na babu vina umbo dogo lipatalo sm30 wameshikana mikono wanatembea taratibu barabarani
 
Vibwengo (Elves)

Kibwengo (Elf)Kibwengo ni aina ya kiumbe kisicho cha ulimwengu ambacho huhusika sana katika hadithi za kitamaduni za Kiingereza na Kiskandinavia. Wao huwa na nguvu za kichawi na ni vigeugeu na watundu katika mambo ya kibinadamu. Neno ?vibwengo? wakati mwingine hutumika kwa istilahi ya jumla ya kurejelea vichimbakazi. Vibwengo husawiriwa kama vijana ambao waliacha kukua wakati wa kubalehe na baada ya hapo huwa hawazeeki. Vibwengo hutofautiana kwa ukubwa kuanzia 4?10?? hadi 5?8??. Kwa kuwaangalia tu, ni vigumu kujua jinsia ya kibwengo. Jinsia zote huwa na macho ya kuonyesha hisia, masikio yenye ncha kali na madume huwa hawana nywele usoni. Wakati vibwengo wanazidi kuzeeka, wao huwa na hekima zaidi na hisia zao huwa kali zaidi. Vibwengo wanaweza kuishi kutoka miaka 100 hadi zaidi ya miaka 1000. Katika hadithi za Kiswahili, kibwengo ni pepo mdogo mbaya wa baharini anayeaminika kucheza na wavuvi wanaovua samaki usiku. Tahajia ya kwanza sanifu ya kuandika lugha za Vibwengo iliundwa miaka ya 1900 na J.R.R. Tolkien.

An elf is a type of supernatural being, prominently featuring in traditional British and Scandinavian folklore. They usually have magical powers and are capricious and mischievous in human affairs. The word ?elves? is sometimes used as a general term for fairies. Elves are depicted as youths who stop growth at puberty and never age thereafter. Elves vary in size from 4?10? to 5?8?. At a glance, it is hard to discern an elf?s sex. Both sexes have big expressive eyes, pointy ears and the males lack facial hair. As elves get older they get wiser and their senses become sharper. Elves can live from 100 to over 1000 years. In Swahili folklore, the elf is an evil diminutive sea-spirit that is believed to play with fishermen who are fishing at night. The first orthographic standard for writing Elven languages was constructed in the early 1900s by J. R. R. Tolkien.

Kibwengo wa Mwanga (Light elf)
Vibwengo wa Mwanga (Light elves)
Kibwengo wa Giza (Dark elf)
Vibwengo wa Giza (Dark elves)

Katika mpito wa wakati, vibwengo wamehamia mahali kwengine duniani na makabila yalipotengana, walipata kubadili sura yao kulingana na mazingira walimokuwepo. Vibwengo wa mwanga ni viumbe wanaopenda amani na mazingira ya asili wenye macho yanayong?aa, nyuso zinazong?aa kuliko jua na nywele ya dhahabu; wanaishi kwenye misitu yenye jua jingi na maziwa yenye miti. Ilhali vibwengo wa giza huwa na ngozi iliyokoza, wenye macho yanayoakisi mwanga na hujihusisha na uchawi weusi; wao huishi kwenye mapango yenye giza na kina kirefu chini ya ardhi.

Source: Swahili Land: Vibwengo (Elves)
 
Vibwengo (Elves)
An elf is a type of supernatural being, prominently featuring in traditional British and Scandinavian folklore. They usually have magical powers and are capricious and mischievous in human affairs. The word ?elves? is sometimes used as a general term for fairies.

these are imaginary beings by the way.

There has never been a record of it an Elf being born or found alive.
 
Kibwengo wewe.
Nakumbuka nikiwa Loleza kulikuwa na uvumi Kuwa wapo wanatokea makuburini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom