Hivi Upweke umri wake mwisho lini ?

Hivi Upweke umri wake mwisho lini ?

Mtu anatakiwa aolewe akiwa na umri gani?
Ukishajua ni maana ya ndoa,ukishaelewa maana kiapo cha ndoa, ukishajua nafasi yako kwenye ndoa na familia na ukishajua nini maana YA MWALI (Ile ya miaka ile) basi upo tayari kuolewa. Sio upwiyange weeee then unaona jioni jua linazama ndio unaanza kutafuta ndoa, wakati bado kwenye tabia zako hujafanya marekebisho unanza kuwasumbua wachungaji na waganga kumbe wewe ndio tatizo.

Upweke ni real kabisa na ndio maana tatizo la mental health limekuwa kubwa sana na kila siku linaongezeka. Kuna wengine wanajifanya kuiponda ndoa kwenye makombano/warsha, majukwaa na social media ili waonekane strong wapo huru, ila jua likizama wakiwa wenyewe ndani wanajutia kukosa ndoa. Wengine watakumbia kwani lazima mtu aingie kwenye ndoa, ila ndoa muhimu sana, zina changamoto zake ila ni kitu muhimu mno, ukilitizama kwa jicho la kiroho.

Ndio maana wengine hukimbilia vilevi,kusafiri sehemu mbalimbali, kula bata ila wakikaa chini wenye majumbani mwao pamoja na hela zao wana experience upweke. Ndoa haijawahi kuwa mbaya na haitokuja kuwa mbaya,sema jamii yetu imeharibu mifumo ya kijamii ya kuwaanda vijana kwa maisha ya ndoa, social media, tamaa ya kutaka makubwa ,siku hizi Madaktari wa Saikolojia wanapiga hela kupitia tatizo hili la upweke, kwani lina impact kubwa kwenye swala la afya ya akili.
 
Back
Top Bottom