Hivi vazi la taifa limekwenda wapi?

Hivi vazi la taifa limekwenda wapi?

Teh teh teh!, ngoja wenyewe wakupe feedback, lol, Bongo kuna mengi, things are always not taken seriously

Bado Clouds Media wanalifanyia kazi...teh teh teh. Nchi hii haiishi vituko
 
serious wakuu...

nauliza vazi la taifa limeishia wapi?
 
Muulize kibonde ktk jahazi lake ndo uwa ana-pretend kujua kila kitu.
 
Hivi huu mchakato ulioanza kwa mbwembwe baada ya Nchimbi kuteua kamati iliyoongozwa na Malinzi umeishia wapi?

Je hiyo kamati bado inaendelea kulipwa?

Je Makala nae atawapa ulaji washikaji zake kwa kuteua kamati mpya?
 
ule ulikua upepo tu mkuu kuonesha tu kuwa wizara ina jambo la msingi inafanya.
ukitaka kujua kuwa ilikua ni usanii tu, mtandao wa "Vazi la Taifa" ulikua hauna content yoyote zaidi ya graphics tu ambazo hata hazivutii...sijui hata kama upo hewani siku hizi.
 
Nakumbuka Emannuel Nchimbi alishikia sana kidedea hii ishu,na ikafikia mahali kamati maalum ikaundwa na kuanza kuzunguka mikoani wakisema wanakusanya maoni ya wadau. Najiuliza ilikuwa ni siasa?au kuna fedha ilikuwa haina kazi na hivyo ikatafutiwa kazi au wameona ni upuuzi mtupu au Waziri kaondoka na ndoto zake?

Utafutaji wa vazi la taifa umefikia wapi kwa wenye taarisa watusaidie
 
Umenikumbusha kipanya.

kipanya_13_-_07_-_2012_20120716_2008650934.jpg
 
Bora uwakumbushe mkuu, wanaishia kututia aibu kwenye olimpiki kwa kuvaa suti wakati si vazi letu....
 
nchi hii kila kitu siasa...utasikia na hili lilikuwa siasa...wameshapiga fedha sasa hivi wananawa mikono na midomo
 
Bora uwakumbushe mkuu, wanaishia kututia aibu kwenye olimpiki kwa kuvaa suti wakati si vazi letu....

Awakumbushe wakati limezuka jipya la vitambulisho vya Taifa. Unaenda kugawa vitambulisho wakati hakuna mtiririko wa pasiport kwa familia kibao.
 
Huu ulikuwa ubunifu wa NCHIMBI KAONDOKA NAO
 
hakuacha file ofisini mtu mwingine akija alitumie?usikute fedha za hii kazi pia alikuwa anatoa kwenye mfuko wake wa shati
 
Tunashughulikia mambo muhimu ya Taifa...vazi baadae sana
 
Nakumbuka Emannuel Nchimbi alishikia sana kidedea hii ishu,na ikafikia mahali kamati maalum ikaundwa na kuanza kuzunguka mikoani wakisema wanakusanya maoni ya wadau. Najiuliza ilikuwa ni siasa?au kuna fedha ilikuwa haina kazi na hivyo ikatafutiwa kazi au wameona ni upuuzi mtupu au Waziri kaondoka na ndoto zake?

Utafutaji wa vazi la taifa umefikia wapi kwa wenye taarisa watusaidie

Hii nchi ya ajabu sana, haina kipaumbele kila kitu kinafanyika bila mpangilio na matokeo yake hatufiki.
Mfano mwaka huu kuna
  1. Mfano mwaka huu kuna sensa ya watu na makazi
  2. Vitambulisho vya uraia
  3. Vazi la taifa
  4. Kilimo kwanza
 
shshshshshsh hili swala lipo mahakamani! ebo!
 
wanaotengeneza katiba ni bora wakajitahidi kui-summarize isizidi kurasa 10 ili kupunguza hii tabia ya kuanzisha mambo mengi ambayo 99% yanaishia kwenye 'mchakato'.

Hili suala tangia mwanzoni niliamini halina maana na bado naamini mpaka mwisho halitaleta maana kwa vile utamaduni wowote duniani haukuwahi kubuniwa kwa watu kukaa vikao na kulipana posho!
 
Hii nchi ya ajabu sana, haina kipaumbele kila kitu kinafanyika bila mpangilio na matokeo yake hatufiki.
Mfano mwaka huu kuna
  1. Mfano mwaka huu kuna sensa ya watu na makazi
  2. Vitambulisho vya uraia
  3. Vazi la taifa
  4. Kilimo kwanza

5. Operation Ziba Mdomo Mabwepande
 
Posho hakuna ndo maana mchakato umesimama
 
Back
Top Bottom